Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Rais kwa moyo wa dhati wa kuwekeza kwenye kilimo kwa rasilimali fedha na watu katika kilimo. Uwekezaji kwenye fedha kupitia Serikali yake, ameongeza bajeti ya kilimo, hivyo kuboresha mipango ya kuendeleza kilimo nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, uwekezaji kwa rasrimali watu, amewekeza kwa kumteua Waziri wa Kilimo bora na Katibu Mkuu wake wenye passion na kilimo na kwa kweli kumwacha Waziri muda mrefu katika Wizara hiyo ili aendelee kutimiza maono yake ya muda mfupi, wa kati na mrefu juu ya maendeleo ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba maombi yafuatayo kwa mijini ikiwemo Mji wa Iringa. Mji wa Iringa ni mji wa kitalii, na kwetu sisi mazao ya mbogamboga ni muhimu sana. Sasa naomba ufanyike ukarabati mkubwa wa scheme ya umwagiliaji Mkoga iliyopo Kata ya Isakalilo ambako inazalisha mbogamboga kwa ajili ya kulisha mji wetu. Pia, tunaomba kuchimbiwa bwawa kwa ajili ya umwagiliaji katika eneo la Kata ya Kiwele, Kitongoji cha Mapinduzi ili tuweze kulima mazao ya mbogamboga.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa kweli kuwapongeza sana viongozi wa Wizara hii, kwani wapo tayari kufanya kazi kwa ushirikiano bila urasimu usiokuwa wa lazima. Mheshimiwa Waziri na Katibu Mkuu, kwa kweli na wataalamu wao wanafanya vizuri. Utendaji kazi wa Wizara hii unapaswa kuigwa na Wizara nyingine. Ushauri wangu BBT isiachwe, bali iboreshwe zaidi kwa kushughulikia changamoto zilizojitokeza kwenye utekelezaji wa mradi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, tuendelee kutoa mafunzo kwa kushirikiana na sekta binafsi na JKT. Halafu tuwawezeshe wale waliofanya vizuri na kuwasimamia warudi na kuendeleza ujuzi huo kule walikotoka na siyo kuwapa maeneo sehemu nyingine ili kusambaza ujuzi huo sehemu nyingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mbegu za kienyeji litiliwe mkazo na zihifadhiwe zikiwepo na za mifugo, mwashauri pia. Tunaomba sasa mikoa ile yenye kilimo ufanyike utaratibu wa kuzitafuta mbegu hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.