Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuwa na uchumi imara na kuwa na mchango mkubwa wa pato katika uchumi ni muhimu Wizara kama msimamizi wa uchumi nchini iwe na kipaumbele katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Nashauri kwamba Wizara iwekeze katika viwanda vinavyohusiana na kilimo ili kuchochea uchumi wa viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo jema kuwa suala la pension kwa wastaafu limezingatiwa katika bajeti hii. Nashauri kwamba uhakiki ukamilike mapema na malipo yafanyike kwa wakati wakiwemo waliokuwa watumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni muhimu sana katika kudhibiti nidhamu ya matumizi Serikalini, lakini imekuwa haiwezeshwi kwa kiwango cha kutosha. Hivyo, nashauri CAG apewe fedha za kutosha kulingana na bajeti yake na fedha hizo zipatikane kwa wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Benki ya Maendeleo ya Kilimo kwa umuhimu wake ipewe mtaji wa kutosha na kutanua mtandao  wake  ili  iweze  kuwafikia  watu  wengi  zaidi wanaohitaji huduma yake hasa walioko vijijini, mfano, Ukerewe. Pia ukopeshaji katika benki hii utoe fursa vile vile kwa Sekta ya Uvuvi kunufaika na benki hii jambo ambalo litaongeza sana nguvu ya kiuchumi ya watu wetu hasa vijijini.