Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Masanja Kungu Kadogosa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Vijijini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

2

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. MASANJA K. KADOGOSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa hii fursa, lakini vilevile nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri kwa hotuba nzuri sana na yenye mwelekeo mzuri sana kwa Taifa letu kwa maana ya Muungano wetu. Vilevile, nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuhakikisha kwamba muungano wetu unakuwa imara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu ninataka nianze kwanza na muungano. Muungano wetu una miaka 62 sasa kwa siku tano zinizokuja, sasa ina maana gani? Ukiangalia Bunge letu hapa wengi wetu kama siyo 90% au 99% tumezaliwa baada ya muungano na hii ina maana kubwa sana kwa Taifa letu. Tafsiri yake maana yake ndiyo ukomavu wenyewe wa muungano wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, picha tuliyonayo hapa ndiyo picha ambayo ipo nje ya Bunge hili kwa wananchi. Kwa hiyo, wananchi wengi wamezaliwa baada ya muungano na ndiyo tafsiri ya uimara wa muungano wetu. Wamarekani wana phrase moja katika constitution yao nitaisoma kwa Kisukuma: “In order to form a perfect union.” Maana yake nini? Hata baada ya miaka 200 ya Muungano wa Marekani, they are still perfecting their union.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, maana yake nini kwa Mheshimiwa Waziri? Ni kwamba, kazi ya muungano is a working progress na wakati mwingine tunapitiwa sana vitu ambavyo ni very trivial, vitu vidogovidogo tunavitumia kuhoji misingi ya muungano na ni jambo ambalo kwa Watanzania ninafikiri ni vizuri sana tukajikumbusha kwa hilo na kujipongeza kwamba Muungano huu miaka 62 sasa hivi tukiwa very strong, tukiwa imara kama Taifa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kizazi, vijana wetu, ninafikiri Bunge letu 90% ni vijana. Wajue kwamba tunapozungumzia umoja wa Taifa hili na amani ya Taifa hili kifungashio chake ni Muungano. Ninataka nirudie hili inawezekana pengine halijasikika vizuri. Unapozungumzia umoja wa Taifa hili na amani ya Taifa hili, kifungashio chake (package yake) ipo ndani ya Muungano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni muhimu sana katika mambo haya tunapokuwa tunajikumbusha. Mheshimiwa Waziri Muungano ni working progress, tusiogope kufikiri especially katika mambo ambayo yanatuimarisha kimuungano, kwa sababu uimara wa kiuchumi ndiyo uimara wa muungano wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo mambo ambayo yanaweza yakajitokeza, pengine yapo nje ya yale ambayo ni kati ya kimuungano. Kwa mfano, suala la utalii yawezekana kabisa… na hili nilikuwa ninaliulizia, silizungumzii kinadharia, nilikuwa ninaulizia kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwamba hivi watalii wanapokuja 100 Zanzibar, wangapi wanakuja bara. Ukiangalia katika ratio wapo ambao wanakuja ku-spend muda Zanzibar baada ya hapo wanakuja safari lakini kuna watu ambao wanakuja safari baada ya hapo wanaenda Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni nini? Maana yake kama kuna ujenzi wa infrastructure ambazo zinaweza kutupa uimara kwa sababu ndiyo maana ya ku-leverage muungano wetu, tufanye tusiogope kwa sababu mambo fulani ambayo tumekubaliana haya hatujakubaliana. Tukae chini tuone kama kuna infrastructure au kuna mambo ya kufanya kuimarisha Zanzibar ili tuweze kupata watalii wengi kwa bara, basi tufanye hayo mambo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya pili nijikite kwenye mazingira na kwa bahati nzuri Mheshimiwa Waziri amezungumzia kwa uzuri sana kwamba mazingira ni nguzo katika nguzo tatu za Dira yetu ya 2050, ni nguzo tatu. Maana yake ukiondoa nguzo moja yale ambayo tunatarajia kuyafikia katika Dira 2050 hatuwezi kuyafikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ina maana gani Mheshimiwa Waziri katika Wizara yako? Maana yake Wizara yako inatoa uamuzi au inapelekea kuwa mwamuzi kama Dira hii tutaifikia au hatutaifikia. Sasa yapo mambo ambayo ni ya msingi yamezungumzwa kwa upande wa mazingira na umeyazungumza hapa Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mojawapo; la kwanza, kuimarisha mazingira yetu na hili ni suala mtambuka. Sasa kuna mengine unaweza ukazungumza kwa upande wako, lakini upimaji wa ardhi ndani ya nchi unalenga katika kulinda mazingira yetu. Kwa hiyo, hili maana yake ni kwamba Wizara yetu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira na Wizara ya Ardhi lazima kuwepo na proper coordination kuhakikisha kwamba tunakuwa na upimaji wa matumizi sahihi ya ardhi katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu huo ni mwanzo mzuri wa kuhakikisha kwamba tunatunza mazingira yetu. Kuna suala ambalo Mheshimiwa Rais amekuwa akili-champion sana la nishati safi na hii ninafikiri kama ni jambo ambalo tutaweza kumkumbuka sana Mheshimiwa Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan kuanzia akiwa bado Makamu wa Rais na sasa hivi akiwa Rais wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni suala la nishati safi pamoja na mambo mengine ambayo ametoka kuya-champion. Suala hili ni muhimu sana tukalikazania na ni vizuri tukawa na focus kwamba yapo maeneo pengine tuwe na focus kama ile ya, ninafikiri kuna mpango wa kaya zile ambazo hazijiwezi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri katika ku-target kwa ajili ya kuhakisha kwamba progamu hii inafanya kazi kukiwa na focus ya maeneo fulani fulani. Kuna baadhi ya maeneo yanaweza pengine kuwa na nafuu zaidi kiuchumi, lakini maeneo ambayo yapo disadvantage tuwe na focus kubwa sana. Ninashukuru katika hili nimekuwa mfaidika, Bariadi Vijijini tumeletewa majiko mengi sana kwa ajili ya nishati safi na wananchi wangu wanafurahia, ninajua kuna awamu nyingine inakuja na kwa hilo ninawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ambalo nilitaka kulizungumzia kuna suala la carbon credit, suala la carbon credit ukiangalia nchi yetu kwa maana ya national park na mapori tengefu almost karibu 32% ya nchi yetu. Kwa maana nyingine kwamba tuna advantage kubwa sana kama nchi ku-leverage katika hili na Wizara ya Fedha waone kama ni opportunity ya ku-utilize, kama ni sehemu mojawapo ya ku-finance baadhi ya miradi yetu hasa ambayo inahusiana na mazingira.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Kadogosa…

MHE. MASANJA K. KADOGOSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzungumza hayo, ninaomba kuunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)