Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi. Awali ya yote ninapenda nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa fursa hii ya jioni hii ya leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesimama hapa sana kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ambayo ameifanya kwenye Jimbo langu la Bunda Mjini, hasa kwenye Kata ile ya Nyatwali. Wananchi wa kata ile wameishi pale zaidi ya miaka 30 na sintofahamu kwa sababu wamekuwa wakiishi pale hawajui kama wataishi pale ama watahama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuja kutatua changamoto hiyo. Amelipa zaidi ya shilingi bilioni 50 kwenye Kata ya Nyatwali na wananchi wale wote wamepata malipo yao. Kilichobaki ni fedha ndogo ndogo kwa ajili ya kuhamisha makaburi na fedha hizo zipo kwenye halmashauri yetu. Wiki iliyokwisha wananchi waliokuwa wamebaki zaidi ya wananchi 40 fedha zao zipo na sasa hivi wanaendelea kulipwa kama kawaida. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa sababu ametatua changamoto hii kubwa ambayo imewasumbua wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini kwa muda mrefu na wamekuwa wakiishi katika maisha ambayo kwa kweli walikuwa hawajui kwamba wanaanza vipi na wanamaliza vipi. Kwa kweli Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sehemu ya kutatua changamoto za Watanzania. Ametatua changamoto hii kubwa ambayo ilikuwa inatukabili kwa muda mrefu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho ni kuhusu kuiomba Wizara ya Maliasili na Utalii. Halmashauri yetu ya Mji wa Bunda ilitoa eneo la kujenga Ofisi za TANAPA Kanda ya Magharibi na wakawapa eneo bure na lipo na watu wa TANAPA wamepanga kwenye majengo ya wananchi wetu pale. Tunaiomba Wizara wawape watu wa TANAPA fedha kwa ajili ya kujenga ofisi zao za Kanda ya Magharibi kwenye Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa sababu eneo lipo. Wajenge na zile ofisi ndizo zitakazopunguza changamoto kubwa za wanyama kwenye maeneo hayo. Hata Wabunge wenzangu wanavyozungumzia kuhusu changamoto hizo wanazozipitia kwenye maeneo yao, ofisi zile zikijengwa pale Bunda Mjini changamoto nyingine zote tunazozizungumza zitakwisha kwa sababu kutakuwa na usimamizi madhubuti kwenye maeneo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Wizara ya Maliasili na Utalii, niwaombe na kwa sababu jambo hili tumekwishalizungumza hapa, leo ni zaidi ya miaka mitatu na lile eneo wamepewa zaidi ya miaka mitatu, lipo na lipo salama, halina mgogoro wa aina yoyote ile.  Kwa hiyo, waje wawekeze pale, wajenge ofisi zao pale, zitasaidia kutatua changamoto mbalimbali kwenye maeneo yale na kanda nzima ya maeneo hayo kwa ajili ya wananchi wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ili niweze kuchangia kwenye eneo hilo.  Ninaunga mkono hoja.  (Makofi)