Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nsimbo
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuungana na Wabunge wenzangu kwa ajili ya hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyokuja Novemba 14.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kupata kura nyingi za kishindo kupitia wananchi waliomchagua tarehe 29 Novemba, 2025. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Spika pamoja na wewe kwa kuaminiwa na Wabunge kuwa mtuongoze katika Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba niwapongeze Wabunge wote waliokuwa ndani ya Bunge hili kwa kuchaguliwa na wananchi na kuaminiwa; tuko mahali hapa kwa ajili ya kujenga Taifa letu la Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba niwashukuru wananchi wa Jimbo la Nsimbo kwa kuniamini tena kurudi tena katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nichangie hotuba ya Mheshimiwa Rais. Ninaomba nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa maono makubwa aliyonayo katika utekelezaji wa kazi mbalimbali za nchi yetu ya Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninampongeza Mheshimiwa Rais kwa sababu gani? Kwa sababu tumeona jinsi gani alivyoanza. Alikuja hapa akasema, utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi utaanza ndani ya siku 100. Tumeona mawaziri kupitia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu pamoja na Mawaziri wote kwa kazi kubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba tumpongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kazi kubwa ambayo ameendelea kuifanya katika nchi yetu. Tumeona akitembea katika maeneo mbalimbali na kutatua matatizo ya wananchi. Vilevile Mawaziri na Manaibu Waziri tumeona kazi ambazo mnaendelea kuzifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaona kazi kubwa ya afya iliyofanywa na Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwatibu Watanzania. Ndani ya mikoa yetu tuna Hospitali za Mikoa, ambazo zimewekwa vifaa vyote ambapo sasa hivi mikoa yote wanajitegemea, hatutegemei tena Muhimbili.
Mheshimiwa Naibu Spika, kila mkoa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amehakikisha amejenga hospitali ya rufaa, na kuhakikisha anaweka vifaa tiba, na vifaa vyote muhimu kwa ajili ya Watanzania. Alisema, amefanya na amethubutu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima tumpongeze kwa sababu Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ana maono makubwa. Sisi wenyewe ni mashahidi, tumeona vitu ambavyo amevifanya katika nchi yetu kupitia zahanati, na kupitia vituo vya afya.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii katika maeneo yetu ya vijijini na vitongojini kuna zahanati na kuna vituo vya afya, wananchi wanatibiwa huko katika maeneo yao ya vijiji, wanajifungua vizuri. Zamani mwanamke alikuwa anatembea maili sita au saba, lakini sasa hivi hakuna. Ambulance zipo. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amepeleka ambulance kwenye kila eneo la vituo vya afya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunakuja kwenye kipengele kingine cha barabara. Amewezesha TARURA, sasa hivi vijiji na vitongoji ameviunganisha, tumejengewa madaraja ambayo hayo yote yalikuwa hayapo, ameyafanya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, na amefanya mambo makubwa ambayo hatukuyatarajia. Kwa hiyo, ni lazima leo tumpongeze kwa kazi kubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona ni jinsi gani Mheshimiwa Rais ameleta fedha katika halmashauri zetu. Ameleta fedha nyingi ambazo hazikuwepo. Halmashauri ilikuwa haina fedha, lakini leo halmashauri wana miradi ambayo mpaka sasa hivi wanashindwa kuifanya kwa sababu ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono mapana aliyokuwa nayo kwa ajili ya Watanzania. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ana haki ya kupata kura za kishindo za 97%. Nni halali yake kwa sababu kazi kubwa imefanyika kupitia Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunakwenda kwenye utalii. Watalii katika nchi yetu walikuwa wanaingia wachache sana. Mimi katika jimbo langu nina Mbuga ya Katavi, kulikuwa hakuna watalii kabisa, lakini kupitia Royal Tour ya Mheshimiwa Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alikwenda kukaa porini kutafuta na kuhakikisha kuwa ana-promote utalii ili watalii waweze kuja katika nchi yetu ili tupate uchumi mkubwa na mapato makubwa. Sasa hivi tunaona watalii wengi ndani ya nchi yetu ya Tanzania, mapato yameongezeka, na watalii wa ndani na nje wote sasa hivi tunakwenda katika mbuga zetu kupitia hamasa ya Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hayo yote ameyafanya, tumeyaona na kuyahakikisha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona kwenye kilimo, kulikuwa na mazao ya kahawa, tumbaku, na pamba ambayo yalikuwa yalikuwa yana bei ya chini, lakini Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuja na mikakati ya kilimo kupitia mazao ya kibiashara ya pamba, tumbaku, kahawa, pamoja na korosho, leo hii tunaona jinsi wananchi walivyo na furaha na mapato ya mazao hayo ambayo Dkt. Samia Suluhu Hassan amehakikisha kuwa yamekuwa katika hali ya kiuchumi zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunaona ni jinsi gani ambavyo pembejeo, mbolea, na mbegu, zimefika kwa wakati katika maeneo yetu ya vijijini. Sasa hivi mbolea inakwenda mpaka kwenye vijiji, mbegu zinakwenda mpaka kwenye vijiji, mbegu zimeondolewa ushuru, sasa hivi mkulima anapewa mbegu kwa bei nafuu ili aweze kulima kwa ajili ya manufaa na uchumi wa nchi yetu ya Tanzania. Haya yote yalikuwa hayapo, ameyafanya Dkt. Samia Suluhu Hassan. Leo wananchi wana haki ya kumpa kura zote za ndiyo kwa sababu ameyafanya mambo makubwa na mazito katika nchi yetu ya Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona umeme katika nchi yetu ya Tanzania vijiji vyote, sasa hivi tunaelekea kwenye vitongoji. Umeme ulikuwa haupo, lakini Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameingia kuhakikisha vijiji vyote sasa hivi tunaenda kumalizia kwenye vitongoji. Ina maana shughuli za viwanda, shughuli ndogo ndogo, wananchi ndani ya vijiji vyetu na vitongoji vyetu wanafanya shughuli zao kwa amani na utulivu.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunamshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia amani ya nchi yetu ya Tanzania, kwa sababu ameisimamia na kauli zake tunazion. Hata kama kulikuwa kuna changamoto ambayo imetokea, lakini alipotoa kauli, Watanzania wote wamejitafakari, wameona lile lililotendeka siyo sahihi kwa sababu tumeibomoa wenyewe nchi yetu ya Tanzania. Haya mambo hayakuwepo, wameona uchungu ule wa kukaa ndani, lockdown ya siku tano, wanasema loo, kumbe hivi ndivyo ambavyo huwa inakuwa? Wenzetu ndivyo ambavyo huwa wanavyopata taabu, namna hii? Leo hii hatutaweza kurudia tena. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vijana walikuwa hawakopeshwi pikipiki, lakini ndani ya halmashauri zetu vijana sasa hivi wanakopeshwa pikipiki, wanakopeshwa 10%, imesimamiwa vizuri, wanapata mikopo, wanafanya shughuli za kilimo, wanafanya shughuli za mashamba kwa mahekta. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lazima tumpongeze Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo ameifanya kwa kipindi cha miaka minne iliyopita. Kazi kubwa na Watanzania wameiona, Watanzania wamethamini, unyenyekevu wake, wamethamini. Ninaomba sisi Watanzania, sasa hivi kilichobaki kwetu ni kuendelea kumwombea Rais wetu maisha marefu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi, ninaunga mkono hoja. (Makofi)