Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nichukue fursa hii kuunga mkono pendekezo la Mheshimiwa Rais kutuletea Waziri Mkuu mahali hapa. Nishukuru kwa maono yanayoendelea kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mwenyezi Mungu anaendelea kuweka nguvu na maono makubwa ndani yake ya kuweza kuliendesha Taifa hili, ili liweze kusonga mbele. Maono yake juu ya kiongozi mwenzetu ambaye kaenda kupata nafasi ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, tunashukuru sisi kama Wabunge, amekuwa kwetu sio Waziri tu, bali amekuwa kaka pia.
Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge waliotangulia kusimama waliweza kusema mengi juu yake. Wamesema ni mtu ambaye anafikika, lakini kwa wale Wabunge wenzetu ambao mmeingia, siyo kufikikia tu, yeye amekuwa kaka, na mwepesi kwa kila Mbunge aliyekuwemo humu ndani. Ana sifa nyingi ambazo zimeweza kuelezewa, lakini kwetu sisi kwa umri wetu, lile la kuona tunapata heshima ya kipekee ni pale tunapomfikia kuweza kutatua matatizo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tumpongeze Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba kwa mambo makubwa aliyoyafanya ya Kitaifa lakini tumeona namna mfumo wa bajeti ulivyokuwa ukienda ndani ya Taifa letu, pale tunapompatia mawazo yetu kuangalia wanyonge kwenda kugusa matatizo ya watu wanyonge, alikuwa mwepesi kuweza kuyatatua. Imani yetu kwake bado ni kubwa, tunaamini kwamba bado tupo na yeye na bado mwelekeo wake utaendelea kuwa kama alivyo na hataweza kubadilika. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tumeambiwa tuseme, na wengi tumeshasema maneno mengi, tunampongeza, lakini pia tunaunga mkono kwa mambo ambayo ameweza kuyafanya ndani ya Taifa hili. Waliopata nafasi, wameweza kuelezea tangu ndani ya chama chetu, Chama cha Mapinduzi ameweza kufanya mambo makubwa, lakini ndani ya Wizara kwa muda wa vipindi vinne nilivyoweza kukaa ndani ya Bunge, ameweza kutumika, kufanya kazi vizuri kwa unyenyekevu, kwa kujishusha, lakini isitoshe ameweza kufanya kazi hata kwa Mbunge mmoja mmoja pale tunapokuwa na shida ndani ya majimbo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa nafasi hii ambayo nimeipata, kwa niaba ya wenzangu, tuendelee kumpongeza hususan Rais wetu kwa maono ambayo Mwenyezi Mungu ameweka ndani yake. Pia, tumpongeze na kumtakia kila la heri katika safari yake hii ambayo anaendelea nayo.
Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa hayo machache. (Makofi)