Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na ninakushukuru kwa kuweza kunipatia fursa ya kuchangia kwenye Wizara hii ya Afya, Wizara ambayo ni muhimu sana kwa uhai wa Tanzania na zaidi kwa uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa kweli na mimi niwapongeze Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara kwa kazi ambazo wamezifanya. Nimepitia pia hotuba hii inatia matumaini kuendelea kuboresha miundombinu ya afya. Zaidi nimpongeze pia Ndugu yetu Dkt. Janabi kwa kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa WHO kwa Kanda ya Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipekee kabisa nimpongeze Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani ameonesha dhahiri kabisa amekuwa na political will ya kuweza kuboresha miundombinu ya sekta hii ya afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona na kweli tunatambua kwamba kipindi chake takribani hospitali tisa za kanda zimejengwa, hospitali za rufaa za mikoa takribani 28 ikiwemo Hospitali yetu ya Mwalimu Nyerere Memorial kule Musoma, Mara ambayo kwa kweli tangu tukiwa Bunge la 10 Mwenyekiti wetu akiwa Mheshimiwa Wasira hapa tumekuwa tukiiomba hiyo hospitali iweze kujengwa kipindi hicho ikiitwa Kwangwa. Sasa kwa kipindi hiki imeweza kujengwa na inaenda kukamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ni pongezi kubwa sana tunatoa na zaidi kwa kuboresha hiyo miundombinu ambayo imepelekea hata kuweza kuboresha zaidi huduma ya afya ya uzazi na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito kutoka 556 mpaka leo tunaongea ni 104 kwa vizazi hai 100,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni jambo kubwa na ni step kubwa ambayo imepigwa na tunatamani sana huko mbeleni tuwe na zero cases za mama wajawazito ambao wakati wakijifungua wanafariki. Kwa kupitia hii tumeona mpaka taasisi za kimataifa, kwa mfano Taasisi ya Gates Foundation iliweza kumpa hiyo The Global Goalkeeper’s Award. Kwa hiyo ninampongeza sana kwa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali yetu ya Rufaa ya Mwalimu Nyerere Memorial ya Mkoa wa Mara tunashukuru, lakini bado haijakamilika kwa 100%. Inahitaji takribani shilingi bilioni 18, sasa hivi tumepata shilingi bilioni nne tu kuweza kukamilika, lakini kuna wakandarasi ambao wame-stop. Kuna mkandarasi wa umeme wa TEMESA, mkandarasi wa lift na mkandarasi wa kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi wamesimama kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunahitaji fedha ziende ili hospitali iweze kuwekewa vifaa kwa ukamilifu. Mmetuletea vifaa ambavyo vinahitaji umeme, lakini havitumiki. Kwa mfano mortuary hai-operate, x-ray na mashine nyingine za kisasa hazi-operate kwa sababu umeme haujawekwa kwa ukamilifu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunaomba sana fedha ziende kwa sababu hii hospitali imeshaanza kufanya kazi iweze kusaidia wananchi wa Mkoa wa Mara. Ninaomba sana Mheshimiwa Waziri hilo muweze kulizingatia, fedha ziende kwa wakati ili hawa wakandarasi waweze kumalizia kazi zao ambazo wanaendelea kuzifanya pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika hospitali ile barabra ya kufika hospitali hii ni mbaya sana. TARURA walisema wangeweza kuitengeneza mwaka huu wa fedha, lakini hawajafanya, wameweka kwenye phase two. Tunaomba kama inawezekana mtutengenezee barabara ambayo inapitika kwa uhalisia kwa sababu ile ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ili waweze kutoa huduma ambayo ni bora zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, campus; jana aliongea Profesa Muhongo hapa, tulitaka campus ijengwe pale ya chuo kikuu. Ardhi imepatikana na kabla hatujatoa hiyo ardhi ekari 20, walikuwa wanasema fedha zipo zinahitaji ardhi. Tunaomba muweze kuongea na Wizara ya Elimu, kama fedha zilikuwepo za mradi, watujengee ile campus ya Chuo Kikuu cha Afya pale ndani ya Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuendelea kuna kijana anaitwa Edward Chimoi, huyu kijana amevumbua robot medical beds ambayo ina uwezo wa kumchukua mgonjwa akiwa katika level yoyote ile, anaweza kutembea, hawezi kutembea, ikambeba kutoka pale ikampeleka sehemu mbalimbali kwenye emergency, ICU, wodini na kwenye radiology na pia inapima kilo za mgonjwa. Ikikubeba inapima kilo za mgonjwa. Pia ametengeneza kifaa kingine cha gauze ambacho kina bend gauze, kama mtu amepata accident ina mawasiliano, ina-communicate.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa huyu kijana amewatafuteni, hebu muwezesheni, kitanda kimoja kina-cost almost sixteen million. Ametafutwa na watu wa nje ili aweze kuwapa code, nao wamefika bei mpaka ya shilingi milioni 200 aweze kuwapa huo ujuzi wamchukue, wampeleke nje, wakae naye miaka mitatu. Tusipomchukua tukamtumia sisi kama Watanzania, kama Wizara, akienda nje tutaishia ku-import hivyo vitanda kwa bei ghali zaidi, mtafuteni ameshawafikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niliona presentation yake akifanya kule Iringa kwenye kongamano la kisayansi kwa wauguzi, anasema kufanya hivyo atasaidia wauguzi wengi. Amesema amefanya tafiti wauguzi wengi wanalalamika migongo kwa sababu ya wanavyofanya ile pushing. Sasa hili robot litasaidia na lita-save time ya wauguzi ambayo wana-spend pale na mbaya zaidi au nzuri zaidi ni lile robot, anasema lina-memorize, linaweza hata likamkumbusha muuguzi kwamba ni muda gani mgonjwa anatakiwa kupewa dawa, linampunguzia muuguzi majukumu mengi, anabaki tu na ile patient operation care ya kawaida, anajua nitafanya hivi, lakini mengine mengi hiki kitanda cha robot kimeyachukua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuwaenzi hawa watoto wa Kitanzania ambao wamekuja na huu uvumbuzi tuweze kuwaendeleza na Serikali mnaichukua hiyo sasa inakuwa ni ninyi. Mnaweza mkawa mnauza hata nchi nyingine za nje vitanda hivi. Ninaomba sana mlizingatie hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni Sera ya Afya ya Taifa ya mwaka 2007 ambayo inasema inatoa huduma bure kwa mama wajawazito na watoto, ni muhimu sana. Nimetoka kusema hapa, dhamira ya Mama Samia na Serikali yake kuhakikisha tunakuwa labda na zero rate ya vifo vya mama na mtoto, nina imani kwanza Serikali mnatakiwa mfanye tafiti ya kina. Tunatambua kwamba kuna Watanzania wana uwezo wa kulipia hizi delivery kits, lakini kuna wengine hawawezi kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fanyeni utafiti wa kina muweze kugundua na mtambue kwamba hata maandiko matakatifu yanasema, nikirejea kwenye Mwanzo 1:28; “Mungu akawabariki na kuwaambia, zaeni muongezeke mkaijaze nchi na kuimiliki...” Sasa Tanzania tusigeuze wamama wajawazito kama vile ni adhabu, yaani leo nikipata ujauzito kama sina uwezo, sitaenda hospitali. Sina delivery kits that mean nitakaa nyumbani. Nitajifungua isivyo salama na ninaweza nikapoteza maisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana, fanyeni utafiti wa kina muweze kugundua na kupitia hata sensa, ile inachukua data za Watanzania. Wale ambao hawajiwezi kabisa wapeni nafuu, wawe wanakuja kujifungua for free. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama vile kwenye umeme walivyofanya, wa mjini wanaunganishiwa kwa shilingi 320,000 wa vijijini kwa shilingi 27,000. Fanyeni utafiti wa kina, wale ambao wanajiweza waje na delivery kits, wale ambao hawajiwezi Serikali iweze ku-take care, tuweze kutafuta hela sehemu nyingine zozote zile ambako kuna imani ya ubadhirifu wa fedha, ikaja kujazia Watanzania waweze kuokoka na kuijaza dunia na kuijaza Tanzania. Anaweza akawa mama amefariki na mtoto, labda anakuja kuwa Rais wa Tanzania. Tuokoe maisha ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine ninashukuru sana, nilitembelea mabanda, Wizara ya Afya mmeleta mabanda mbalimbali pale. Sasa katika kupita nikapata hiki kitabu, “Mtindo wa Maisha na Magonjwa Yasiyoambukiza.” Nimekisoma kwa muda mfupi tu jana usiku, baadhi ya maneno, ni kitabu kizuri sana. Pamoja na kwamba mnasema mnatoa elimu, mkitoa elimu siyo wote kwanza wenye TV! Pili, siyo wote wapo kwenye social media! Tatu, siyo wote wanasoma magezeti na nne, siyo wote wanasikiliza redio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, printing ya hiki kitabu tuhakikishe kila kaya inapata. Kama kweli tunataka tu-save nchi yetu iwe na watu wenye afya, namba moja ni kila kaya iweze kupata hiki kitabu, lakini haya magonjwa myaoneshe mengi na mseme; “tafiti ya mwaka 1986/1987 ilionesha katika watu hai 100, mtu mmoja alikuwa na kisukari na watu watano walikuwa na shinikizo la damu.” Tafiti ikaja mwaka 2012 ikasema, “katika watu 100 watu tisa kisukari, 26 shinikizo la damu.” Kuanzia mwaka 2012 nina imani hamjafanya mpaka sasa hivi. Mkifanya, it is worse, yaani ni mbaya zaidi na mmeonesha hapa mambo mbalimbali, vyakula, kutokufanya mazoezi na sijui pombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi ninaenda kwenye mawili tu kwa sababu ya muda na nitaomba uniongezee muda kidogo. Kwenye mazoezi tumekuwa tukiongea na nina imani wale wa vijijini wengi wako active naturally, lakini mjini. Mmeeleza hapa, kukaa sana, kutokufanya mazoezi na kufanya nini, hatuna miundombinu. Serikali muongee, Wizara ya Afya muongee na Wizara ya Michezo muweze kuweka viwanja, katika kila mtaa hakikisheni kuna sehemu za kukimbia. Watu wakitoka kazini waende wakimbie, kusema eti wanafanya mazoezi asubuhi, mimi ninaamka nikimbizane kwenda, kuna foleni, nitafanya mazoezi saa ngapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikirudi baada ya kazi nitajua kuna sehemu kwenye mtaa wangu. Nitaenda nitakimbia, nitafanya mazoezi, watu wajengewe hii culture. Wekeni miundombinu wezeshi kuweza kuwa-save Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija kwenye nyingine, wamezungumzia pombe. Tena hapa mmeweka pombe za kawaida kabisa, ila mkasema excessive pombe ina madhara mengi. Mmeainisha hapa, moyo, kongosho, sijui figo, kisukari, ini, ubongo, sijui nini, mengi. Utapiamlo na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa letu linateketea na uzazi na vingine. Taifa letu linateketea kwa pombe, achilia hizi ambazo mmeziandika hapa nzuri. Tumeshaongea mpaka huku Bungeni hadi Mheshimiwa Spika akaelekeza mkafanye uchunguzi, mlete tafiti za kina, vijana wanateketea kwa pombe ambazo nyingine ni fake, leo sitaji, siku ile nilitaja. Zinauzwa holela mpaka kwenye maduka ya chakula, mnasema sijui figo ni expensive, if we don’t prevent, definitely itakuwa expensive.

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hatutazuia pombe ambazo zinaleta magonjwa mengi tutatumia fedha nyingi sana kuwatibu Watanzania.

MWENYEKITI: Taarifa. Mheshimiwa Festo Sanga.

TAARIFA

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mbunge hodari kweli kweli wa Tarime, Mheshimiwa Dada Esther kwa mchango wake mzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge wengi tumezungumza hapa kuhusu bima ya afya kuchangia, tutatafuta fedha nyingi sana kuweka kwenye Mfuko wa Bima ya Afya na bima ya afya itawezeshwa, lakini mzigo tunaoutengeneza utakaotumia hiyo hela kwenye bima ya afya unaotokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye ilani mpya inaelekezwa, ukurasa wa 62, itakuwa ni changamoto kubwa sana, kama Wizara haitakuwa na mkakati wa kudhibiti pombe zinazoleta magonjwa ya figo na magonjwa tofauti tofauti kwa sababu mzigo wote wa fedha tunaoupeleka kwenye bima ya afya utaenda kuishia kwenye magonjwa haya, kama hatutadhibiti mapema.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Esther Matiko, umepokea Taarifa hiyo?

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaipokea in a very positive aspect. Ni kweli sasa hivi watu wanajituma ila tukija kuweka universal health coverage itakuwa ni bombshell kwa sababu tutakuwa tunatumia hela nyingi sana kutibu haya magonjwa. Kwa hiyo, tu-prevent, tuhakikishe tunadhibiti. Shirikianeni na Wizara ya Viwanda na Biashara, shirikianeni na mamlaka nyingine zozote, hizi pombe ziko mtaani, hata haziuzwi kwenye store ambazo zinatakiwa kuuza pombe, zinauzwa kwenye maduka ya vyakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawaua Watanzania, unakuta mtu anakunywa pombe, tunazika sana, labda ninyi hamziki. Mtu anakunywa pombe, tena siyo mpaka kwa figo, mwingine anakufa tu kwa sababu anakunywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu ameshikilia ki-energy drink, siyo energy drink that one! Bodaboda wengine, siyo energy drink, vijana wanakufa. Wengine wanakuwa hawali, wanakufa, Taifa linateketea. Tuwa-save, yaani kama nchi mnatumia mitutu ya bunduki kulinda mipaka ya nchi wakati ndani vijana wanateketea kwa vitu ambavyo Serikali mngeweza kuvifanya mkapunguza vifo vya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba sana, hii ni crisis, mui-take as a priority mhakikishe mnadhibiti pombe zote hizi na hata watu wanaouza rejareja. Wakikamatwa washtakiwe, watu wakinywa, wanywe kwa staha kwa mamlaka ambazo zimepewa leseni ambapo wanauza kwa mujibu wa taratibu na kanuni za nchi yetu. Ahsante sana. (Makofi)