Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Magharibi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, kwa unyenyekevu mkubwa wa moyo wangu, ninaomba nitumie nafasi hii, kwanza kabisa kukushukuru wewe kwa kunipa heshima ya kutoa neno la shukrani kwa kaka yetu kipenzi, Mheshimiwa Rais Dkt. William Ruto kutoka Kenya, kipenzi cha Wabunge wengi wa Tanzania na kipenzi cha Watanzania wengi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, maneno aliyoyatoa Mheshimiwa Rais Dkt. William Ruto katika Bunge hili leo, nafsi yangu imenikumbusha niamini ya kwamba ndoto za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ndoto za Jomo Kenyatta, zingali zinaishi katika mioyo ya Marais hawa wawili, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Dkt. William Samoei Ruto, kipenzi cha Watanzania, kaka yetu kutoka Kenya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hotuba aliyoitoa Mheshimiwa Rais Dkt. William Ruto, ninashawishika kabisa kuamini, mapenzi aliyonayo Mheshimiwa Rais wetu kwa Wakenya, mapenzi aliyonayo Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kaka yake Mheshimiwa Rais Dkt. William Ruto, yamenithibitishia beyond reasonable doubt kwamba Wananchi wa Kenya hawakufanya makosa kumchagua Mheshimiwa Rais Dkt. William Ruto kuwa kiongozi wao. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Wananchi wa Kenya hawakufanya makosa kumwamini Mheshimiwa Rais Dkt. Samoei Ruto kuwa kiongozi wa nchi yetu jirani, watu ambao tunawapenda. Ninataka nikuhakikishie Mheshimiwa Rais Dkt. William Ruto, utakaporudi Kenya, fikisha salamu za Wabunge wa Tanzania, waambie Bunge la Tanzania linawachukulia Wakenya kama kaka na dada zao. Fikisha salamu kwa Wakenya, waambie Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Spika wa Bunge la Tanzania anawachukulia Wakenya kama ndugu zao wa damu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, borders haziwezi kutukutenganisha na ninataka nikuhakikishie sisi tutaendelea kukuombea na ninataka nikuachie neno la bwana kwa sababu ninajua nawe ni mpakwa wa mafuta wa bwana, ninajua huduma zako katika kazi ya bwana ninataka nikuachie neno la Bwana Mheshimiwa Rais Dkt. Ruto. Neno la Mungu linasema katika Zaburi ya 121: 7-8 na mimi kwa sababu pia ni mpakwa mafuta ninakuachia upako Mheshimiwa Rais Dkt. Ruto utakaporudi Kenya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, neno la Mungu linasema; “Bwana atakulinda na mabaya yote, Bwana atakulinda nafsi yako, Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, tangu sasa na hata milele.” Mheshimiwa Rais Dkt. Ruto bwana amekupa kibali usiyogope sisi Watanzania tunajivunia kazi za Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sisi Watanzania tunathamini kazi na mageuzi makubwa ambayo Mheshimiwa Rais wetu aliyafanya katika nchi hii na kwa sababu wewe umechagua kumwamini Mheshimiwa Rais wetu kama dada yako, sisi Waheshimiwa Wabunge wa Tanzania ni nani tusikuombee wewe ushinde uchaguzi wako mwakani bwana akubariki, neema ya Mungu ikufunike, malaika wa bwana wakuatamie. Nenda shujaa Mheshimiwa Dkt. Ruto tutakukumbuka Watanzania, sisi ni damu yako, sisi ni mifupa yako, bwana akubariki na kukutengemaza, katika jina la bwana ahsante Mheshimiwa Dkt. Rais Ruto. (Makofi/Kicheko)