Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Musoma Mjini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangia katika hii Wizara ya Kilimo. Mimi pia naungana na wenzangu kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Kilimo pamoja na Naibu wake kwa kazi nzuri na kubwa ambayo wameendelea kuifanya katika hii sekta ya kilimo. 
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu ya muda, mimi nichangie tu kwenye maeneo mawili, hasa yale ya BBT kwa ajili ya wale ma-giant wakubwa lakini pamoja na hawa wadogo wadogo. Nianze na lile la wakubwa. 
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wale wakulima wakubwa, nimshauri Mheshimiwa Waziri atengeneze tu ile data bank ya wakulima wakubwa, wafahamike. Wakishafahamika, yaani hao wala hahitaji hata kuchukua fedha ya Serikali katika kuwasaidia. Anachohitaji kufanya hapo ni kazi ndogo tu. Aangalie tu hata yale mashamba ya Wizara yote ambayo yako tupu na ambayo najua yako mengi. Hayo mashamba ukiangalia leo, yako mazao ya muda mfupi, lakini bado yanafanya vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, nilikuwa najaribu kuangalia hapa kwa mwaka 2023/2024 kuna zao kama la ufuta ambalo limeingizia Serikali, siyo chini ya shilingi trilioni mbili, zimeingiza fedha za kigeni. Sasa, ufuta ni zao ambalo unalima tu katika kipindi kifupi, tayari unaweza kuvuna. Yako pia mazao mengine kama hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nini kifanyike? Kumbe cha kufanya ni kwamba, akiwashirikisha hao wakulima wakubwa ni rahisi sana wakafanya kazi hiyo. Tena wakati mwingine anaweza katika lile soko akafunga ile forward contract, ukajua kabisa kwamba tani kiasi kadhaa zinatakiwa kwenye nchi fulani, akawahamasisha wakalima. Kwa hiyo, ndani ya muda mfupi tayari yale matokeo yakaweza kuonekana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, katika yale maeneo yote ambayo tuna mashamba makubwa, hao wafanyabiashara wakubwa wengi wanahitaji tu elimu na waelekezwe kwamba hapa kuna fursa, atatumia fursa zake. Hata pale ambapo hana uwezo; leo nimemwona Mkurugenzi wa CRDB, ninadhani amekuja hapa na amekaa kwa muda mrefu. Ni kwa sababu naye nadhani ameanza kuwa na interest katika kilimo. Kwa hiyo, anaweza naye akatusaida, pamoja na benki nyingine kwenye upande huo.
Mheshimiwa Naibu Spika, unapokuja kwenye lile suala la wale wakulima wadogo, ushauri wangu kwa Mheshimiwa Waziri, asichukue ile mikoa 21 tu. Hebu BBT hii ya wakulima wadogo iende kila mkoa. Nitoe tu mfano, na nimwombe siku moja apate nafasi aje pale kwangu, nami ni mkulima, ninalima pale Bunda. Yaani pale pembeni yangu ziko eka zaidi ya 500 lakini unakuta kila mkulima anaweka ka-pipe ka inchi moja na nusu, anatumia hivi vi-honda, kwa hiyo anahangaika, yaani usiku mzima wanahangaika. Yaani unaangalia hawa watu, kumbe wanachohitaji hapa ni vifaa tu, na wala siyo vifaa vingi. 
Mheshimiwa Naibu Spika, wanahitaji tu bomba la inchi sita, wanahitaji ile pump ya shilingi milioni mbili pamoja na ile motor ya milioni tatu horsepower 50. Wale watu Mheshimiwa Waziri akiwavutia kwa kuwawekea hivyo vifaa vyote, akivi-consolidate havivuki shilingi milioni 50 mpaka 100. Kwa hiyo, akiwawekea pale wanaweza kumwagilia eka 500. Sasa, leo tujiulize, kwenye nchi hii hao wakulima, yaani hayo maeneo ya eka 200, eka 500 yako mengi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kumbe leo akiamua ndani ya mwaka mmoja wakulima wengi kabisa wa nchi hii, hao wadogo wadogo wanaweza wakafanya kazi. Watu wa kusaidia kusimamia, yaani badala ya yeye sasa kwa level yake, anahitaji aanze kufikiria mambo makubwa. Badala ya kufikiria habari ya kwenda kuangalia vijana wa Chinangali, sijui vijana 200, vijana 100... (Makofi)
(Hapa, kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Manyinyi.
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)