Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. MARY D. MURO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kama ifuatavyo:-
(i)	Naishauri Serikali kuangalia upya kuhusu pembejeo kwa ajili ya kilimo kufika mapema kulingana na misimu na pia mbegu ziboreshwe;
(ii)	Serikali ijitahidi kuwajali wagani tulionao kwa kuwapa vitendea kazi, usafiri wa kuwafikia wakulima wetu;
(iii)	Nashauri Serikali itoe elimu ya ufungashaji ambayo imegharimu mazao yetu yanafungashwa Kenya na kusafirishwa hivyo kupata fedha nyingi kuliko wakulima;
(iv)	Nashauri Serikali kuangallia jinsi dawa zinavyohifadhiwa kwani kuna nyingi ni sumu na zinaharibu afya za wananchi;
(v)	Nishauri Serikali kuhakikisha wanashughulikia miundombinu ya kutoa mazao mashambani;
(vi)	Nishauri Serikali kuelimisha wananchi juu ya uuzaji mazao siyo kuzuia tu kwani mwananchi anatakiwa kuuza ili kununua mahitaji mengine.