Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia hoja ambayo imetolewa mezani. Kwanza, niseme kwamba ninaunga mkono hoja ya kuwapongeza Serengeti Boys. Pia ninampongeza aliyeleta hoja hii mezani, dada yangu Mheshimiwa Ester Bulaya, jirani yangu kabisa hapa, kwa kazi kubwa ambayo ameifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais amekuwa na mafanikio makubwa sana kwenye michezo, inawezekana ukipima ni kuliko Marais wote ambao wamewahi kuwepo katika nchi yetu. Kwenye sekta ya michezo kipindi cha Dkt. Samia tumefanya vizuri sana kwenye riadha, ngumi, football na hata kwenye timu kubwa ya Taifa tumefika 16 bora kwenye AFCON. Ni kitu kikubwa sana kwenye nchi yetu. Haya ni mafanikio makubwa sana kwa Mheshimiwa Rais na ndiyo maana CAF waliamua kumpa tuzo ya kutambua mchango wake kwenye michezo na kwenye mpira. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais alipokuwa anamwapisha Mheshimiwa Paul Christian Makonda alizungumza maneno haya; alisema, “Nina uhakika kazi ninayokupa unaiweza na mchaka mchaka huu unauweza.” Kwa haya yanayoendelea tunaona kabisa kwamba Wizara inafanya kazi kubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimuunge mkono Mheshimiwa Waziri, Paul Christian Makonda. Wizara ya Michezo sio Wizara ya kulala, ni Wizara ya mchakamchaka. Ni Wizara ambayo kila siku tunahitaji kuona matunda na tunahitaji kuona watu wakishughulika hapa na pale. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hata haya yanayoendelea ni kwamba ni kazi kubwa Wizara na Baraza la Michezo linafanya, lakini pia TFF wanafanya kazi kubwa. Nimuunge mkono Mheshimiwa Waziri na nimpongeze na tuna uhakika diplomasia ya michezo inatafsiriwa kwa vitendo siyo kwa kuzungumza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hawa vijana walichokifanya kule Rabat, Morocco, diplomasia ya michezo kati ya Tanzania na mataifa mengine inakua. Watu wanaendelea kuiangazia Tanzania kwenye sekta ya michezo na ndiyo maana kati ya watu wabobezi wa soka duniani Arsene Wenger jana amejitokeza akiipongeza Tanzania kwa kile ambacho wamekifanya. Ni lini tungempata Arsene Wenger akaipongeza Tanzania kama si kupitia mafanikio ya Dkt. Samia Suluhu Hassan? Kwa hiyo, ninaipongeza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza katika issue yoyote ile Mheshimiwa Waziri, Rais akiwa na political will ya kuendeleza michezo ndipo tunapoenda kufanikiwa. Tumeiona political will ya Mheshimiwa Rais kwenye kujenga infrastructures za michezo. Viwanja vinajengwa kila kona. Pili ni hamasa anayoitoa, goli la mama, anayoyafanya na maeneo mbalimbali ambayo anachagiza kuhakikisha kwamba ana-support timu zetu za michezo. Ni vyema tukaendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais. Pia Mheshimiwa Waziri asichoke, aendelee kuhamasisha michezo kwenye nchi yetu. Wapo watakaomkatisha tamaa, ni kazi yao lakini sisi tunachagua kusonga mbele katika kuhamasisha michezo. Mheshimiwa Makonda huu muziki anauweza kuucheza na ninajua kuwa yeye si kinara wa sifa tu, wakikuchukia wanakuchukia, wakikufurahia wanakufurahia, wewe unasonga mbele. Kwa hiyo, mimi ninamuunga mkono.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri kama tunawaunga mkono vijana hawa tafsiri yetu ni moja, Watanzania huko nje wanajiuliza swali moja, kwamba wakishatoka huko hatua gani zinafuata? Nitoe angalizo kwa Watanzania, tuna changamoto ya kuwa na mameneja uchwara, tuna changamoto ya kuwa na watu ambao wanaitwa mawakala, kwa hawa wachezaji na tuna changamoto ya kutokuwaandaa kisaikolojia hawa wachezaji. Kwa jinsi ambavyo wame-perform jana, ungekuwa unafuatilia michezo, wali-perform katika kiwango ambacho tunahitaji kama Taifa kuwaandaa vijana wakirudi basi tuwe na watu maalum ambao wataa nao kisaikolojia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, masoko maalum yaandaliwe kwa ajili ya hawa vijana, kuliko wakija wakakimbilia kwenye hizi timu nyingine ambazo zimekuwa na tamaa kuwachukua na kuwakalisha wachezaji bila kuwatumia. Basi tuwaandalie masoko ya kimataifa wachezaji wetu wakafanye vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaunga mkono wa hoja na ninaiunga mkono Wizara ya Michezo. Ninamtakia kila la heri Mheshimiwa Rais na hawa vijana tunaamini fainali tunabeba ubingwa, tunarudi nao nyumbani...
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
NAIBU SPIKA: Ahsante sana.
MHE. FESTO R. SANGA: ... lakini nimtakie kila la heri Mheshimiwa Waziri, Makonda, pamoja na timu nzima ya Wizara ya Michezo kuhakikisha kwamba tunamuunga mkono. Zaidi na TFF kwa kazi kubwa wanayoifanya. Kubwa zaidi ni kwamba...
NAIBU SPIKA: Ahsante sana.
MHE. FESTO R. SANGA: ...aliyeifikisha nusu fainali au fainali hii timu ni kocha ambaye ni mzawa, akina Mirambo na kocha mwenzake. Ni watu ambao ni Watanzania wenzetu. Ni jambo kubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Kama mdau wa michezo nina furaha na Watanzania wanafurahi kuona Serengeti Boys inafanya vizuri. Ahsante sana. (Makofi)