Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu 2026/2027–2050/2051, Mapendekezo ya Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2026/2027–2030/2031 na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2026/2027; na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali Katika Muda wa Kati ya 2026/2027 hadi 2028/2029.

Hon. Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu 2026/2027–2050/2051, Mapendekezo ya Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2026/2027–2030/2031 na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2026/2027; na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali Katika Muda wa Kati ya 2026/2027 hadi 2028/2029.

MHE. KENETH E. NOLLO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitumie nafasi hii nikupongeze wewe kwa kupata nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Bunge. Pamoja na yote, vilevile niishukuru Serikali kwa kuleta mpango huu wa miaka mitano pamoja na mpango huu mrefu kwa ajili ya kujadili dira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaanza mchango wangu, nilitaka ninukuu sehemu ya Hotuba ya Waziri aliyowasilisha hoja hii kwamba, Tanzania ina historia ndefu ya kuandaa mipango ya maendeleo. Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu wa kwanza uliandaliwa mwaka 1964 na maelezo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo mipango hii haikutekelezwa kikamilifu kutokana na changamoto za kiuchumi zilizoikumba dunia na nchi yetu ikiwemo ukame na hali mbaya ya hewa, kuharibika kwa soko la mafuta duniani na vita ya Tanzania na Uganda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto hizi mbili ambazo Waziri amezionesha za suala la ukame na suala la kupanda bei ya mafuta duniani bado zipo zinazunguka. Suala la ukame kwa kiasi kikubwa bado tunategemea kilimo cha mvua. Kwa hiyo, tatizo hili bado lipo kama ambavyo liliharibu mipango ile ya nyuma, tatizo hili bado hatujalitatua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni suala la mafuta na uhakika wa mafuta katika nchi yetu. Mabadiliko makubwa yanatokea hasa katika nchi zinazozalisha mafuta, lakini tunaona hali ya usalama katika nchi za Mashariki ya Kati. Vilevile, tunaona namna ambavyo Mataifa makubwa hasa Marekani yanavyotoka katika mradi wa kufanya biashara na zaidi ya kutumia niseme mabavu katika biashara hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sisi Tanzania kama watumiaji wa mafuta ambayo kwa kiasi kikubwa 100% tunaagiza kutoka nje. Serikali ina mpango gani wa kuangalia kwamba 1974 tulifungua mtambo wetu wa kusafisha mafuta (Tiper) na zao lake, tumeona kama tumefanya ya kupeleka mafuta Zambia ile crude oil.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tumepata mafuta kutoka Uganda, na sisi ni sehemu ya bomba lile. Naishauri Serikali ione namna ya kuanza kusafisha mafuta hapa nchini. Lengo letu ni tuwe na uhakika wa mafuta badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili tukilifanya, kwanza tutaweza kuhudumia nchi nane ambazo zitatutegemea sisi kwa ajili ya kuingiza mafuta hapa nchini. Suala hili Serikali haiwezi kusema ni gumu, tulishalifanya kupitia Tiper. Mimi ninaomba mpango huu tuufufue ili Tanzania sasa iwe ni sehemu ya kuzalisha mafuta na kuzalisha nchi nyingine ambazo zinatutegemea katika ukanda wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika suala zima la uchumi ukiangalia mpango na dira, Serikali inasema tuwe na ustawi mzuri wa Uchumi, lakini kubwa zaidi tunalenga katika sekta binafsi. Mimi ninataka niseme na Serikali iangalie bado uchumi wa dunia sasa unaongozwa na Serikali. Tukichukua mfano wa China, mashirika 362 yote yanaongozwa na Serikali (state owned enterprises).

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili siyo baya, na wala siyo aibu kwa Serikali kufanya biashara, lakini kufanya biashara katika maeneo ambayo yanahitaji mitaji mikubwa sana. Kama nilivyosema, kwa mfano, China yale mashirika yanayomilikiwa na Serikali 100% yako mashirika 100.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye majimbo kama halmashauri zetu ni karibu mashirika 150. Halafu yapo mashirika yanayoendeshwa na wawekezaji, Serikali ina mkono wake pale, ndiyo inafika karibu 362. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii maana yake ni nini? Tukiweza kuwekeza fedha zetu katika maeneo ambapo unahitajika mtaji mkubwa, tutakuwa na uchumi himilivu bila kutegemea fedha kutoka nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashauri nchi yetu ifanye uamuzi katika maeneo matatu. Kwanza, uzalishaji wa chuma ambapo ndiyo fedha nyingi nchi yetu inaingiza, na chuma hiki tunachopata ni chuma chakavu, tunakirudisha lakini hatujawa na chuma ghafi cha kuweza kuzalisha chuma. Chuma hicho tukitumie sisi wenyewe, na pia tukiuze katika nchi zinazotutegemea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina uwezo wa mtaji, inaweza ikaamua kuanza uzalishaji wa chuma. Story ya Liganga na Mchuchuma imechukua muda mrefu sana, lakini story hii ya Liganga na Mchuchuma ipo kampuni ambayo inatoka kwenye jimbo mojawapo la China. Is a state-owned company.

Mheshimiwa Mwenyekiti, imetuchukua muda mrefu sana. Mimi siamini kuwa Serikali haina uwezo wa kuanza ujenzi na kiwanda cha pale Mchuchuma kwa ajili ya uzalishaji wa chuma. Jambo hili tunalifanya. Kielelezo cha kujenga SGR ni kielelezo cha kuonyesha nchi hii inaweza kufanya jambo lolote ikiamua kuwekeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema, China sasa ameenda katika suala zima la madini. Ameanzisha Kampuni kubwa ya rare earth minerals. China sasa anazalisha yale madini yanayohitajika sana duniani. Wana kampuni yao ya kuzalisha mafuta, The PetroChina, lakini The China Minmetals kwa ajili ya chuma, zinc, na copper, na wana China Coal kwa ajili ya aluminium.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa na sisi kwa nini tusizalishe dhahabu? Nchi yetu ina dhahabu nyingi, kwa nini Serikali isiingize mkono tuanzishe shirika? Tunayo STAMICO, tuweke mtaji mkubwa wa kuzalisha dhahabu ambapo tutaenda kiwango sawa kama akina GGM na akina Barrick. Ninaiomba sana Serikali, suala la kuwekeza kwenye dhahabu nchi yetu itapata dhahabu za kutosha, tutaweza kuuza na tutakuwa na uchumi mkubwa kupitia uzalishaji wa dhahabu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni textile, uzalishaji wa nguo. Sote ni mashahidi kwamba nchi yetu kwanza imekaa katika lango, kwamba nchi zinazotuzunguka zinategemea importation kupitia nchi yetu. Jirani yetu ambaye vilevile ana sifa kama za kwetu anakwenda speed kubwa katika uzalishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ethiopia ambaye ana sifa kama za kwetu anazalisha sana textile. Katika jambo hili tuondoe story za Urafiki, na za Musoma Textile. Vile ni viwanda vya zamani, hatuwezi kuvifufua. Serikali iamue kabisa kwamba ianze uzalishaji wa nguo ambapo tutahudumia watu wetu na nchi zinazotuzunguka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni suala la uwekezaji mkubwa katika kilimo. Fedha nyingi tunaitumia katika kuagiza ngano katika nchi yetu. Suala hili kama nilivyosema, na kwenye mpango huu, Serikali iangalie. Kwanza matumizi ya jembe la mkono tuseme jambo hili tunakwenda kulikomesha kama ambavyo tulimtua mama ndoo kichwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, matumizi ya jembe la mkono kwanza ile ni corporal punishment, hatuwezi kwenda nayo. Kwa hiyo, Serikali ije, kama hatuwezi kwenye matrekta, basi hata majembe ya kukokotwa na ng’ombe. Tuwe na timeline ya kuli-phase out jembe le mkono. Serikali iliangalie jambo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, takribani kaya milioni saba bado zinatumia jembe la mkono. Sasa hatuwezi tukawa na uzalishaji wa kilimo kama tutatumia jembe la mkono. Kwa hiyo, Serikali katika mpango wake ninadhani iweke timeline kwenye dira, kwamba mwaka 2030 au mwaka 2035 jembe la mkono sasa likae kwenye maktaba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo ninakushukuru. Ahsante sana, ninaunga mkono hoja. (Makofi)