Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Donge
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. SOUD MUHAMMED JUMAH: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais katika hotuba yake amesisitiza kuziendeleza na kuhifadhi maliasili za nchi. Katika kumuunga mkono  na  ili  kumsaidia  kufikia  malengo  ni  vyema changamoto za sekta za maji, ardhi, kilimo na mifugo ambazo zinachangia moja kwa moja uharibifu wa maliasili zishughulikiwe kwa ushirikiano wa kisekta.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, ripoti ya Mawaziri saba kuhusu ardhi iletwe Bungeni na kujadiliwa, kwani kuna michango mizuri ya kujenga kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba Serikali iwe makini katika kumega hifadhi na mapori ya akiba kwa lengo la utatuzi wa changamoto za sekta za ardhi, mifugo na kilimo. Huu hauwezi kuwa ufumbuzi wa kudumu.