Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Jambo la kwanza niunge mkono hoja iliyoko Mezani ya Mheshimiwa Bashe kaka yangu, lakini jambo la pili nampongeza kwa kazi kubwa ambayo anaifanya katika kuhakikisha kwamba sekta ya kilimo inasonga mbele. 
Mheshimiwa Naibu Spika, nina mambo machache. Jambo la kwanza nichukue nafasi hii kwa niaba ya wananchi wa Makete kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa sababu amekuwa na utaratibu wa takribani miaka mitatu kutupatia mbegu ya ngano, na kwa kweli kwa niaba ya wananchi mimi kama mwakilishi wao nakuja kumshukuru sana lakini nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa sababu mbegu ile inatusaidia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kwenye soko mbegu ya ngano inauzwa zaidi ya shilingi 180,000 mpaka shilingi 200,000 kwa mfuko, lakini sisi mnatupatia bure. Wananchi wa Wilaya ya Makete wanapongeza sana. Pia hapo naomba tu angalizo kwamba ngano tumelima, lakini tumevuna, na kuna malipo baadhi bado hayajalipwa. Kwa hiyo, tunatamani watu wetu wa ASA waweze kutusaidia kutulipa mapema ili wakulima waingie tena kwenye msimu mwingine na iweze kuwasaidia. 
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili; kwanza, tumefanya kitu kikubwa kwenye kilimo kwa maana ya kupandisha bajeti yake kutoka shilingi milioni 200 hadi shilingi trilioni 1.2 sasa ambazo tunakwenda. 
Pili, tu-appreciate jitihada ambazo Serikali inafanya katika suala la ruzuku na maeneo mengine kuhakikisha kwamba kilimo kinakua, hususan Mheshimiwa Waziri amekuwa ni champion kuhamasisha umwagiliaji kwenye nchi yetu, kwamba bila umwagiliaji kilimo hakiwezi kwenda mbele. Tumeona transformation kwenye hilo, kwani mmeweka fedha nyingi kwenye umwagiliaji. Mheshimiwa Waziri I really appreciate kwa niaba ya vijana wa Taifa hili, na kwa niaba ya wakulima wote wa nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mambo machache ninatamani kumshauri Mheshimiwa Bashe. La kwanza, ni kweli mkulima tunampa ruzuku ya mbegu, lakini tumemsaidia mkulima anapima udongo. Ukiangalia kwa sisi Makete udongo tulikuwa tukienda kupima Uyole ni zaidi ya shilingi 140,000 lakini tunapima kwa free kwa sababu Maafisa Ugani wamewezeshwa. 
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, ana ajenda ya BBT, ameimarisha Benki ya Ushirika, sasa tunaiona, na ni kitu kizuri kama Taifa, lakini mkulima ameenda kwenye single digit kwenye suala la mikopo. Mkulima huyu ukisoma kwenye page ya 189 kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri anasema, “Hatuwezi kuondoa umasikini kama hatuwezi kuwaondoa wakulima wadogo kwenye umasikini.” Hoja yake ni kubwa na ni nzito kwa Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kama haya yote tumeyafanya ambayo nimeyataja, yeye kama Waziri anamsaidia vipi mkulima huyu asiibiwe mazao yake? Leo ninapozungumza, mkulima wa Makete analima kiazi na ngano, hadi afike sokoni na hadi apambane na soko, kwa kweli ameumia kwa kiwango kikubwa sana. So, with all the efforts ambazo tumeziweka kwenye mkulima ku-support ruzuku na kufanya nini, Mheshimiwa Waziri lazima aje na jibu la kumsaidia mkulima huyu ili ile nguvu aliyoiwekeza isiwe for nothing, iwe ni yenye tija kwa mkulima. 
Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii tunakuwa na mkulima kutoka Taifa lingine, anakuwa na access ya kwenda kufika Makete nyumbani kwangu kwa mkulima akapata zao, akanunua kitu bila kupitia kwa mfumo halali ambao unatakiwa. Nashauri kama Wizara hilo mtengeneze. Hatutamani tuone wanunuzi wanatoka moja kwa moja nje kuja kum-access mkulima, wakati sisi Tanzania hatuwezi kuingia kwenye hizo nchi kwenda kumkuta mkulima na tukanunua mazao. Sasa Mheshimiwa Waziri madalali hawa wanawaumiza wakulima kwa kiwango kikubwa sana. 
Mheshimiwa Naibu Spika, tunazungumza lumbesa is not a case kwa kiwango kikubwa, lakini tunachotamani kukiona ni Waziri kutengeneza mazingira kwamba, effort zote walizoziweka za mikopo, ruzuku, mbegu ziende kuwa na tija kwa mkulima; akishalima, basi aweze kunufaika na tuone mkulima huyu anatoka kwenye umaskini kama alivyosema na kama ambavyo Serikali imekusudia, naomba sana kwa niaba ya wakulima wa nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, wenzangu wamezungumza kuhusu kitunguu na soko holela. Tunatamani soko holela liondoke kwenye nchi yetu, tutengeneze mfumo ambao unaweza kudhibiti madalali ambao wamekuwa wakiwasumbua wakulima, wameweza kudhibiti kwamba Mataifa mengine yaende kuwa na access na mkulima moja kwa moja kwa kununua mazao na hatimaye kuondokana na soko holela ambalo linawaumiza wakulima. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri, jitihada hizi ziwe ni jitihada zenye tija kwa ajili ya kumwinua mkulima maskini kama ambavyo amesema amenuia, na kweli Serikali imefanya kazi kubwa na hii ndiyo inatufanya sisi pia Wanamakete tukaichagua Serikali mwaka 2020 kwa kazi kubwa ambayo umeifanya, kwa sababu asilimia zaidi ya 90 wananchi wa Makete ni wakulima na we really appreciate kwenye effort ambazo amezifanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo natamani kushauri ni kwenye suala la Bodi za Mazao. Mheshimiwa Waziri unafahamu na ninadhani unafanya study nyingi, unazisoma. Ukisoma study za India kwenye rubber, coffee na tea, ukiangalia Bodi za Mazao zinavyofanya kazi, angalia Ivory Coast, angalia Ghana, wenzetu wameweka u-serious mkubwa sana kwenye hizi Bodi za Mazao ili kuhakikisha kwanza, wana-monitor kwenye bei ili kusiwepo na bei holela. Pili, kuhakikisha kwamba, kunakuwepo na tathmini ya zao lenyewe katika ukuaji wao.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunatamani kama Wizara ya Kilimo, imarisheni angalau hata bodi nne au tano, yaani iwe ndiyo foundation ambayo Waziri ameitengeneza yeye kwenye nchi hii, kwamba bodi hii inatupa matokeo chanya kwa ajili ya mazao fulani, kuliko kipindi hiki unakuta pia kunakuwepo na changamoto ya bodi nyingine ambazo aidha, zimechelewa kuteuliwa au kuna…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Sanga.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kengele ya kwanza.
NAIBU SPIKA: No, ni dakika tano tu.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, sawa nashukuru, naunga mkono hoja. (Makofi)