Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya wananchi wa Ukerewe nitoe shukrani kwa kuanza kwa ujenzi wa hospitali ya rufaa ngazi ya mkoa jimboni Ukerewe, kukamilika kwa hospitali hiyo itakuwa ni mkombozi wa maisha ya wananchi wengi. Niombe yafuatayo:-
(i)	Majengo ya awali yaliyokuwa yanajengwa na SUMA JKT yaliyopo eneo la hospitali ya wilaya yakamilishwe haraka na kukabidhiwa halmashauri ili yapunguze shida ya miundombinu katika hospitali ya wilaya.
(ii)	Ifanyike tathmini ya majengo yanayotumika kwa sasa kama ofisi za halmashauri na kama yatakidhi basi kianzishwe chuo cha uuguzi na uganga kwa sababu pale tuna jengo jipya la halmashauri, litakapokamilika basi majengo haya hayatakuwa na kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la upatikanaji wa huduma za afya kwa makundi ya wajawazito na watoto bure kama ilivyo sera bado lina changamoto nyingi sana, naomba kushauri Wizara iwe na kitengo maalum cha kufuatilia utekelezaji wa sera hii ili changamoto zinazojitokeza kwenye eneo hili ziwe zinapatiwa ufumbuzi na kuondoa malalamiko mengi kwenye jamii na kuepusha vifo kwa makundi haya.