Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Spika, ninamshukuru Mungu kwa uzima na afya kuimarika na kuendelea kutimiza wajibu wa kazi ya Kibunge.
Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Spika na wasaidizi wake wote kwa kuendesha Bunge kwa ukamilifu na ushirikiano. Pia nimpongeze Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri kwa kuendelea kuijenga na kuilinda Jumuiya yetu kwa amani na upendo hali ambayo inatufanya Watanzania kujidai kwani amekuwa mama mnyenyekevu na msikivu.
Mheshimiwa Spika, niwapongeze Wizara hii ya Mambo ya Nje kuendeleza sera ya kujenga nchi yetu kwa kuendeleza mahusiano yetu na nchi za umoja huu. Niwapongeze mabalozi wetu kwa kufanya kazi zao za kibalozi kwa uaminifu na wamejitahidi kuchangamkia fursa hasa za kiuchumi, lakini niombe elimu itolewe kwa Watanzania ili fursa hizi ziweze kuchangamkiwa na wananchi kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, niendelee kumpongeza Rais wetu kwa kuendelea kukamilisha bajeti inayoombwa na Wizara hii kwani tumekuwa mfano bora kwa kulipa michango yetu katika Bunge la Umoja wa Afrika Mashariki
Mheshimiwa Spika, ninaomba kuunga mkono hoja.