Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema. Pia nimpongeze Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uchapakazi wake na jitihada za kuhakikisha anaendelea kutangaza na jitihada za kukuza utalii kwenye nchi yetu.  Niendelee kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara kwa uchapakazi wao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishauri Wizara kwamba kwa kuwa Mheshimiwa Rais amefanya jitihada kubwa kuhakikisha utalii wa nchi yetu unakuwa hivyo Wizara nayo ifanye jitihada kwa kushirikiana na Wizara ya Miundombinu kuhakikisha barabara zote zinazoingia kwenye mbuga zetu zinapitika mwaka mzima. Kwa mfano, barabara inayotoka Mandela kuingia kwenye mbuga yetu ya Saadani wakati wa mvua haipitiki kabisa. Hivyo Wizara iendelee kufanya jitihada.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia changamoto ya tembo kuendelea kuvamia makazi ya wananchi bado ni kubwa sana. Kwa mfano kwa Jimbo la Mkinga katika maeneo ya Mwanyumba, Mavovo mpaka Mwakijembe changamoto bado ni kubwa sana. Hivyo niiombe Wizara kuendelea kuchukua hatua zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaunga mkono hoja.