Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. SALUM MWINYI REHANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka kujikita zaidi kwenye suala zima la kilimo. Bajeti haikumtazama mkulima, haikutazama kilimo kwa ujumla wake. Mimi kilichonisikitisha zaidi, bajeti ya mwaka uliopita pembejeo zilitengewa karibu zaidi ya shilingi bilioni 50, lakini mwaka huu ambao tunajiandaa kuwa Tanzania ya viwanda pembejeo haikuzidi shilingi bilioni 20. Sasa tunaposema kwamba tuna lengo la kuongeza uzalishaji au kupata mazao kwa ajili ya viwanda, mazao haya yatapatikana vipi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia tathmini ya pembejeo zilizotoka miaka iliyopita siyo zaidi ya asilimia 10 kwa wale wasambazaji wa pembejeo, wakulima walikuwa wanapata pembejeo hizo katika maeneo yao. Hali hii mwaka huu tunaitazama kwa jicho gani? Obvious, uzalishaji utashuka. Hakuna njia ya mkato, uzalishaji utashuka kwa sababu hakuna pembejeo ambazo zitatosha kwa ajili ya kuwafanya wakulima hao waweze kuzalisha.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala hili litaathiri maeneo mengi, litaathiri kwanza wazalishaji wenyewe, litaathiri zile Taasisi na Mamlaka tulizoweka kwa ajili ya kununua mazao katika maeneo yao mbalimbali na hasa kwa zile taasisi ambazo tumeziweka zinunue chakula kwa ajili ya chakula cha akiba na kile cha ruzuku, hakutakuwa na chakula cha kutosha kwa hali inavyokwenda. Vilevile athari nyingine iliyojitokeza hapa ni kufungua milango kwa private sector au waleta pembejeo binafsi kuweza kuleta hizi pembejeo na kuziuza kwa bei ya juu sana kwa sababu ndiyo mahali pekee panapopatikana hizi pembejeo.
Mheshimiwa Naibu Spika, niliona kwenye ripoti au taarifa ya Kamati ya Bajeti na tulilipeleka kama Wajumbe wa Kamati ya Kilimo suala hili liongezewe fedha na lipewe msukumo maalum ili kuwafanya wananchi wa nchi hii waweze kuzalisha kwa uhakika na ile surplus itakayopatikana iweze kupelekwa kwenye hivyo viwanda ambavyo tunataka tuvianzishe. Wasiwasi wangu, mpango mzima wa kuanzisha viwanda katika maeneo haya hasa kwa kutumia raw materials za kilimo utaweza kuathirika na vinginevyo usiweze kufanyika kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka kuzungumza kwenye suala zima la kilimo cha umwagiliaji maji. Bado Serikali hapa haijawa na kipaumbele. Tanzania hii ya leo iliyokuwa imeathirika na mazingira na hali ya hewa katika maeneo mbalimbali vyazo vingi vya maji vimepotea, hata yale unayochimba sasa hivi unayochimba katika urefu mkubwa sana kwenda chini, water table imeshuka. Njia pekee ya kulima ni kutumia umwagiliaji. Scheme zetu zilizokuweko nyingi zimechoka zimetengenezwa zamani na zile zinazotengenezwa sasa hivi speed ya utengenezaji wa hizo scheme mpaka kuwafanya wakulima waweze kulima kwa kutegemea maji ni ndogo, lakini fedha vilevile zilizotengwa kwa ajili ya masuala mazima ya umwagiliaji maji ni kidogo sana. Sasa nina wasiwasi nia ya kweli ya dhati ya Serikali ya kuhakikisha kwamba wakulima hawa wana uhakika wa kulima iko wapi.(Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninamuomba Waziri wa Fedha aangalie sana, tuwe na mpango maalum wa kuhakikisha kwamba tunaongeza maeneo ya umwagiliaji angalau asilimia kumi kila mwaka ili tuwe na uhakika wa uzalishaji wa mazao mbalimbali na kuweza kuwafanya wakulima wetu wawe na uhakika wa uzalishaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine katika hilo ni suala zima la utafiti. Nchi yoyote katika eneo ambalo linatakiwa liwe na kipaumbele utafiti ni eneo mojawapo kwa sababu ndipo mahali ambapo unapata hizo facts. Nina-declare interest kwamba na mimi niluwa mtafiti kwa zaidi ya miaka nane, ninajua machungu, adha na taabu za utafiti kama hakuna fedha zinazotikawa. Leo hakuna msukumo wa fedha ambazo zinakwenda kwa watafiti moja kwa moja wakati watafiti wale tayari wameshaanza kazi kubwa ya miaka mitatu, miaka minne kutafiti aina mbalimbali, aidha, mbegu, au maradhi mbalimbali au dawa au ufumbuzi wa tatizo ambalo limekabili katika eneo fulani. Leo hii kama hakuna fedha ambazo zinapelekwa katika m