Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jimbo la Lushoto lina zaidi ya shule za msingi 33 nasekondari 26 za Serikali, lakini katika shule hizi kuna changamoto nyingi kama:-
(i)	Ukosefu wa nyumba za walimu wa shule ya sekondari na msingi;
(ii)	Ukosefu wa hostel katika sekondari zetu;
(iii)	Fedha za ukarabati wa shule za msingi za Kilole, Kwemashai, Malibwi, Kwembago, Ngulwi, Ubiri, Milungui, Kwemakame na Yogoi;
(iv)	Kumalizia maabara zilizojengwa kwa nguvu za wananchi;
 
(v)	Upungufu wa walimu wa shule ya msingi na sekondari;
(vi)	Walimu kutolipwa posho zaonakuwekewa miundombinu rafiki;
(vii)	Watumishi kutopandishwa madaraja; na
(viii)	Ukosefu wa fedha za kumalizia maboma yote ambayo hayajakamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kuwasilisha.