Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
							Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. SUZANA C. MGONOKULIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ningependa kutumia nafasi hii kuainisha upungufu unaofanywa na baadhi ya Jeshi la Polisi. Polisi kazi yao ni kulinda wananchi na mali zao, mipaka ya nchi na pia kuhakikisha amani inapatikana. Pia kudhibiti uhalifu wowote unaoweza kutokea ndani ya nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kwa sasa imekuwa ni kinyume na hayo, Jeshi letu la Polisi limepoteza uaminifu kwa wananchi wake kutokana na vitendo wanavyofanya. Kwa mfano, wananchi kubambikiwa kesi awapo kituoni. Unakuta mtu ana kesi ya kupiga mwenzake anaambiwa ameiba na kuvunja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuzuia mikutano ya vyama vya siasa kinyume na taratibu ya Katiba ya nchi. Hivyo ningeomba Waziri mwenye dhamana aelekeze Jeshi la Polisi majukumu yao halisi na siyo vitendo vya uonevu wanavyovifanya sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Askari wanapenda rushwa na kuchelewesha kesi Mahakamani sababu wanachopewa hakiendani   na   kazi   wanazofanya.   Hivyo   naomba waongezewe mishahara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia na makazi ya baadhi ya askari nchini hayaridhishi na  yanaenda  kinyume na mila na desturi ya nchi yetu. Unakuta mtu anaishi kwenye chumba kimoja na ana familia, chumba kinatenganishwa na pazia au ma-box. Je, hayo  ni maadili gani? Hao askari wanatembelewa na ndugu zao, uhuru hawaupati kabisa. Namwomba Waziri, Mheshimiwa Mwigulu  jambo hili litazamwe kwa makini japo wakirudi  majumbani kwao kupumzika wapumzike vizuri ili wakirudi kazini warudi na nguvu nzuri.