Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nikuchukue nafasi hii kukushukuru kwa kunipa hii nafasi ya kuchangia leo kwenye Wizara ya Kilimo. Kipekee, nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ambayo ameifanya kule Manyoni upande wa kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru ndugu yangu Mheshimiwa Waziri Bashe, Naibu Waziri na Katibu Mkuu Mweli kwa kazi kubwa ambayo wameifanya katika ku-transform Wizara ya Kilimo. 
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi niseme kwamba Mheshimiwa Bashe naye akiwa na Mheshimiwa Rais wameitendea haki sana Manyoni. Upande wa umwagiliaji, kuna miradi ilikuwa imeongelewa zaidi ya miaka 15. Kila ilani ilikuwa inataja Bwawa la Mbwasa na Scheme ya Umwagiliaji ya Udimaa, lakini ndani ya hii miaka minne ya Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Bashe akiwa Waziri wa Kilimo, ameweza kuweka historia ya kutangaza tenda ya ujenzi wa Bwawa la Mbwasa la Umwagiliaji, na tayari mkandarasi ameshapatikana na tayari ameshakabidhiwa site. 
Mheshimiwa Naibu Spika, huyu mkandarasi amekabidhiwa site, lakini hayupo site. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri, huyu mkandarasi afike sasa site aanze kazi, na wananchi wananiulizia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na Bwawa la Udimaa la Umwagiliaji, vilevile nimshukuru Mheshimiwa Waziri, alitangaza tenda Udimaa ya ujenzi wa bwawa. Tayari mkandarasi ameshapatikana. Naomba vilevile huyu mkandarasi aweze kwenda na kuanza kazi. 
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ningeshauri, tukiacha hii miradi mikubwa ya umwagiliaji, kuna hawa wakulima wadogo wadogo wa mboga za majani ambao kimsingi wangeweza kuhitaji umwagiliwaji katika small scale. Ningeshauri, Mheshimiwa Bashe aangalie, tunawezaje kuja na mfumo wa pump kwa ajili ya kusawaidia hawa wakulima wadogo wadogo wa umwagiliaji?
Mheshimiwa Naibu Spika, najua hii miradi mikubwa ni kwa ajili ya Large Scale Irrigation System, lakini anaweza akaja na mfumo mzuri kwa ajili ya hii miradi midogo ya umwagiliaji. Nakumbuka niliwahi kufanya kazi Word Vision, tulikuwa tunatumia pump fulani zinaitwa Money Maker Pump, ambazo kimsingi zilikuwa zinasaidia sana wakulima wale wadogo wadogo. Tuangalie ni jinsi gani Serikali inaweza ikasaidia hata kwa kuweka ruzuku, ili nayo tuwasaidie wakulima wengi. 
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la pili ni korosho. Kwa kweli Manyoni tunalima sasa korosho. Watu wa Mtwara walikuwa wanatucheka Manyoni hatulimi korosho, lakini Mheshimiwa Bashe pamoja na Mheshimiwa Rais wameleta mapinduzi makubwa kwenye kilimo cha korosho. Mwaka huu tumeweza kuuza zaidi ya tani 100,000 za korosho, lakini vile vile hata bei ya korosho tumeuza katika daraja la kwanza 3,167. Haya ni mafanikio makubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mbali ya hiyo, Mheshimiwa Bashe ameweza kujenga ghala Manyoni, ameweza kujenga Kituo cha TARI Manyoni, ameweza kupeleka pikipiki nyingi pale Manyoni, na ameweza kupeleka wataalamu pale Manyoni. Kwa hiyo, mimi namshukuru sana Mheshimiwa Bashe. 
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, korosho ya Manyoni bado ina changamoto. Moja, ni tembo. Hili Mheshimiwa Waziri analifahamu, yeye na Waziri wa Maliasili. Naomba tukatatue changamoto ya tembo wale wa Manyoni kwa sababu wanamharibia korosho. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine namshukuru ametoa ruzuku ya dawa kwa wakulima wa korosho wa Manyoni, wanashukuru, lakini wanaomba vile vile ifike kwa wakati. 
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho ni kuhusu tumbaku. Manyoni tunalima tumbaku. Namshukuru sana Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku, alifika Manyoni na wataalamu wake wamehamasisha watu kulima tumbaku. Tunaomba sasa Mheshimiwa Bashe aje Manyoni. Mbali na korosho, sisi tuna maeneo mengi ya kulima tumbaku na wananchi wamehamasishwa kulima tumbaku. Tunataka vilevile kuwekeza kwenye tumbaku.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuyasema haya, mimi nakushukuru tena. Pia namshukuru sana Mheshimiwa Rais, nimshukuru na Mheshimiwa Bashe na ninamwombea. Najua atarudi kuwa Mbunge na atarudi kuwa Waziri wa Kilimo. Akirudi aendeleze kilimo cha umwagiliaji Manyoni, hasa Tarafa ya Kintinku. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, na ninaunga mkono hoja. (Makofi)