Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU:  Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawapongeza kwa kuimarisha utalii kusini na nchini. Kipekee kama Mbunge wa Iringa Mjini ninawashukuru kwa kuanza ujenzi wa Kituo cha Utalii Kusini, uwezeshaji wa kikundi cha ufugaji wa nyuki wa ukanda wa kijani toka Kata ya Kitwiru pamoja na mambo mengi mliyofanya. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Wizara ya Maliasili waharakishe ujenzi wa Kituo cha Utalii Kusini kinachojengwa eneo la Kihesa kilolo ndani ya Manispaa ya Iringa. Kwani, tayari Uwanja wa Ndege wa Iringa umepanuliwa na kuanza kazi, idadi ya watalii imeongezeka kitakwimu kusini. Hii inasababisha sasa watalii wengi kukosa sehemu ya kupata taarifa sahihi za utalii kusini. Hivyo, tunaomba sasa kituo hiki kikamilike mapema ili kutengeneza muunganiko wa utalii vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Wizara ya Utalii isimamie na kuendesha maonesho ya Utalii Kusini, ambayo huwa yanafanyika ndani ya Mji wa Iringa katika eneo linalojengwa kituo cha utalii kusini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaishauri Wizara ianzishe Maonesho ya Nyama Pori au Nyama Pori Festival. Sisi Iringa Mjini tuko tayari kushirikiana na Wizara katika Maonesho hayo ya Nyama Pori Festival.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba pia mradi mwingine ukitokea kama wa REGROW, basi eneo la Iringa Manispaa liwe linaingia kama lango la utalii kusini. Ili kuwaandaa wananchi wa Iringa kuupokea utalii kusini. Ninaomba pia ili kutunza mazingira mazuri ya utalii, basi uwezeshaji wa vikundi vya ufugaji nyuki viwe vingi ili kusaidia hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Wizara ishirikiane na wadau waliopo Iringa Mjini ili kukuza utalii na kutangaza utalii. Pia, wakati wa AFCON wasisahau kuleta watalii kusini. Ahsante ninashukuru na ninawasilisha.