Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. DUA  W.  NKURUA:
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  ahsante  sana  kwa kunipa nafasi ili niweze kutoa mchango wangu katika Wizara hii ya TAMISEMI. 
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  awali  ya  yote,  nitumie  nafasi  hii  kuwashukuru sana  wananchi  wa  Jimbo  la Nanyumbu  kwa  kunifanya  kuwa  kiongozi  wao kama  Mbunge  na  kuwa msemaji  wao  katika  eneo  hili,  nawashukuru  sana. (Makofi)
Mheshimiwa   Naibu   Spika,   nitumie   fursa   hii   kumpongeza   Rais   wetu Mheshimiwa  John  Pombe  Magufuli,  kwa  kazi  kubwa  anazofanya    ambazo  kila mtu mwenye dhamira ya kweli katika nchi yetu ni lazima amuunge mkono, kwa sababu analengo la kuwafanya Watanzania waishi maisha mazuri na Tanzania iwe sehemu salama ya kuishi watu.  Nampongeza sana Rais wetu. (Makofi) 
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  sasa  nataka  nianze  kuchangia  katika  suala  la elimu. 
MHE. DUA W. NKURUA:
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Katika suala  la  elimu  ni  dhahiri  kwamba,  mkakati  ambao  umekuja  na  TAMISEMI unaonesha  una  dhamira  ya  kweli  ya  kupambana  na  hali  halisi  tuliyonayo  sasa hasa  ya  mfumuko  kwa  watoto  ambao  wamezalishwa  utokana  na  tamko  na Sera ya CCM inayotamkwa kwamba, sasa elimu itakuwa bure. 
(Makofi)
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  katika  hali  kama  hii  ni  lazima  Serikali  ijipange vizuri  kuhakikisha  kwamba  yale  mambo  ya  ziada  ambayo  lazima  yaongezeke Serikali  ianze  kuweka mkakati.  Kwa  sababu  tuna  ongezeko  kubwa  la  watoto tutahitaji Walimu wengi, tutahitaji nyumba nyingi za Walimu, tutahitaji madarasa ya kutosha kwa ajili ya kuweza kukabiliana na hawa watoto. 
Mheshimiwa Naibu Spika, katika hali hii tusiziachie Halmashauri peke yake kujenga  nyumba  za  Walimu  na  kuongeza madarasa,  kwa  sababu  mapato  ya Halmashauri  nyingi  nchini  ni  madogo  sana.  Kwa  hiyo  lazima  Serikali  ije  na mpango utakaozisaidia Halmashauri kujenga nyumba za Walimu, madarasa na vifaa  vingine.  Waziri  atakapokuja  aje  na  mkakati  akaotuonyesha  kwamba tumejiandaa  kukabiliana  na  ongezeko  kubwa  la  watoto  katika  mashule  yetu. (Makofi)
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  sehemu  ya  pili,  ni  kuhusu  suala  la  maji,  maji  ni tatizo katika nchi yetu hasa katika Jimbo langu la Nanyumbu.  Kutokana na hali halisi ya mazingira na uoto 
tuliokuwa nao maji ni tatizo kubwa sana. Nashukuru bajeti   hii   imejitahidi   kuonesha   mikakati   mbalimbali   katika   nchi   nzima   ya kupambana na shida ya maji, lakini naiomba Serikali iweke mkakati maalum na wa  kipekee,  kuliondoa  tatizo  la  maji  katika  Mji  wa  Mangaka  ambapo  ndiyo Makao Makuu ya Wilaya na Nanyumbu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Mtwara kwa ujumla una shida kubwa sana ya maji, naomba Serikali ijipange kama ambavyo imeshatoa maelezo na nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba, wananchi wa Tanzania wanapata maji ya kutosha ili waweze kufanya shughuli zingine za kiuchumi. (Makofi)
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  kuhusu  maslahi  ya  Madiwani  na  Wenyeviti  wa Halmashauri  za  Vijiji.  Waheshimiwa  Madiwani  wanafanya  kazi  kubwa  sana katika  maeneo  yao  ya  kazi,  kila  tatizo  linalotokea  katika  maeneo  yetu,  watu ambao  wananchi  wanakwenda  kuwafuata  moja  kwa  moja  ni  Madiwani.  Kwa hiyo,   Madiwani   ni   lazima   tuwatengenezee   mkakati   utakaowapa   maslahi yatakayoweza  kusaidia  kukabiliana  na  kazi  ambazo  zinawakabili  kwa  sasa. 
Naomba  maslahi  ya  Madiwani  yaangaliwe  na  Wenyeviti  wa  Vijiji  walipwe mshahara.    Mkakati  huu  lazima  uanzie  huku  Serikali  Kuu,  Halmashauri  hazina uwezo huu ambao tunauzungumza leo. 
Naomba  Serikali  iwalipe  Wenyeviti  wa  Vijiji  nao  ni  watu  wanaofanya  kazi kubwa  sana  k
atika  nchi  yetu,  tusipowaangalia  hawa  tutakuwa  hatutendi  haki. 
Naomba suala hili tulipe kipaumbele. 
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nichangie asilimia 10 ambayo inapaswa iende  kwa  Vijana  na  akinamama,  ni  kweli  Halmashauri  nyingi  nchini  hazitengi pesa  hii, hata  kama  zinapata  mapato  haya  lakini  hazipeleki  asilimia  10  ya mapato  yao.  Naomba  tutengeneze  mpango  ambao  utakuwa  endelevu  na mpango  ambao  utazifanya  Halmashauri  ziweze  kutimiza  hiki  kigezo,  kwa  sasa kuna mambo yanawashinda kufanya hii kazi ambayo tumewapa waifanye. 
Mheshimiwa Naibu Spika,  tukumbuke kwamba, asilimia 60 ya mapato ya ndani  ya  Halmashauri  yanatakiwa  yaende  kwenye  miradi  ya  maendeleo, asilimia  20  ya  mapato  ya  Halmashauri  ya  ndani  yanatakiwa  yaende  kwenye vijiji,  asilimia  10  iende  kwa  wanawake  na  vijana.  Asilimia  10  peke  yake  maana 90  tayari  tumeshazigawa,  kumi  peke  yake  ndiyo  ifanye  kazi  zingine  ikiwa  ni pamoja  na  posho  za  Madiwani,  kuendesha  vikao  na  kadhalika.  Kwa  sababu OC ambayo ingekwenda kule kusimamia posho za Madiwani na vikao haziendi kwa  wakati.  Kwa  hiyo,  inalazimu  Halmashauri  zitumie  pesa  ambazo  zingeweza 
kwenda kwa akinamama na vijana. (Makofi)
Mheshimiwa  Naibu  Spika,    kama  tunataka  kweli  wanawake  na  vijana wapate  pesa  ni  lazima  Halmashauri  zetu  tuziongezee  pesa,  hii  asilimia  10 tuliyowapa  ni  ndogo,  tukumbuke  kwamba  Halmashauri  zinalipa  mchango  wa ALAT-Taifa,  Halmashauri  zinalipa  mchango  wa ALAT-Mkoa,  Halmashauri zinalipa loans  board, asilimia 10  ile  ndiyo  inafanya  hiyo  kazi,  katika  hali  hii unatekeleza vipi hili agizo, ni vigumu. (Makofi)
Mheshimiwa    Naibu    Spika,    tutakwenda    kuwalaumu    Waheshimiwa Wabunge   hapa,   Madiwani   kule,   tutawalaumu   Wenyeviti   wa   Halmashauri, tutawalaumu  Wakurugenzi  lakini  uhalisia  haitekelezeki.  Hao  Madiwani  ndiyo wanaosimamia  hizi  pesa  ambazo  tunazipeleka  kwao,  kikao  hakifanyiki  kwa sababu hawana pesa watasimamia vipi?
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  naomba  sana,  asilimia  10  iliyobaki  haiwezi kumudu  kuyafanya  haya  ambayo  tunataka  yafanyike,  mazingira  ni  magumu sana tumewatengenezea hao watu. 
(Makofi)   
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana tuheshimu bajeti, hapa tunajadili bajeti  na  hatimaye  itapita.  Naomba  sana  mambo  yatakayopitishwa  hapa yafanyike  hayo  hayo  yasiongezeke  njiani  wala  yasipungue  njiani.    Tuna  uzoefu wa  kutosha  kwamba,  mara  baada  ya  bajeti  yanatokea  maagizo  mengine ambayo Halmashauri sasa yanawachanganya.  Ni kweli maagizo yanakuwa na lengo zuri kwa mfano, tutengeneze madawati kwa watoto wetu ni jambo jema, 
lakini  halipo  kwenye  bajeti!    Tunawaambia    tujenge  maabara  ni  jambo  jema, lakini  haikuwa  kwenye  bajeti.    Kwa  hiyo,  kwa  sababu  haipo  kwenye  bajeti kinachotokea   hao   Waheshimiwa   Madiwani   na   Wakurugenzi   wanakwenda kuharibu mipango mingine ambayo ilipangwa. (Makofi) 
Mheshimiwa Naibu Spika, tuliwaambia kwamba, wao watenge asilimia 10 ya  mikopo  ya  akinamama  na  vijana  maana  tunalalamika  sana  Waheshimiwa Wabunge,   mikopo,   mikopo,   Wakurugenzi   hawatengi,   watatengaje   wakati wameambiwa  wapeleke  madawati  na  wamepewa deadline watafanya  lini! 
Wameambiwa  maabara  tarehe  fulani  iishe,  pale  kinachoendelea  mipango mingine baadaye, kipaumbele ni madawati na mabaara.
Mheshimiwa  Naibu  Spika  na  Waheshimiwa  Wabunge,  kama  tunaruhusu watu  waendelee  kupewa  maagizo  nje  ya  bajeti,  tukubaliane  kwamba  na asilimia 10 inaharibika tusilaumu, tunyamaze, haiwezekani! (Makofi)
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  naomba  sana,  kama tumekubaliana   na   hii   bajeti   twendeni   tuiheshimu.   Kule   Nanyumbu   tunao Viongozi   wa   Jadi   tunaita   Mamwenye,   wengine  mnaita   Machifu,   wengine mnawaita  Watemi.  Mamwenye  kwa  mila  yetu anaposimikwa  na  kufanyiwa sherehe, mtu wa kwanza kwenda kumuamkia ni Baba Mzazi na Mama Mzazi wa 
yule  Kiongozi.  Hii  ni massage kwa  watu  wengine  kwamba,  huyu  anapaswa kuheshimiwa  kuanzia leo.  Sasa,  kama  kweli  tunataka  bajeti  iheshimiwe mtu  wa kwanza    kuheshi
mu    bajeti    ni    Serikali.    Naomba    sana    Serikali    tuheshimu 
tutakayoyapitisha  hapa  ili  ikatekelezwe  kule  kwa  ufanisi  ambao  tumeutaka  na 
hapo tutakuwa tumetenda jambo jema.(Makofi)
Mheshimiwa  Naibu  Spika,  baada  ya  mchango  huo  nashukuru  sana  na 
naunga mkono hoja. 
(Makofi)