Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

Hon. Oran Manase Njeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbeya Vijijini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026

MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee ninaomba kuungana na Watanzania wenzangu kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza vyema miaka minne kwa kuongoza nchi yetu akiwa Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tumeshuhudia mafanikio makubwa katika kuimarisha miundombinu hususan barabara, reli, viwanja vya ndege na bandari. Vilevile huduma za kiuchumi na kijamii kama vile ujenzi wa madarasa, hospitali, zahanati na vituo vya afya. Pia huduma za maji, utawala bora, pamoja na kuhamasisha uwekezaji na utalii.

Mheshimiwa Spika, pia ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri iliyotukuka ya kumsaidia Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, kwa kuteuliwa kuwa Mgombea Mwenza wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa uzoefu na weledi wake, kama ilivyo kwa Watanzania walio wengi nina imani kubwa kwa Mheshimiwa Nchimbi na kumtakia afya njema na kila la heri kwenye mchakato ujao.

Mheshimiwa Spika, ninampongeza Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kwa kutekeleza majukumu ya kumsaidia Waziri Mkuu ikiwa na pamoja na jukumu la kuendelea kuisimamia ipasavyo sekta ya nishati.

Mheshimiwa Spika, ninapenda pia kutumia fursa hii kukupongeza wewe binafsi, Naibu Spika na pia uongozi wote wa Bunge kwa uongozi mahiri na wenye ubunifu wa hali ya juu katika kuongoza Mhimili wa Bunge.

Mheshimiwa Spika, ninapenda kumpongeza Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa hotuba nzuri iliyojaa ubunifu mkubwa na imedhihirisha utayari wa Taifa letu katika ushindani wa kimataifa (national competitiveness). Bajeti hii ambayo ni ya mwisho inaenda sambamba na Dhima ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/2022 – 2025/2026 ambayo ni Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu.”

Mheshimiwa Spika, katika kipindi chake akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki tathmini zinathibitisha mafanikio makubwa ya utekelezaji na usimamizi wa mpango wa kwanza na wa pili na kupelekea Taifa letu la Tanzania kufanya vizuri mno kuinua uchumi katika kipindi hiki kigumu.
Mheshimiwa Spika, ninapenda kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ya kuimarisha mahusiano ya kimataifa na pia kwa mafanikio makubwa ya Royal Tour ambayo imeanza kuleta matunda makubwa ya kiuchumi kwa nchi yetu, hususani sekta ya kitalii na uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, ninapendekeza Serikali kuimarisha diplomasia ya uchumi kwa lengo la kuongeza uwekezaji kutoka nje (FDIs), masoko ya uhakika kwa mazo ya kilimo, madini na utalii pamoja na kuongeza mapato kwa Taifa letu. Hii itaisaidia kuongeza fedha za kigeni na kuimarisha uchumi wa Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja.