Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Selemani Moshi Kakoso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tanganyika

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza nami nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kufanya maboresho makubwa sana kwenye sekta ya kilimo. Pia, nimpongeze Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, na Watendaji wote wa Wizara kwa juhudi kubwa ambazo wamezifanya hasa katika kukuza masoko kwenye maeneo ya mazao ya kibiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona ufanisi mkubwa umefanyika kwenye zao la tumbaku, na saa hizi kuna ongezeko la uzalishaji mkubwa sana kutoka tani 117,000 mpaka kufika 160,000. Ni maendeleo makubwa sana ya zao ukiangalia lilipokuwa huko chini. Ilishuka sana, lakini tunafurahishwa sana na bei ya zao kwa sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, bei ya zao kwa wakulima walio wengi wanafurahia uhalisia wa kile wanachokipata. Vilevile, tunaipongeza Serikali kwenye maeneo ya kuleta pembejeo. Tumepokea pembejeo ambazo zina ruzuku ya Serikali zinazokaribia shilingi bilioni 7.6. Haya ni maendeleo makubwa sana kwa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo ambalo napenda kuishauri Serikali ni kwenye miradi ya umwagiliaji. Kwenye eneo hili bado hatujafaulu, jimboni kwangu mimi nina Mradi wa Skimu ya Karema na Serikali iliahidi kutoa shilingi bilioni 30 ili ule mradi uweze kukamilika. Eneo lile tunaomba Serikali itoe fedha ili skimu ile iweze kukaa vizuri na iwasaidie wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo tunaishauri Serikali ni kwenye suala la mazao ya chakula. Mheshimiwa Bashe kabla hajawa Waziri alikuwa mpambanaji sana wa kuwatetea wakulima ambao walikuwa wanalima mazao yao na wanapangiwa na Serikali, na hili leo hii umepewa dhamana. Tunaomba sana Mheshimiwa Waziri waachieni wakulima wazalishe na wanapozalisha wakipata kuuza sokoni bila kupangiwa, mazao yao yatapanda na tunawapa motisha sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, haya ni mazao ya mahindi na mpunga. Kumekuwa na tabia Serikali inaangalia kwamba kuna uwezekano wa kuwa na njaa, wale wakulima tunawavunja moyo. Tunafunga mipaka, hili halijakaa vizuri. Naishauri Serikali iangalie na iwaachie wakulima wanapopata fursa wazitumie ili ziweze kuwaendeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naendelea kuishauri Serikali kwenye eneo la umwagiliaji. Tuna Ziwa Tanganyika ambalo halijatumika ipasavyo, Ziwa Tanganyika lina maji mengi na lina kina kirefu, ndiyo ziwa linaloongoza kuwa na maji mengi na safi lakini kwa bahati mbaya Serikali haijatumia rasilimali hiyo kwa sababu tunayategemea sana kwa ajili ya kunywa tu yale maji, lakini tungeishauri Serikali tuyatumie kwa ajili ya mfumo wa umwagiliaji, ahsante. (Makofi)