Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. KIJAKAZI Y. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangia hotuba ya bajeti ya Wizara hii muhimu sana kwetu sisi Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote na mimi nitumie nafasi hii kwa niaba ya wanawake wa Mkoa wa Lindi na wananchi kwa ujumla, wamenituma nimshukuru na nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa mengi aliyoyafanya katika sekta kwenye Mkoa wetu wa Lindi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaendelea, ninampongeza sana babu yangu, mtani wangu Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa, pamoja na Naibu wake, Waziri na Watendaji wote wa Wizara ya Afya wakiongozwa na Katibu Mkuu, wanafanya kazi nzuri, kazi kubwa, kazi iliyotukuka. Tunawashukuru sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianzia, pale katika mkoa wetu wa Lindi, imewekezwa takribani shilingi 9,000,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa pamoja na vifaatiba. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa niaba ya wanawake wa Mkoa wa Lindi na wananchi kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nimshukuru sana Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa, kwa sababu baada ya majengo yale kukamilika ulipita muda kidogo kabla ya kuanza. Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa baada ya kuteuliwa tu kuwa Waziri, alifanya jitihada kuhakikisha kwamba hospitali ile ya rufaa inaanza kazi. Tunashukuru sana. Pamoja na kwamba hospitali ile imeanza kazi, tunazo changamoto, majengo hayajakamilika kwenye hospitali ile. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti iliyopita, tuliahidiwa au ilitengwa shilingi bilioni 5.4 ambayo hadi sasa haijaenda. Inawezekana fedha ile ingeenda, ingeweza angalau kukamilisha baadhi ya majengo. Ilitoka almost shilingi 1,000,000,000 tu ambayo ilienda kumlipa mkandarasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, changamoto ni kubwa kwa sababu moja kati ya changamoto ni majengo ya kulaza wagonjwa (Wodi) ambapo kwa sasa majengo ambayo yanayotumika ni ya OPD pamoja na jengo la ICU. Wodi hizo ni pamoja na wodi ya mama na mtoto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana Mheshimiwa Waziri atakapokuja ku-wind up atuambie wananchi wa Mkoa wa Lindi ni lini majengo yale yatakamilika? Ninaomba commitment ya Serikali, kwa sababu nimesikia asubuhi Mheshimiwa Naibu Waziri akieleza kwamba mwaka huu Disemba hospitali ile itakamilika. Kwa hiyo, tunaomba commitment ya Serikali na watwambie mipango na mikakati ipi ambayo wataitumia kuhakikisha kwamba hospitali ile muhimu kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi inakamilika. (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa
muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Muda wako umeisha.
MHE. KIJAKAZI Y. MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ninaunga mkono hoja. (Makofi)