Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo, nampongeza Waziri wa Kilimo, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na wataalamu wote kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwa bajeti hii miradi jimboni Busanda, Mradi wa Umwagiliaji wa Nyamalulu Kata ya Magenge, na ombi la mradi wa umwagiliaji Kayenze (Saragulwa) Kata ya Nyamwilolelwa vifanyiwe kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile mpango wa ruzuku kwenye pembejeo za kilimo uendelezwe na kuimarishwa na kupelekwa kwa wakati ili shughuli za kilimo maeneo yetu hususan Jimboni Busanda ziimarike. Usimamizi wa shughuli za kilimo uangallwe upya, Maafisa Ugani na shughuli za ugani hazikidhi maono makubwa yaliyopo sasa na baadaye.