Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bahi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza nianze kuunga mkono hoja bajeti hii ambayo iko mbele yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sote tunaamini na hata mimi bado ninaamini kwamba nchi yetu ni nchi ya ujamaa, na ujamaa halisi unaweza kuuona katika maisha ya wakulima wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nichukue nafasi hii kwa dhati kabisa nimpongeze Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama ni haki na kama ni kuitendea haki Sekta ya Kilimo, amefanya vya kutosha. Kwa hiyo, kama ukitaka kumwelezea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huyu ni mjamaa katika vitendo katika kuwainua wakulima. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hii vilevile nimpongeze Waziri wa Kilimo, ndugu yangu Bashe. Kwanza, ni mtu mbunifu, lakini ni mtu anayejaribu. Tatizo kubwa la uongozi katika nchi yetu ni kwamba watu hawawezi kujaribu kufanya mambo na kutokuwa na maamuzi, lakini Mheshimiwa Bashe ni mtu anayejua kutumia madaraka katika kuamua. Kwa hiyo, jambo hili mimi nampongeza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona ubunifu mkubwa uliofanyika katika Wizara hii, lakini tumeona namna ambavyo Sekta ya Kilimo imekua kwa kiasi kikubwa. Tangu mwaka 2021 mpaka leo tumekuwa na miradi 780 ya umwagiliaji. Haya ni mapinduzi makubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niende kwenye hoja ya kwanza kwenye suala zima la mbolea na pembejeo. 60% ya wananchi wa Taifa letu ni vijana na kwa maana hiyo vijana wengi inatakiwa waingie kwenye kilimo, lakini hawawezi kuingia kwenye kilimo kwa kutumia jembe la mkono. Jembe la mkono ni corporal punishment. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ipo haja ya kuangalia tutoke kwenye jembe la mkono, tuingie kwenye mechanization, hasa katika jembe la kukokotwa na ng’ombe. Mimi ninamshauri Waziri, jembe la ng’ombe sasa linauzwa shilingi 150,000, Serikali inaweza ikaweka ruzuku kule, ikaondoa kodi, tukaweza kununua hata kwa shilingi 50,000 ili wananchi wengi waweze kulima, waachane na jembe la mkono. 
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine kuhusu uzalishaji, wenzangu wamesema kwenye bustani (horticulture), kilimo ambacho kinavutia vijana wengi, lakini kinatengeneza fedha kwa muda mfupi. Tunazo mashine za pump, zile za man maker, ambazo hutumii umeme, unatumia nguvu zako mkulima katika ku-pump, kwa sasa inauzwa shilingi 500,000; wakulima na wananchi wa vijijini wengi hawawezi kununua.
Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba Mheshimiwa Waziri, zile pump za man maker ziondolewe kwanza kodi na vilevile kutoka shilingi 500,000 walau ziuzwe shilingi 200,000. Tukifanya hivyo, tutaweza kuajiri vijana wengi katika umwagiliaji. Nakupongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa namna ambavyo mmenunua magari kwa ajili ya kuchimba visima. Jambo hili ni kubwa, sisi bado tunaiogopa sana rasilimali ya maji.
Mheshimiwa Waziri mimi ninakushukuru sana, katika Wilaya yangu ya Bahi umeweza kunipa miradi ya umwagiliaji mikubwa. Mradi ule wa Kongogo pale Babayu, Mradi wa Kukarabati Skimu ya Umwagiliaji ya Bahi na mingine, juzi mitano nimeipata katika Bonde la Lukali pale Mtitaa na wanakushukuru sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jana nilikuwa na mkutano pale na pia, pale Mkakatika. Mheshimiwa Waziri kwa kweli, mimi nakushukuru katika suala zima la kutaka kunyanyua kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni suala la mbolea. Mheshimiwa Waziri kwenye mbolea uzalishaji wetu wa viwanda vya ndani ni kama 158,000, lakini mahitaji ni makubwa, kama 1,500,000 sasa bado inatakiwa tuweke umadhubuti katika kuongeza uzalishaji wa mbolea. Bahati mbaya mbolea nyingi tunaitoa nje, lakini Kiwanda kama cha INTRACOM kimeonesha mbolea hii na wakulima wameikubali; kwanza inatumia Samadi, ambayo tunanunua kwa wafugaji, inatumia dolomite na gypsum, ni material ambayo yanapatikana hapa hapa nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)