Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Nisiwe asiyekuwa na fadhila, ninamshukuru sana Mheshimiwa Waziri, kwa Ujenzi wa Masoko ya Kimkakati ya Kyerwa, Mlongo, lakini pia Mheshimiwa Esther Matiko ameomba pia niongelee Soko lake la Remagwa. Siyo kwamba yamekamilika, hapana hayajakamilika, lakini kuna ujenzi unaendelea. Kwa hiyo, ninaomba ni-reserve pia hizi shukrani mpaka yale masoko yakikamilika yakaanza kutumika. Hizo shukrani nitazileta rasmi kwa niaba ya wananchi wa Kyerwa na Tarime kama alivyoniongezea Mheshimiwa Esther. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasikitika sana kwamba Bajeti ya Kilimo imekuwa haitoki yote. Tunakuja hapa tunafurahia sana, tunasherekea sana, tunachekelea sana, lakini fedha haziendi kwa wakati. (Makofi)      
Mheshimiwa Mwenyekiti, unaweza ukawaza mtu afanye maajabu, atafanya maajabu gani kama fedha haijaenda kwa wakati? Kwa hiyo, nitoe wito na niongeze kupaza sauti. Ninaomba turudi kwenye commitment yetu za Malabo Protocol, kwamba 10% ya bajeti itengwe kwa ajili ya kilimo na siyo kutengwa tu, itengwe na ipelekwe kwa ajili ya kilimo. Hivi vilio vyote mnavyovisikia Waheshimiwa Wabunge wanavitoa hapa vya kuhusu wakulima wetu kutumia jembe la mkono, linaweza kufikia mwisho. Hakuna fahari ya mtu kutumia jembe la mkono, hakuna utajiri kwenye kutumia jembe la mkono. Sisi tumelelewa tumekua wazazi wetu wanatumia majembe ya mkono mpaka leo bado ni maskini lakini ni watu ambao wanafanya kazi kwa bidii, wanajituma sana, lakini utaongeza tija gani kama ni jembe moja moja yaani unahesabu jembe moja moja, kwa hiyo, kwa siku kama ni jembe 1,000 imeishia hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama tunataka tulete mabadiliko kwa 61%, Waziri ameeleza 61% ya Watanzania wameajiriwa kwenye kilimo, kama tunataka ku-empower the 61% ambao ni majority ni lazima tuboreshe kilimo kwa ku-mechanised agriculture. Ni lazima tuweke fedha za kutosha kwa ajili ya ku-boost uchumi wao. Vinginevyo itakuwa ni mark time tu na ndiyo maana tunaona mabadiliko hayaonekani kwa sababu ya wakulima wetu wengi bado ni maskini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Mtu wa Kyerwa nikisimama hapa cha kuongelea ni kahawa tu. Kahawa kwetu ni uchumi, kahawa kwetu ni maisha, kahawa ndiyo kila kitu. Nilikuja Bungeni hapa ninakumbuka kipindi fulani Mheshimiwa Hasunga akiwa Waziri, nikaeleza umuhimu wa kutumia minada katika kununua kahawa. Nilitoa mifano niki-cite hata mikoa kadha wa kadha ambayo ununuzi au uuzaji wa kahawa ni minada. Wengi sana walipinga bila kuelewa nilikuwa nasema nini. Ninashukuru sana Mheshimiwa Bashe na Serikali iliyokuwepo ilielewa mantiki ya kwa nini tunapaswa kutumia minada. (Makofi)   
   
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunavyotumia ushindani wa kiminada at least kuna unafuu wa bei tumeuona. Walienda mbali zaidi waliokuwa kwenye vyama vya ushirika, waliowahi kukutana na mimi wananitambia kwamba Anatropia kushinda uchaguzi hutatoboa kwa sababu tu nilisema ninataka minada na KBC waunde kampuni na wao washindane na wanunuzi wengine na hiki ndiyo kinafanyika na wakulima wetu wanafurahi sana. (Makofi)      
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sijui hofu yao ilikuwa ni nini kama leo kwenye soko ni win win situation.  Ninaomba nimwambie kitu kingine Mheshimiwa Waziri, pengine anakijua au hakijui. Kahawa zinazopita kwenye minada pengine ni robo kuliko nyingine zote ambazo haziingii kwenye minada, sijajua ni kwa kiwango gani atasaidia kudhibiti hiyo, lakini namna pekee ya kuwasaidia watu wa Kyerwa na mikoa inayozalisha kahawa kama Kagera na maeneo mengine ni kuhakikisha kila kahawa inayozalishwa inapita kwenye mnada na wanaonunua kwenye minada wanalipa kwa wakati. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu shida tuliyonayo, wananchi wanaanza kuwaza kwamba tukwepeshe kahawa ili tuweze kupata hela kwa haraka, kitu ambacho kinawadidimiza. Mheshimiwa Waziri, tafadhali tusitengeneze na tusikubaliane na ma-cartels ambao wanahakikisha kwamba watu hawauzi kahawa zao kwenye mnada. (Makofi)      
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali watazijuaje hizi tani? Leo Waziri anaeleza kwamba uzalishaji wa kahawa umepanda kutoka tani 58,000 mpaka 81,000, atajuaje kama hazipiti kwenye minada? Kwa hiyo ili tuweze kupata correct record, ili tuweze kupata the right revenue ili hata halmashauri zetu zikusanye cess ni lazima tu tupambane kahawa zetu zote zipite kwenye mnada, full stop. (Makofi)    
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine kabla sijaenda mbali zaidi, leo ninavyoongelea Kyerwa kuna wizi mkubwa wa kahawa. Watu wanavuna kahawa mbichi wasiokuwa waaminifu wanavuna kahawa mbichi, wanavuna mashambani usiku kucha wanawaibia wakulima maskini ya Mungu. Mtu amejiandaa zaidi ya miezi nane anasubiri kahawa, kahawa hazijaiva zimeshavunwa na watu wasiokuwa waaminifu. Unadhani wanauza wapi? 
Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu hana hata mti mmoja wa kahawa, hana shamba, hana mche, lakini anaenda kuuza kahawa, ni kwa nini tusiamini kwamba wafanyabiashara wanawashawishi watu wasiokuwa waaminifu kuvuna kahawa?  Nninachotaka kusema hapa, ni lazima kila kahawa inayonunuliwa iwe na source. Wewe kama ni mkulima umeleta kahawa utuambie umezivuna wapi, hiyo ndiyo namna pekee ya kuzuia wizi unaoendelea leo. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ninavyoongea, baba yangu wa zaidi ya miaka 80 amelazimika kutafuta watu wa kulinda kahawa zake na kama hawezi ku-afford kulinda kahawa anapaswa kujikongoja na yeye akalinde kahawa. Do you think that is fair? Siyo sawa. Ni lazima utaratibu utengenezwe, tuwe na source, umevuna wapi kahawa unazotaka kuuza. (Makofi) 
Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo la kwanza lakini jambo la pili, tumekuwa kwa muda mrefu na habari ya butura. Ni kwa nini mnadhani watu wanauza butura? Ni kwa sababu hawana fedha ya kujikimu kipindi chote wanasubiri kahawa ziive. Leo Mheshimiwa Waziri nikuongezee sifa, tumezindua Benki ya Ushirika. Kazi ya Benki ya Ushirika iwe ni benki ya washirika kweli ya wananchi, waweze kunufaika na benki yao kwa maana waweze kukopa, tulegeze masharti. Wasi-behave kama commercial banks ambao wao kuweza kukopesha mkulima ni story nyingine. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, benki tuliyonayo leo ya ushirika iweze kukopesha wakulima wadogo wadogo kwa dhamana hata ya miti yao ya kahawa, kwa sababu wanajulikana. Wafungue bank account, mashamba yanajulikana, hiyo ndiyo namna pekee ya kuzuia wao kuuza kahawa kabla ya wakati, lakini ndiyo suluhisho la wao kula butura. Kwa hiyo, nimwombe sana Mheshimiwa Waziri, hii benki iwepo kwa ajili yao, isiwe tu ni cosmetic kama benki zilivyo nyingine. (Makofi)      
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja nyingine ni kwa kiwango gani tumeweza ku-tap potential ya kahawa? Nikiwa ninazunguka nimepata fursa ya kuzunguka maeneo mengi duniani, na nina-feel kwamba sisi watu wa Kyerwa tunawezaje kuendelea kuwa maskini tumezungukwa na rasilimali kubwa kama kahawa. Hivi ni kweli sisi kahawa yetu kitu pekee kinachofanya ni kuweza kunywa na kula? Nika-google lakini pia nimeona kuna matumizi mbalimbali ya kahawa duniani na huko jimboni nimekuwa nikiwaambia ninasema, leo ninyi ni maskini lakini mmelalia uchumi mkubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikaona kahawa inafanya vitu kadha wa kadha ukiachana na kunywa. Kahawa bado inaweza kutengeneza kiungo, kahawa bado ni mbolea, kahawa inaweza kutengeneza keki, kahawa inaweza kufanya vitu kama cosmetics. Ninyi wote tunajua kuna scrub ambazo leo kwenye mtandao google scrub ya kahawa, ni moja kati ya scrub very expensive.
Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hiyo tu, Waheshimiwa Wabunge, ambao wamefanikiwa kusafiri na Ethiopian Airways, kuna kinywaji ambacho ni kizuri sana, kinaitwa Bottega, kiko kwenye ladha tofauti tofauti, hizo ni products zimetengenezwa na kahawa. Wao pia wana Amarula, they have their own brand wanaita Amarula Coffee Drink. Siyo hizo tu, ziko nyingi tu nitamtumia Waziri aone. (Makofi)      
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi tunawezaje ku-add value kwenye kahawa yetu? Tukaondoa, sisi kama wakulima wa mikoa ya kahawa tunachokiwaza ni kahawa zikiwa tayari, sisi tunakula, tunakausha tunakula kidogo, lakini baadaye tunawaza ku-export. Ni kwa kiwango gani tunaweza kuji-squeeze tuka-attract wawekezaji waka-add value kwenye kahawa, tukaondoka leo kuwa market driven, tukawa watu ambao tunaweza ku-add value na tukafaidika na kahawa yetu? Hayo ndiyo nilitaka niyaeleze (Makofi)      
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, Kyerwa bado ina potential kubwa sana. Zao letu haliwezi kuwa kahawa tu. Wabunge wote wanajua Mkoa wa Kagera ni ndizi, lakini ni kwa kiwango gani tumefaidika na ndizi? Niliwahi kueleza hapa Bungeni kwamba nilifanikiwa kwenda nchi fulani Ulaya, nimekuta kuna ndizi ziko imported kutoka nchi jirani ya kwetu sisi. Sasa sisi ni kwa kiwango gani tunaweza tuka-capitalize katika hizi ndizi tunazozilima na mind you, sisi hatulimi kwa tija, ukienda kwenye shamba letu huko Kagera, hatulimi tena kwa tija. Migomba kwanza haina kiwango kizuri kwa sababu tulikuwa na changamoto ya mnyauko kama ilivyo kahawa, mazao yamekuwa ni kama ni kilimo cha zamani. Tunahitaji kilimo cha kisasa cha migomba ili tuweze ku-add tija na ku-export. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hiyo tu, zao la vanila. Sisi eneo letu au Mkoa wetu una-attract vanila. Ninadhani Mheshimiwa Waziri unajua kesi ya vanila. Wakulima walishawishika kulima vanila, wakapambana kupata masoko. Waziri alieleza kwamba amefungua kiwanda, sijui kwa kiwango gani ameweza kuwasaidia ili waweze kuuza hayo mazao yao, lakini bado sisi eneo letu linaweza kuzalisha alizeti. Kwa hiyo, hayo ninaweza kueleza kwamba bado tuna potential ya kusaidia Mkoa wa Kagera. Bado tuna potential ya kuwafikia wakulima wetu ili waweze kunufaika na zao la kahawa, lakini na advantage ya eneo husika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho lakini siyo kwa umuhimu, hizi kahawa zimekuwa zikiwanyanyasa wananchi. Ninarudia, nimemwambia mara nyingi sana Mheshimiwa Bashe kwamba, ikifika msimu wa kahawa pamoja na wao kuwa na wizi wizi mdogo mdogo, kumekuwa pia na kunyanyasa wananchi kwa sababu eti wanavusha kahawa kwenda Uganda. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukweli ni kwamba, kama bei yetu ni nzuri kama ilivyokuwa 5,000, 6,000, 7,000, anavusha Uganda ili iweje? Soko letu likiwa zuri, wakulima wetu wakalipwa kwa wakati, hakuna atakeyevusha kahawa, lakini hivi vyote vikikosa, utegemee kwamba watu by nature watatafuta faida, tutayaona hayo mengine. (Makofi)   
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi. Mwisho lakini siyo kwa umuhimu, kumradhi. Nimeona Waziri ameandika kwenye kishikwambi kwamba “tutajenga Kituo cha Umahiri wa Maendeleo ya Kahawa Jijini Dodoma” inaitwa The Coffee Centre of Excellence. Hivi what, where, when Dodoma na kahawa wapi na wapi? Ninaomba m-cancel hiyo mipango yenu hii centre of excellence siyo lazima iletwe Kyerwa au kokote Kagera lakini ipelekwe kwenye mikoa ambayo ina-reflect uchumi unaotokea kwenye hilo eneo. (Makofi)   
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. (Makofi)