Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Tunayo mengi sana ya kuzungumza kuhusu kilimo, na hii ni kutokana na jinsi kilimo kilivyopiga hatua. Baada ya ujio wa Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumekuwa na mabadiliko makubwa sana au mapinduzi makubwa sana ya kilimo. Kama ilivyokuwa utaratibu wake, ameamua kupeleka fedha za bure kabisa moja kwa moja kwa wananchi wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona nia hii akiwa anaifanya tangu alipoingia. Kwanza tuliona alivyopeleka fedha za bure kwa wananchi kupitia mafuta. Wakati tulipopata changamoto ya mafuta, alitoa fedha za bure kabisa ambazo tulikuwa tukizitumia. Kwenye eneo la kilimo pia ametoa fedha za bure na bado anaendelea kutoa fedha za bure. Hapa ninawashauri wananchi wote, hususan wananchi wangu wa Jimbo la Lulindi, kutumia fedha hizi za bure. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais ametoa fedha za bure kwenye pembejeo za kilimo. Pembejeo zote, kwa mfano, kwenye upande wa korosho tunapewa bure kabisa, hatulipii hata senti moja. Ni fedha za bure kabisa. Mheshimiwa Rais ametoa fedha za bure kwenye mbolea. Hapa ametoa takribani fedha nyingi sana zinazowezesha wananchi kupata fedha za bure. Kama wataamua kulima takribani nusu ya mapato yao inatokana na fedha za bure walizopewa na Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais pia ameendelea kutoa fedha za bure kwenye mradi wa BBT. Huu ni mradi ambao unalenga katika kumwezesha kijana popote alipo ili apate fedha za bure kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, halikadhalika Mheshimiwa Rais amewezesha pia upatikanaji wa fedha za bure kwenye miundombinu ya umwagiliajia kwenye mabwawa. Kwa mfano, mabwawa yote yanayojengwa, yanajengwa na fedha za bure kabisa, ambapo kama wananchi wataamua kwenda kwenye kilimo na kufanya kazi hii ya kutafuta fedha za bure watazipata, ni za bure kabisa, ziko pale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nawashauri, kama nilivyosema tangu huko mwanzo, wananchi kwa nguvu kabisa tuzichukue fedha hizi, ziko wazi kabisa, wala hazihitaji shida yoyote, wala hazihitaji msukumo wowote. Ni kuamua tu kwenda na kuzipata pale. Ziko bure kabisa, twende tukazichukue. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi kwa upande wangu natamani pia fedha hizi za bure nizipate katika jimbo langu. Katika kata takribani kama sita saba hivi; Kata ya Mpindimbi, Kata ya Mbuyuni, Kata ya Lupaso, Kata ya Sindano, Kata ya Lulindi, Kata ya Lipumburu, Kata ya Mnavira, na Kata ya Mchauru. Kata hizi zote pamoja na Kata ya Lulindi, ni kata ambazo zinawezesha kilimo cha umwagiiaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maana hiyo, kama miundombinu ya umwagiliajia itajengwa pale ambayo itawawezesha wananchi wangu wa kata zile kupata fedha za bure, hakika jimbo langu litastawi kweli kwa sababu ni ustawi ulio wazi ambao umepewa nyenzo za kukua kwa haraka kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namwomba sana Mheshimiwa Waziri, atakapokuja ku-windup hapa, anihakikishie na mimi katika jimbo langu fedha hizi za bure naweza kuzipata vipi, hususan katika maeneo haya niliyomwambia? Mimi na yeye tulikaa huko nyuma tukaanza kuzungumzia suala la kuweza kutoa pia ruzuku mbalimbali kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine, kuna jambo ambalo tumeona halifanyiwi kazi. Kwa mfano, benki. Kama benki imekuwa ikipitia fedha nyingi sana za wakulima. Kwa mfano, Pato letu la Taifa katika nchi hii ni takribani kiasi cha bilioni 80 fedha za kigeni. Bilioni 80 dola, hayo ni mapato ya nchi hii. Sasa, katika pato hili kilimo kinaingiza takribani 26%. Ukifanya mahesabu yako, 26% ya pato hili ni takribani shilingi trilioni 54 za Kitanzania. Fedha hii yote imekwenda benki, imepitia benki.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, fedha hizi benki wamekuwa wagumu sana kuwasaidia wananchi, kwa sababu chanzo cha mapato yao makubwa, hiyo shilingi trilioni 54 inatokana na wakulima, lakini wao hawatoi mkopo kwa wakulima ambapo ndiyo chanzo chao kikubwa cha mapato hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba Mheshimiwa...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Mchungahela.

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)