Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha mahitaji ya pesa shilingi 3,708,000,000 kwa ajili ya ukamilishaji wa miundombinu mbalimbali kama ifuatavyo:-
(i)	Elimu ya msingi maboma 56 kila moja shilingi 17,500,000 mahitaji ni shilingi 980,000,000;
(ii)	Elimu ya sekondari maboma 73 kila moja shilingi 20,000,000 na mahitaji shilingi 1,460,000,000;
(iii)	Matundu ya vyoo shule za msingi matundu 20 kila moja shilingi 1,500,000 na mahitaji ni shilingi 30,000,000;
(iv)	Matundu ya vyoo shule za sekondari matundu 17 kila moja shilingi 1,500,000 na mahitaji ni shilingi 25,500,000;
(v)	Maboma 32 ya Ofisi za Serikali za Mitaa kila moja shilingi 15,000,000 mahitaji shilingi 480,000,000;
(vi)	Maboma sita ofisi za kata kila moja shilingi 20,000,000 na mahitaji shilingi 120,000,000;
(vii)	Maboma matano ya zahanati kila moja shilingi 50,000,000 na mahitaji shilingi 250,000,000;
(viii)	Maabara tatu katika shule za sekondari kila moja shilingi 20,000,000 na mahitaji shilingi 60,000,000;
(ix)	Ukamilishaji ujenzi wa bwalo Sangabuye Sekondari mahitaji shilingi 10,000,000;
(x)	Maabara zahanati moja mahitaji ni shilingi 7,500,000;
(xi)	Ukamilishaji Kituo cha Polisi Nyamhongolo mahitaji ni shilingi 25,000,000;
(xii)	Ukamilishaji wodi mbili za wagonjwa kila moja shilingi 50,000,000 na mahitaji shilingi 100,000,000; na
(xiii)	Bweni la shule ya sekondari shilingi 20,000,000 mabweni mawili ya watoto wenye mahitaji maalum kila moja shilingi 70,000,000 na mahitaji ni shilingi 140,000,000.
Mheshimiwa Naibu Spika, msaada wa Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI ni muhimu sana kwa wananchi wa Jimbo la Ilemela; pili, naomba kilometa 12 za barabara za lami ahadi ya Mheshimiwa Rais tayari tumeshaainisha barabara husika kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Pansiasi kwenda Kiseke kilometa 3.2; na barabara ya Kahama kwenda Kayenze kupitia Nyamhongolo, Shibula, Bugogwa, Sangabuye hadi Kayenze kilometa tisa.
Mheshimiwa Naibu Spika, Manispaa ya Ilemela ina upungufu mkubwa wa watumishi katika idara mbalimbali kama ifuatavyo:-
NA.	CHEO/IDARA	MAHITAJI	WALIOPO	UPUNGUFU
1.		Elimu ya msingi	1943	1492	451
2.		Elimu ya Sekondari	1348	1107	241
3.		MEO ajira za kudumu	171	86	85
4.		MEO wa Mikataba	41	41	0
5.		Daktari Bingwa	6
	1	5
6.		Daktari	38
	25	13
7.		Daktari Msaidizi	44
	9	35
8.		Daktari wa Meno	2	1	1
9.		Daktari wa Meno Msaidizi	5
	1	4
10.		Afisa Muuguzi	30
	17	13
11.		Wauguzi	228	101	127
12.		Mteknolojia Maabara	20
	9	11
13.		Mteknojia Msaidizi Maabara	26	7	19
14.		Mteknolojia Mionzi	12
	4	8
15.		Mteknolojia Macho	5	0	5
16.		Mtaalamu wa Miwani	4	0	5
17.		Afisa Muuguzi wa Macho	7	0	7
18.		Mteknolojia Msaidizi Dawa	46	1	45
19.		Afisa Afya Mazingira	54	24	30
20.		Msaidizi Afya	111	41	70
21.		Tabibu Msaidizi	48	6	42
22.		Jumla 	4460	3189	1271
Mheshimiwa Naibu Spika, upungufu wa watumishi ni mkubwa sana ningeomba Wizara ione namna ya kutuongezea watumishi ili kupunguza adha hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.