Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nachukua fursa hii kumshukuru Mungu kwa kunijalia afya njema. Pia, naomba nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uchapakazi wake na kuongeza bajeti kwenye sekta hii ya kilimo na jitihada zake za kuhakikisha anawanyanyua wanyonge. Naomba pia nimpongeze Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara kwa uchapakazi wao.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuishauri Wizara mambo maiwili. Moja, mazao yote yanayouzwa kwa kilo sokoni, basi yanunuliwe kwa kilo hata shambani. Mfano, vitunguu na nyanya, sokoni vinauzwa kwa kilo, ila kutoka kwa mkulima vinauzwa kwa tenga na lumbesa.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kwenye kila ukanda lazima tuweke mkazo na kufufua mazao yetu ya kimkakati na ya kibiashara. Kwa mfano Kusini wameshajipambanua kwa korosho, parachichi na kahawa. Sisi Tanga tunalo zao la minazi, korosho na chungwa. Mazao haya yanafanya vizuri ukanda huo, lakini ni kama kwa sasa yanakufa. Tunaomba Wizara iweke jitihada kama ilivyoweka kwenye mkonge.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, naomba kuunga mkono hoja ya Wizara.