Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Eng. Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi hii ya kuchangia. Awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu, lakini kipekee kabisa nichukue fursa hii kuishukuru sana Serikali kwa mageuzi makubwa katika Sekta ya Kilimo nchini kwetu, hakika tumeyaona kuanzia miaka ya 90 kwa majina mbalimbali, kama watangulizi wangu waliozungumza wameweza kuyataja hapa, lakini commitment ya kweli ya yenye mikakati ya uhakika imetokea kufanyika wakati huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweka commitment ya kibajeti na kwa kupitia watendaji mahiri, kama kaka yangu Mheshimiwa Bashe pamoja na wasaidizi wake kwenye Wizara hii ya kilimo wakiongozwa na kaka yangu ndugu Mweli. Hakika wameweka mikakati inayokwenda kuonesha taswira ya kweli ya tunakoelekea kwenye mageuzi ya kilimo nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa shukrani nyingi za dhati, hakika tunakoelekea tunaona taswira kubwa. Mioyo yetu inafarijika kwamba, leo Tanzania badala ya mkulima kuwa na hofu ya kutegemea mvua itanyesha lini, tunakwenda kukimbia mvua zisizokuwa na uhakika, mvua haribifu; unakwenda kuchimba na kuwa na uhakika wa kumwagilia, hakika haya ni mageuzi makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutuwezesha Mkoa wa Tanga shilingi bilioni 11, kwa ajili ya mashine zile za mkonge. Mheshimiwa Rais amesema tusiziite tena korona, tunawashukuru sana, wamewajali wananchi wa Mkoa wa Tanga na hakika Serikali imesimamia kwa dhati zao hili la mkonge kuendelea kuwa la biashara Kimataifa. Tunatoa shukrani zetu nyingi sana, kwa ajili ya hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakika shilingi bilioni 11 zile zitasababisha kuzalisha mkonge wa grade ya juu kwa sababu, the more we delay kwa sababu ya kutopatikana mashine the more product inakuwa imepungua ubora wake. Kwa hiyo, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa commitment hiyo ya fedha nyingi ndani ya Mkoa wetu wa Tanga, tunashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba pia, nitoe shukrani zangu za dhati, kwa ajili ya kituo atamizi kilichopo pale Tanga Jiji, kwa ajili ya kuzalisha bidhaa zinazotokana na mkonge kwa kutumia mikono yetu wanawake wa Mkoa wa Tanga. Vijana wa Mkoa wa Tanga na hata watu wenye ulemavu wametengenezewa kituo kile na Serikali imeweka commitment ya shilingi milioni 600, tunawashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunaishukuru Bodi hii ya Mkonge ya Tanga, hakika inafanya kazi nzuri sana kwenye kituo hiki, nimekitembelea, nimeona. Ninaomba sana Serikali ijitahidi kuhakikisha shilingi milioni 600 hizi walizoziweka kwenye kituo atamizi zinafika pale, ili wakufunzi wale waweze kulipwa ipasanyo, ili mashine zile ambazo bado hazipo pale ziweze kuwepo, ili mafunzo yale yaweze kuleta tija kwa haraka. Shilingi milioni 600 zile tunaziomba kwa haraka ipasavyo, ziende kuongeza nguvu katika kituo kile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo atamizi cha Mkoa wa Tanga matamanio yetu siyo tu kuzalisha bidhaa zinazotokana na mikono ziuzwe ndani ya Tanzania, tunatamani kuona zile trade centers zilizopo nchi mbalimbali, kwa ajili ya mazao ya mkonge na products za mkonge zinakwenda kurudi. Mheshimiwa Bashe, historia inaonesha kulikuwa na trade centers katika nchi mbalimbali, ambapo products za mazao ya mkonge zilikuwa zinafika kule na watu wananunua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye balozi zetu mbalimbali tulikuwa tunakuta bidhaa za mkonge kule. Sasa hivi ukienda kwenye balozi zetu zote utakuta kahawa ya Kilimanjaro, lakini bidhaa zile za mkonge za Tanga sasa hivi hazipo, tunaomba warudishe trade centers zile kwa kuanzia na vituo atamizi kama hivi, ili tufanye biashara za Kimataifa zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sitaki kukukwaza, dada yangu. Naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)