Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais Dkt. William Ruto Rais wa Kenya Mimi ni dadako mkubwa niruhusu niite jina lako kidogo Mheshimiwa William. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ukimwangalia Mheshimiwa Dkt. Rais Ruto moja kwa moja ana roho nzuri na ana upendo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mimi nimesikiliza hotuba yake vizuri tangu mwanzo, Waheshimiwa Wabunge alichotaka kutuambia Mheshimiwa Rais Dkt. Ruto amekuja kwa upendo kwetu. Anachotaka Mheshimiwa Rais Dkt. Ruto Wabunge wa Tanzania maana yake ukishazungumza Wabunge wa Tanzania ukizungumza nao umezungumza na Watanzania wote, message kubwa aliyoileta kwetu Mheshimiwa Rais Dkt. Ruto tuendelee kushirikiana sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais Dkt. Ruto, sisi Watanzania tunawapenda sana Wakenya na nikwambie ukweli mimi ninasafiri kupitia kupitia Kenya mara kwa mara, tunapata mahusiano mazuri sana na Wakenya wenzetu, hatuna malalamiko na Wakenya wenzetu. Iwapo Kenya na Tanzania tunataka kweli tupate maendeleo ni lazima tushirikiane kama nyie mnavyoshirikiana, Mheshimiwa Rais Dkt. Ruto na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ninyi wawili mnavyopendana na sisi na Wakenya tutaendelea kupendana hivyo hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa sababu nimepata nafasi hii kidogo ya kuzungumza na wewe nikuletee salamu kutoka kwa Baba yako anaitwa John Samuel Malecela, ndiye mume wangu. (Makofi)
Ameniambia nikusalimie sana, lakini na sisi wanawake wa Tanzania tunaomba ukamsalimie sana Mama Rahel Ruto, tunampenda sana, tunamtamani sana na tumesikitika leo hukuja naye lakini mpelekee salamu zetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)