Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Josephine Tabitha Chagulla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. JOSEPHINE T. CHAGULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi hii, niweze kutoa mchango wangu katika hotuba hii ya Wizara ya Afya iliyoko mbele yetu. Ninaanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema kwa kunijalia afya njema na kuweza kusimama hapa leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa jinsi anavyopambana kuhakikisha Watanzania na nchi yetu inasonga mbele. Nampa hongera sana Mama yetu kipenzi kwa kazi nzuri. Pia, ninampongeza sana Waziri Mkuu pamoja na Baraza lote la Mawaziri kwa jinsi wanavyomsaidia Mheshimiwa Rais. Hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana Waziri wa Afya, Mheshimiwa Mchengerwa, pamoja na Naibu Waziri, wifi yangu. Hongera sana kwa kazi nzuri wanazofanya kuhakikisha afya za Watanzania zinakaa imara. Hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na muda, ninaenda moja kwa moja kwenye mchango wangu. Katika Mkoa wa Geita tuna Hospitali ya Kanda ambayo iko Chato. Hospitali hii imekuwa ni msaada mkubwa sana katika ukanda ule. Wananchi wengi wameweza kunufaika pale. Hospitali ile inatoa huduma mbalimbali nzuri, na pia huduma za kibingwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeweza kushuhudia wananchi wengi wanatoka sehemu mbalimbali, wengine kutoka Uganda, kuja katika hospitali ile kupata huduma. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuweza kutujengea Hospitali ya Kanda katika Mkoa wa Geita. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto kidogo kuhusu upungufu wa madaktari bingwa. Kwa sasa tuna madaktari bingwa wawili. Ninaomba sana Serikali iweze kutupatia madaktari bingwa wa kutosha kulingana na mahitaji ya pale. Wagonjwa ni wengi na huduma ni nzuri sana. Ninaomba sana Mheshimiwa Waziri aweze kuliona hilo na kutupatia madaktari bingwa ambao watatosheleza mahitaji ya hospitali yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisemee Hospitali yangu ya Mkoa wa Geita. Hospitali ya Mkoa wa Geita inatoa huduma nzuri sana. Tunamshukuru sana Mganga Mkuu wa pale, lakini pia, tunawashukuru sana Madaktari Bingwa wa Watoto, Daktari Bingwa wa Akinamama, pamoja na madaktari wengine wote, wanafanya kazi nzuri sana kwa kiwango cha juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto iliyopo pale ni ukosefu wa jengo la mama na mtoto. Jengo la mama na mtoto bado halijakamilika, ujenzi wake umesimama kutokana na upungufu wa fedha. Pia, mortuary haijakamilika. Ninamwomba sana Waziri, Mheshimiwa Mchengerwa, alione hilo, atupatie fedha ambazo zitaweza kukamilisha jengo hili, ili akinamama na watoto wawe na jengo lao kwa sababu, kwa sasa wazazi inabidi wachanganyike na wagonjwa wa kawaida, kitu ambacho ni hatari sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ninaunga mkono hoja. (Makofi)