Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu. Pili, ninaomba nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kampeni nzito sana aliyoifanya akituongoza na sisi wengine. Ninampongeza na Makamu wa Rais. Ninakupongeza na wewe umetupatia dakika tatu, sitazungumza mengi zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kutuletea Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu. Pia ninampongeza kwamba tangu alipochaguliwa mara ya kwanza kuwa Rais huwa anawaona sana Mawaziri wa Fedha. Kipindi cha kwanza alipoteua Makamu wake wa Rais, alimwona Waziri wa Fedha ambaye alikuwa ni Makamu wa Rais aliyestaafu kama sikosei Mheshimiwa Dkt. Mpango, alimtoa akiwa Waziri wa Fedha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, leo amemwona Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba aliyekuwa aliyekuwa Waziri wa Fedha wetu, aliyekuwa mwenzetu tuliyekaa naye hapa kwa muda. Ninamkumbuka akiwa Mbunge nikiwa nina maana backbencher, akiwa Naibu Waziri, akiwa Waziri katika Wizara mbalimbali. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niwaambie Waheshimiwa Wabunge wenzangu wote, sifa hii hakuna mtu alizungumza. Sifa kubwa ya Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye sasa anaenda kuwa Waziri Mkuu wetu, anafikika. Waheshimiwa Wabunge mlioko humu ndani lazima niseme ukweli, kuna watu wakiwa Mawaziri wanakuwa wagumu kufikika. Waziri Dkt. Mwigulu Nchemba amekuwa Naibu waziri, Waziri, Waziri wa Fedha mtu yeyote anamfikia wakati wowote pale alipoketi. Waziri Mkuu ajaye, huyu hapa, nyumbani kwake ni nyumbani kwa kila mtu. Hongera sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu hajui, lakini ameigusa mioyo yetu sana. Mimi nina uhakika wale tuliokaa na Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba tunamfahamu, nyie mliokuwa nje ambao mmeingia sasa mlikuwa mnamsikia ni kijana mzuri sana, ana upendo kwa wenzie, anakukaribisha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nisingependa kuongea kwa muda mrefu, lakini ninaomba niwashawishi Wabunge wenzangu tumepata Waziri Mkuu mzuri. Sisi tunamtaka Waziri Mkuu atakayetupokea pale mbele, ukienda akupatie nafasi. Wote mtakuwa mnataka hivyo. Yule pale ndiye mwenzetu atakayetupokea wakati wowote. Ninamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa unyenyekevu mkubwa, ametuletea Waziri Mkuu ambaye Wabunge wote tunamhitaji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)