Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kuipongeza Timu ya Taifa ya Vijana Wanaume Chini ya Umri wa Miaka 17 (Serengeti Boys) kwa Kufuzu Fainali za AFCON 2026 na Kukata Tiketi ya Kushiriki Mashindano ya Kombe la Dunia la Vijana Chini ya Umri ya Miaka 17, Mwaka 2026

Hon. Jafari Wambura Chege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kuipongeza Timu ya Taifa ya Vijana Wanaume Chini ya Umri wa Miaka 17 (Serengeti Boys) kwa Kufuzu Fainali za AFCON 2026 na Kukata Tiketi ya Kushiriki Mashindano ya Kombe la Dunia la Vijana Chini ya Umri ya Miaka 17, Mwaka 2026

MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza ninaanza kuunga mkono hoja ya dada yangu Mheshimiwa Ester na niseme imekuja wakati muafaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kiukweli kwa moyo wangu wa dhati nimesimama hapa kuipongeza timu yetu ya Serengeti Boys kwanza kama mdau wa michezo, lakini na kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya vijana hawa kwa kuendelea kuipeperusha bendera yetu ya Taifa na kwa kuendelea kuonesha kwamba kumbe bado kama Taifa letu la Tanzania tunavyo vipaji mahiri vya vijana ambao wakiwezeshwa, wakipewa nguvu wanaweza kufanya vizuri katika soka la kimataifa. Vijana hawa kiukweli wametuonesha mfano mzuri sana wa kuigwa na nimesimama hapa kuwapongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haya hayawezi kutokea hivi hivi. Kama mdau wa michezo lazima niseme, haya yanatokea ni pamoja na maono mazuri ya utekelezaji wa Serikali hii ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Michezo ni pamoja na mazingira unayoandaa, ushindi unatengenezwa kutokana na mazingira unayoandaa kwa timu yako ili uweze kushinda. Hawawezi kwenda kushinda kama hawajajiandaa kisaikolojia, hawawezi kwenda kushinda kama sera za nchi hiyo hamuwa-support vijana wale katika michezo na hawawezi kushinda kama mazingira yenyewe hayajakaa katika kuwawezesha hawa vijana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mazingira ya sasa ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimiwa Dkt. Samia inawawezesha vijana hawa kwenda kifua mbele kushindana kwa sababu wanaamini nyuma yao yupo jemadari ambaye amesimama kwa ajili ya kuhakikisha kwamba michezo inapaa na ndiyo maana wamefanya kazi vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninachukua nafasi hii pia kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, niseme upele umepata mkunaji. Mheshimiwa Waziri kazi yako tunaiona, sisi kama vijana wenzako tunakuombea, tunatamani uendelee kukanyaga hapo hapo ulipokanyaga. Ninaamini katika awamu yako, kipindi chako hiki michezo utaifikisha mahali ambapo itatengeneza historia katika nchi hii kwa sababu nyuma yako yuko jemadari ambaye anakupa support ambaye ni Dkt. Samia na wewe unakwenda na unafanya kazi katika kutekeleza maono ya Mheshimiwa Dkt. Samia. Kanyaga hapo hapo Mheshimiwa Naibu Waziri tutafika kule tunakotaka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, michezo ni furaha, lakini michezo katika Taifa letu ndiyo inayotuunganisha sisi kama Taifa moja. Sehemu ya michezo ndiyo haina itikadi za kisiasa, haina ukabila, haina udini. Kazi kubwa iliyofanywa na hawa vijana imetuunganisha sisi kama Taifa. Vijana hawa wametoka kwenye maeneo mbalimbali katika utendaji wao wa kazi na kazi kubwa na nzuri wametuunganisha sisi kama Taifa. Tunawapongeza sana kwa kazi kubwa na nzuri iliyotukuka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninachukua nafasi kumshauri Mheshimiwa Waziri. Pamoja na mazuri utakayoyafanya vijana hawa wakirudi lazima tuone namna ya kuinua vipaji vyao. Tunazo academy hapa za football academy ndani ya nchi, lakini fikiria namna ya kuwapeleka vijana hawa kwenye academy za kidunia na academy zilizo bora za kimataifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaamini na sisi tunataka tupate wachezaji kama Messi wa kesho, tupate mchezaji kama Ronaldo wa kesho kwa kuwapeleka kwenye academy za kidunia, academy za kimataifa kama ambavyo zinavyofanya vizuri Barcelona academy, zipo academy kama Manchester academy. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukiwapeleka kule hawa vijana badala ya kubaki hapa Tanzania wanatapakaa, ukiwapeleka kule hawa vijana maana yake kesho yake tunakwenda kupata wachezaji wazuri wakirudi kutumikia Taifa hili kwenye timu ya Taifa. Pia utakuwa umewasaidia katika kuinua kipato chao na sehemu ya ajira kama sehemu ya ajira yao kwenye michezo ambayo wameamua kuichagua. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana.

MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikuombe sana iwe sehemu ya ahadi yako. Wape moyo hawa vijana waambie mkishinda nje na kubaki ndani ya Tanzania tuna namna ya kuwapeleka nje ili muendelee kuimarisha ujuzi, mpate maarifa na mtakaporudi kama Taifa muweze kutumikia Taifa kama Timu ya Taifa na ndiyo chanzo kizuri cha mchango wa Taifa kupitia sehemu hii ya michezo. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana, ninaunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)