Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutupa fedha nyingi za miradi ya elimu, afya, miundombinu ya barabara, umeme, maji pamoja na kilimo na kadhalika. Nikisema niyaandike yote, nitaandika kwa wiki moja na bado nitakuwa sijamaliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, itoshe kuendelea kumwombea Rais wetu Mwenyezi Mungu aendelee kumpa siha njema, pamoja na umri mrefu ili azidi kuwatumikia Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto ndogo ndogo zilibaki kama vile barabara hasa za TARURA. Pamoja na kwamba barabara hizi zinatengenezwa kila wakati, lakini kwa kuwa barabara hizi zinatengenezwa kwa changarawe, ndiyo maana zinaharibika mapema hasa kwa Wilaya ya Lushoto ambao mvua haziendi mbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba TARURA itengewe fedha nyingi ili iweze kujenga kwa kiwango cha zege hasa maeneo korofi, hasa barabara hizi zifuatazo; Malibwi - Kwekanga hadi Makole; Mbula - Kwemashai hadi Gare; Ngwelo – Mlola - Makanya hadi Milingao; Milungui - Masange hadi Kwesine; Migambo - Kwaboi hadi Kwai; na Kwemakame - Ntambwe Mazumai hadi Baga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa sekta ya afya, vituo vinavyohitajika kwa sasa ni pamoja na Kituo cha Afya Gare, Kituo cha Afya Malibwi na Kituo cha Afya Makanya pamoja na zahanati kwenye baadhi ya vijiji sambamba na watumishi wa kada zote pamoja na gari la wagonjwa katika hospitali ya wilaya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa elimu ni kama ifuatavyo: Shule Kongwe ya Makanya, Shule ya Msingi Kwai, Shule ya Msingi Kwemashai, Shule ya Msingi Kigulunde, Shule ya Msingi Makole, Shule ya Msingi Mshizii, Shule ya Msingi Chumbageni Ngulwi, Shule ya Msingi Kitopeni, Shule ya Msingi Mbula 'A', Shule ya Msingi Ubiri, Shule ya Msingi Lushoto, Shule ya Msingi Ntambwe, Shule ya Msingi Kwekanga, Shule ya Msingi Mziragembei, Shule ya Msingi Mzimkuu, Shule ya Msingi Mavului, Shule ya Msingi Mbogoi, Shule ya Msingi Mlola, Shule ya Msingi Kwaboi, Shule ya Msingi Milungui, Shule ya Msingi Mkuzi, pamoja na nyumba za walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa sekondari, changamoto kubwa ni maabara zilizojengwa kwa nguvu za wananchi, ni za kumalizia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mamlaka ya Mji Mdogo wa Lushoto tangu ianzishwe haijakabidhiwa vyanzo vyake vya mapato hadi sasa ukizingatia ni zaidi ya miaka 14 tangu ianzishwe. Naiomba Serikali yangu tukufu, isimamie hili ili mamlaka ya Mji wa Lushoto iweze kusimama yenyewe bila kutegemea Halmashauri husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hayo, Lushoto ina changamoto ya soko la kisasa, kwani lililopo ni la zamani na limechakaa mno.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natanguliza shukrani zangu za dhati kwako kwa namna unavyotuongoza vyema tena kwa weledi mkubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho na siyo kwa umuhimu, nampongeza sana Eng. Seff kwa hekima na busara aliyojaaliwa na Mwenyezi Mungu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.