Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru kwa miradi mingi ya sekta ya elimu nchini na Jimbo la Iringa Mjini. Sasa kipekee kwa mara ya tatu naomba suala la ujenzi wa Shule ya Msingi Nduli iliyopo ndani ya Uwanja wa Ndege wa Iringa ihamishwe ndani ya uwanja wa ndege ikajengwe eneo lingine kama ilivyopangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa ndege kubwa zimeanza kushuka katika uwanja wa Iringa na shule iko ndani yake. Usumbufu ni mkubwa kwa watoto, lakini shule imechakaa sana, inaweza ikaleta madhara makubwa wakati wowote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba wodi za kujifungilia wanawake katika vituo vya afya viwili vya zamani ambavyo vinahudumia zaidi ya wananchi 20,000, Kituo cha Afya Ipogolo na Ngome. Naomba suala la machinjio ya kimkakati na ya kisasa Ngelewala Iringa Mjini, ikamilishwe ili ifanye kazi kama machinjio ya kisasa kama ilivyokusudiwa kwa kuongezewa shilingi bilioni 1.9 ili kukamilisha, kwani miundombinu imeshakamilika tayari kwa kuuza nyama nje na kuhudumia watalii hasa ukizingatia Iringa Mjini ni lango la utalii Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunashukuru kwa fedha za ujenzi wa jengo la utawala ambazo tumeanza kupewa, basi zije zote twende haraka haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niliomba kupewa fedha za ujenzi wa barabara eneo la Wilolesi kupitia TARURA takribani shilingi bilioni 1.6 za dharura ili kupisha msongamano kwenye barabara kubwa ya Iringa inayokatisha katikati ya Mji wa Iringa. Tumekuwa tukipata sana ajali kwa vyombo vya moto kama bajaji na bodaboda kwa ajili ya msongamano wa malori mengi katikati ya mji.