Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Dorothy George Kilave

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Temeke

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimshukuru Mungu kwa afya na uzima niliokuwa nao. Naomba nimshukuru Mungu kwa afya ya Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan. Hakika Mwenyezi Mungu amempatia uzima na afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Rais Samia kwa kazi nzuri na kubwa kwa manufaa ya nchi yetu nzima ambayo ni mengi yamefanyika na ya kuridhisha kwa miaka minne. Ni kazi kubwa sana katika afya, elimu, miundombinu, nishati na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi sana, Rais ameimarisha amani ndani ya nchi yetu. Namshukuru sana Rais kwa kazi nzuri ya Jimboni Temeke, hakika ndani ya jimbo letu limeongezeka kwenye sekta ya elimu, madarasa ya shule za msingi yameongezeka, lakini shule za sekondari nazo zimeongezeka. Naomba sasa Shule ya Sekondari ndani ya Kata ya Makangarawe na Kata ya Chang’ombe tuweze kumaliziwa ili kata zote 13 ziwe na sekondari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye sekta za miundombinu tunashukuru TARURA wamefanya kazi nzuri, lakini naomba sana kuhusu Mradi wa DMDP uanze kazi mara moja kwani mikataba imeshasainiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Sekta ya Afya Wana-Temeke tunashukuru sana, kazi nzuri imefanyika na bado zinaendelea. Nampongeza Rais wetu na kuipongeza Wizara ya TAMISEMI kwa kuendelea kumsadia Rais kwa uaminifu. Wanatemeke tunamwahidi Rais wetu ambaye ndiye mgombea pekee wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi kura za kutosha za Wanatemeke atazipata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru Wizara ya TAMISEMI wote wakiongozwa Mheshimiwa Waziri Mchengerwa, Wanatemeke tunawashukuru na kuwaombea sana, Mungu awabariki kwa kuwatumikia Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napenda kumshukuru Mungu ametujalia afya mimi na Wanatemeke. Namshukuru sana Mungu kwa afya ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumpongeza Rais Samia kwa kazi nzuri na yenye tija na ufanisi kwa wananchi wote wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu kwa kazi nzuri na kubwa sana inayoendelea kufanyika ndani ya Jimbo la Temeke. Kwenye sekta amegusa kwa uwezo mkubwa; afya, miundombinu, nishati, na elimu nampongeza sana Rais wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Wizara ya TAMISEMI chini ya Waziri Mheshimiwa Mchengerwa na Naibu Mawaziri wote wawili na Makatibu wa Wizara na watendaji wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kazi nzuri ndani ya Jimbo la Temeke. Kwenye afya tumepata vituo vya afya vitatu. Kwenye miundombinu, barabara za TARURA tunashukuru, tunaomba sasa Mradi wa DMDP uanze kazi mapema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu nishati, umeme umepungua katika kukatikakatika na mengi sana ambayo yamefanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa Shule ya Sekondari Kata ya Makangarawe na Kata ya Chang’ombe ipewe kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kwa kuiweka nchi yetu kwenye amani. Ahadi yake kutoka kwa Wanatemeke ni kumpa kura za kishindo wakati wa kumchagua tena kuongoza miaka mitano mingine, kwani atakwenda kufanya kazi nzuri zaidi kwani kwa hii miaka minne amefaya kikubwa, je, tukimwamini tena? Hakika tutasonga mbele sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)