Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa jitihada kubwa za kufanya nchi yetu iongeze watalii, potential ya kuongeza watalii ni kubwa, nchi imebarikiwa ina vivutio vya kila aina kwa hiyo, ni Wizara kuwa creative zaidi kila wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Waziri, Mheshimiwa Balozi Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri na timu yetu. Leo sitakuwa mkali sana kwa sababu ya tukio walilofanya asubuhi la ile GN, Serikali yetu ni sikivu, wanapozungumza wananchi wanachukua hatua haraka sana. Kwa hiyo, kwa kweli, leo tena ninawaombea warudi kabisa kwenye Bunge lijalo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utalii na uhifadhi ili uwe mzuri ni lazima ujali haki za wananchi na kwa sababu tumepata uhuru ni vyema watu wetu wanaohifadhi wakawa wanafahamu kwamba, Watanzania hawa ndiyo wahifadhi namba moja na kila wakati ni vyema kujenga mahusiano zaidi, ili tulinde maeneo yetu ya hifadhi, lakini Watanzania wakiwa wana furaha. Siyo kuwa, wapoteze mali zao, ama mifugo yao, ama maisha yao kutokana na wanyamapori. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipindi karibu cha miezi miwili, mitatu hivi, Watanzania wa Kiteto karibu watano wamepoteza maisha kwa sababu ya tembo huko mashambani. Watanzania hawa ambao wanahangaika kila wakati kulima hawalali usiku na mchana. Tembo wamekuwa ni kadhia kubwa na binadamu wanapopoteza maisha kwa sababu, si sawa. Kwa hiyo, kila wakati waongeze nguvu na teknolojia, ili Watanzania hawa wasipoteze maisha, kwa ajili ya tembo hawa. Vijiji vya Makame huko wameshafariki wananchi karibu watatu, Ndorokoni, Ndaleta, Olpopong’I, karibu kila mahali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, ni vyema kila wakati timu zenu zikawa quick ku-respond kwenye vitu kama hivi, lakini ni lazima nimpongeze Naibu Waziri, amekuwa very quick kujibu meseji kila wakati na ametuma timu hata kuna tembo mmoja ameshauawa, ambaye ni mkorofi sana, tunashukuru, kila wakati wawe wana-respond, lakini bado kuna mmoja anasumbua sana. Wananchi wamesham-identify kwa mkia wake, ninasikia ana mkia mfupi hivi, sasa wanapopata taarifa hizi na wao wawe quick kufanya hivyo ili tuendelee kuokoa maisha ya binadamu. Wananchi wetu wanahangaika, kila wakati wanapopoteza mazao yao, siyo sawa. Hatutaki tuwatengeneze Watanzania wanaokuwa maskini kwa sababu ya kupoteza mifugo yao, mazao na maisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la fidia limezungumzwa hapa, sheria zetu hazipo vizuri sana kwenye kutoa fidia, inaitwa kifuta jasho, lakini hata hicho kifuta jasho hakiji. Kwanza, inachukua muda mrefu sana, kesi za Kiteto zimeshaletwa, fomu zaidi ya 300, lakini fidia haziji kila wakati. Mheshimiwa Waziri kuna kesi ya Mahakama, kesi ya Lenina, nimeshazungumza ni kesi za Mahakama Kuu, hukumu ya mwisho ya 2020 mpaka leo. Wananchi hawa Mahakama ilishawapa haki yao, lakini mpaka leo hawajalipwa na Mheshimiwa Attorney General, I am very glad unanisikiliza; hizi hukumu za Mahakama, Mahakama zinapofika mwisho na kutoa hukumu wananchi wapate haki zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri. Mheshimiwa Waziri tafuteni mpango wa mtu anapofanya kosa ng’ombe wakaingia kwenye maeneo haya, badala ya kuwakamata na kukaa nao watengeneze namna ya ng’ombe kukaa nje ya hifadhi waendelee kuhudumia watu kwa sababu, ni vyakula vya watu. Sasa leo hivi ng’ombe wakitoka wakaenda kwenye hifadhi na wakawakamata, ndama wanabaki nyumbani na sisi tunasubiri tunywe maziwa jioni. Kwa hiyo, tusubiri kweli miaka mitatu ndio tunywe maziwa! Kweli? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninadhani Mheshimiwa Waziri kwa sababu yeye ni wakili, kwenye eneo hili lazima wafanye vizuri zaidi, tudumishe mahusiano. Ukikamata ng’ombe wangu, kwani ukisema wakae kijijini wakati wanaendelea na kesi na huyo asiondoke, kwani kuna shida gani? Ukishinda si utakuja kuwachukua? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo suala ya WMA, Wabunge wengi wameongea hapa na Kamati ya Bunge imezungumza kwamba, pesa za WMA ziende haraka. Wewe imagine tu, wao wana-struggle baada ya zile hela kwenda Hazina, lakini angalau wanapata mshahara, si ni kweli?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi ni pesa tu za operation zina-frustrate mambo mengi, ndiyo maana wanataka pesa zirudi. Sasa imagine za WMA, za mishahara, za operation, zote zipo kule ni kwa sababu, tulishatengeneza Kanuni za WMA na wakaandika vizuri, kila mtu apate chake kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kipindi ninafikiri wao walikuwa wakiomba hizo fedha zitoke Hazina, kuna kipindi nilikuwa ninataka zisitoke, ili na wao wapate joto kidogo. Sijui ndio ile akina Mheshimiwa Shangazi wanasema ubaya ubwela ili na wao wapate pinch, ili waelewe kwamba, pesa zinaweza zika-frustrate mambo yasipoenda vizuri na Waziri ni Wakili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo WMA ikiingia mkataba na mwekezaji halafu anayeweka hela ni mwingine, halafu huyu anashindwa ku-meet zile obligations za mikataba eti kwa sababu, pesa zipo mahali. Waziri wa Fedha, kama yupo hapa, pesa za WMA haziruhusiwi kwenda Hazina, hizi ni pesa za wananchi, ile cut inayooenda maliasili, pengine nwao ndiyo wapambane huko, lakini za WMA zinatakiwa ziende moja kwa moja kwenye WMA.

MWENYEKITI: Ahsante. Muda wako umeisha, malizia.

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, haya. Basi kwa kuwa, leo nina furaha, ninaunga mkono hoja na niwatakieni kila la heri. (Makofi)