Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadiro ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Adonis Alfred Bitegeko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadiro ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. ADONIS A. BITEGEKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi mahiri na wenye maono uliowezesha mageuzi makubwa katika Sekta ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawapongeza Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na watumishi wote wa sekta husika kwa kazi nzuri na maendeleo yakiwemo ya TEHAMA upande wa ardhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa ushauri ufuatao kwa Serikali :-

(i) Serikali kupitia Wizara itatue mgogoro wa muda mrefu wa mpaka kati ya Wilaya ya Muleba na Karagwe katika Kata za Rutoro na Rugera, Vijiji vya Rutoro na Omukakajinja, Vitongoji vya Rwamisha B na Kamzinzi.

(ii) Serikali iwezeshe usafiri wa ofisi za ardhi katika Halmashauri ya Muleba.

(iii) Serikali iwezeshe upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi katika visiwa vilivyopo Wilaya ya Muleba.

(iv) Maafisa Ardhi ajira zao ziwe chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI ili wawajibike kiutendaji. Hii itafanya shughuli za ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi kupewa kipaumbele katika halmashauri. Ofisi za ardhi katika halmashauri ziwezeshwe zaidi ili ziongeze kasi ya kupanga na kupima ardhi.

(v) Mapitio ya sheria yafanyike ili madalali wa ardhi/mashamba/viwanja na estate developers wadhibitiwe kisheria.

(vi) NHC wajenge nyumba za gharama nafuu zaidi zinazoweza kununuliwa au kupangishwa na wananchi wa kima cha chini kama madereva wa bodaboda na mama ntilie. Kuna haja ya Serikali kufanya mapitio ya sheria au kuweka utaratibu wa kuwa na mradi wa affordable houses na affordable houses fund.

(vii) Serikali iendelee kuweka mifumo thabiti zaidi ya kudhibiti udanganyifu unaoleta migogoro ya ardhi. Maafisa wa Wizara wanaoshiriki katika vitendo vya uvunjaji wa sheria wawajibishwe. Udanganyifu na utapeli kwa kutumia nyaraka za kughushi.

(viii) Serikali iweke madawati maalumu ya wanawake wajane, walemavu na wazee katika halmashauri ya kutoa huduma za ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi.

(ix) Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya na Kata yavunjwe na utaratibu wa mahakama utumike kwa kuwa yamekuwa hayafuati taratibu za kutatua migogoro

(x) Serikali iongeze kasi ya uhuishaji wa kumbukumbu za ardhi. Katika mwaka 2025/2026, Wizara ilipanga kuhuisha kumbukumbu za wamiliki wa ardhi 500,000. Hadi tarehe 15 Mei, 2026, kumbukumbu za ardhi 146,345 zimehuishwa.

(xi) Serikali iongeze kasi ya uandaaji na usajili wa hati na nyaraka za kisheria za umiliki wa ardhi kwa wananchi na taasisi. Katika mwaka 2025/2026, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilipanga kuandaa na kusajili hatimiliki 500,000 na hati za hakimiliki ya kimila 520,000. Hadi tarehe 15 Mei 2026, Wizara ilikuwa imeandaa na kusajili hatimiliki 107,683 sawa na asilimia 21.54 ya lengo; hati za hakimiliki ya kimila 99,762 sawa na asilimia 19.19 ya lengo.

(xii) Serikali iongeze kasi kutoa huduma za uthamini na usajili wa nyaraka zinatolewa kupitia Mfumo wa e-Ardhi nchi nzima.

(xiii) Serikali ifanyie kazi na kuondokana na uwepo wa mitaa mingi ambayo imeendelezwa bila kupangwa na kupimwa.

(xiv) Serikali ifanyie uwepo wa trading centers nyingi ambazo zinahitaji kutangazwa, kupangwa, kupimwa na kumilikishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.