Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi nichangie hoja iliyoko mezani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai, lakini ninaendelea kuwashukuru Wanaurambo kwa ushirikiano wanaonipa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachukua nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia na Serikali anayoiongoza kwa jinsi ambavyo ametufikiria sisi Wana-Urambo, shida ya maji tuliyonayo. Tunashukuru sana Serikali hii kwa kutuletea mradi ambao ninaamini kabisa utatusaidia. Mheshimiwa Waziri Aweso, Naibu wako, Katibu Mkuu, wote ni watendaji wazuri sana na wakuu wa idara wengine. Kwa kweli kazi mnaifanya, hongereni sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo ninawashukuru pia mainjinia wa RUWASA, TUWASA, ngazi zote kwa kushirikiana na sisi Wanaurambo katika kushughulikia hili suala la maji. Ahsante sana kwa kazi kubwa mnayoifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Aweso na Naibu wake na watendaji wake kwa kweli wanakuja Urambo, ahsante sana Mheshimiwa. Mheshimiwa Aweso time uliyokuja Urambo nilishangaa, ulikuja jioni bila kujali umbali. Ukatembelea Mradi wa Miji 28 ambao ninaishukuru sana Serikali kwa kutuweka sisi Urambo ndani ya Mradi wa Miji 28. Ulikuja ukaona maji yamefika, ukatoa maagizo tenki lile lianze kujazwa na mara moja ukawaambia watendaji wote waanze kuangalia usambazaji wa maji na wafanye majaribio ili wananchi wa Urambo katika vijiji vile vya kwanza 20 waanze kutumia maji. Tunakushukuru sana wewe na Naibu na wote kutoka Wizara yako. Kazi mnaitendea haki ya kutafuta maji kwa ajili ya Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakushukuru sana, wewe na Naibu na wote kutoka Wizara yako, kazi mnaitendea haki ya kutafuta maji kwa ajili ya watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Aweso, ulipofika Urambo uliwaagiza ma-engineer ngazi zote ambao wanafanya ushirikiano mkubwa sana wa upande kama nilivyokwambia, ngazi zote za TUWASA na RUWASA, uliwaambia waanze kufanya majaribio ya kusambaza maji. Ninachokuomba leo pamoja na kukushukuru ni kwamba tuongeze nguvu katika kusambaza. Nikutolee mfano, ulipokuja mradi Urambo wa visima 900 sisi tukapewa visima vitano na kutokana na shida ya maji, kisima kimoja tu ndio kilipata maji. Maana yake ni nini, mradi tunaotegemea ni huo wa Lake Victoria kutuletea maji. Kwa niaba ya wananchi wa Urambo ninakuomba, ulivyochapa kazi wewe na Wizara nzima, fedha ziletwe zaidi ili usambazaji wa maji uongezeke, tuanze kuyatumia maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi wala sina wasiwasi na wewe, wewe ni mchapakazi naamini kabisa maji yatafika mara moja utakapoamua kuongeza fedha. Umetusaidia, umeleta mabomba ya majaribio, kwa hiyo naamini kabisa nguvu itaongezwa ili maji yaanze kusambazwa tupate maji Wana-Urambo, kwa sababu hakuna mbadala wa maji, ahsante sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwa kututhamini, uhitaji wetu wa maji ulikubali bwawa likaanza kujengwa la pale Muungano na limeshafikia 88%. Tunakushukuru sana, ombi letu sisi yule mkandarasi anaomba tu mumpe shilingi bilioni 1.2 akamilishe lile bwawa. Tunaamini kabisa likishirikiana na yale maji ya kutoka bwawa lile na maji ya kutoka Lake Victoria, Urambo tutakuwa tumepata nafuu sana ya kupata maji, tunakushukuru sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo huo tulipopewa Bwawa la Muungano, mlitupa pia matumaini. Walikuja ma-engineer wakaona pia kuna uwezekano wa kupata maji katika Kata ya Uyumbu, kwa hiyo tunachoomba sisi sasa, bwawa lile la Uyumbu nalo lianze kufanyiwa utafiti ili lijengwe, kwa sababu ninaamini hilo la Uyumbu litasidia pia umwagiliaji.
Kwa hiyo, kwa heshima na taadhima tunaomba Bwawa la Uyumbu liweze na lenyewe kuchimbwa, lipate maji lisaidiane na lile Bwawa la Kalemela ili tuweze kupata maji pamoja na yale yanayotoka Lake Victoria. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ningeweza kuongea maneno mengi, lakini sina haja ya kuongea maneno mengi, Mheshimiwa Aweso wewe unakuja, umekuja, umeona na umetilia mkazo, ninachoomba tu ni kwamba chonde chonde fedha zipelekwe ili maji yasambazwe katika vijiji vya kwanza 20, bwawa lile ukilipiga wewe, bwawa lile ni la shilingi bilioni tano, ukiliongezea tu shilingi bilioni 1.2 linakamilika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii, ninaunga hoja mkono na ninawatakia Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara ya Maji, kazi njema, ahsante sana. (Makofi)