Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchagia. Kwanza kabla sijachangia mpango ninawatoa hofu wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ipo kwa ajili yao, haijatoa maelekezo yoyote ya kuwasumbua wananchi wa Nyatwali, haijatoa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi nimetoka kuzungumza na Waziri wa Utalii na Waziri wa Ardhi, tayari ametoa maelekezo. Hakuna mtu wa kuwasumbua wananchi wa Nyatwali mpaka jambo lao liweze kukamilika; tayari nimeshalifanyia kazi Mbunge wao wa kazi kwa vitendo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninachangia mpango. Mheshimiwa Waziri na Waheshimiwa Wabunge, tutakubaliana kwamba, chakula, mazao, mbegu, ni usalama wa nchi. Bila mbegu bora hakuna chakula cha kutosha, bila mbegu bora hakuna mazao na, bila mazao bora hakuna masoko. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa letu lina mahitaji ya mbegu tani 250,000, lakini uwezo wa Taasisi yetu ya ASA pamoja na wawekezaji binafsi wanaolima mbegu capacity yetu, ya uzalishaji wa mbegu, ni tani 70,000 inayobaki tunaagiza. Ni risk pia kwa Taifa letu watu wakiamua kuchochea vita ya kiuchumi kupitia sekta ya kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tafiti zilizofanywa, Mheshimiwa amezungumzia ukame, mbegu zinazozalishwa nchini kupitia Taasisi yetu ya Serikali ASA na wazalishaji binafsi zina uwezo wa kuhimili ukame. Sasa kwa nini, tusiiwezeshe Taasisi ya Serikali ya Wakala wa Mbegu (ASA) wakawa na uwezo wa kuzalisha mbegu za kutosha? Kwa nini, tusiwawezeshe wawekezaji binafsi wanaozalisha mbegu nchini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, wao wanazalisha tani 61,000. Taasisi ya Kiserikali ya ASA inazalisha tani 9,000 na hapo wana hekta 13,000. Zinatosha kwa uzalishaji wa mbegu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, imagine, mbali na kutegemea mvua kwenye hiyo tani 9,000, ASA inachangia mapato ya Serikali shilingi bilioni 11 leo hii kwa hizo hekta 13,000. Kwa hii ASA (Wakala wa Mbegu) tukiweka miundombinu ya umwagiliaji itakuwa ina uwezo wa kuzalisha mbegu tani 22,000 na kuiwezesha Serikali kupata mapato shilingi bilioni 33. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, imagine tukiwapa eneo lenye umwagiliaji wa hekta laki moja, ASA itazalisha mbegu kiasi gani? Tukiwawezesha wawekezaji wa ndani wanaozalisha mbegu tani 61,000, tukawawekea mazingira mazuri wana uwezo wa kuhakikisha usalama wa mbegu wa nchi yetu ni mkubwa na tusiagize mbegu nje ya nchi. Mbegu ni usalama wa nchi, mbegu ni uhakika wa chakula, mbegu ni uhakika wa soko, halafu unakwenda kwenye masuala mengine ya pembejeo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia huu mpango umesema zaidi ya 70% zitaenda kwenye sekta binafsi. Sekta binafsi utakuta kwenye kilimo, kwenye uvuvi, kwenye viwanda, leo hii kwenye sekta ya kilimo tunazo hekta milioni 29.4 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, leo hekta ambazo zimeunganishwa mfumo wa umwagiliaji ni hekta 700,000 peke yake na tumeona mwaka huu tumekuwa na tishio ya hali ya hewa ya mvua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi leo tukiamua kuwekeza kwenye sekta ya umwagiliaji, tukasema tunafunga mkanda, tunaanza na hekta milioni tano, kwa wakulima wadogo wadogo kuunganishiwa mfumo wa umwagiliaji tutaongeza pato letu pia tutakuwa na uhakika wakulima muda wote eneo ambalo walikuwa wanalima kwa msimu mara moja watalima mara mbili, pili pato la mkulima mmoja mmoja litaongezeka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri hata ile idea yako ya kusema lengo la kufikisha pato la Mtanzania mmoja mmoja mwaka 2050 kufikia dola 7,000 itatekelezeka kama haya yakikamilika hata huko 2050 hatufiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakutolea mfano tu kwa mkulima wa parachichi, heka moja ya parachichi yenye miche 80 mkulima mdogo mdogo ukimwezesha kupata miche bora, ukimwezesha kumpa miundombinu ya umwagiliaji, hiyo dola 7,000 anaifikisha kwa msimu huu, wala hasubiri 2050. Hujaenda kwa mkulima wa kahawa, hujaenda kwa mkulima wa alizeti na huku ndiko ambako umaskini upo mwingi, sekta ya kilimo ndiyo inayochangia kutengeneza ajira nyingi kwa vijana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mipango hii imewekwa sasa tuende tukatekeleze, Dkt. Samia Suluhu Hassan ana kiu ya kubadilisha kilimo kutoka kilimo cha kutegemea mvua mpaka twende kwenye kilimo cha uhakika cha umwagiliaji. Mungu ametujalia mito, mabonde, Mungu ametujalia ardhi yenye rutuba, sasa mipango yetu tuende tuka-implement tubadilishe hali ya kiuchumi ya Watanzania kupitia sekta ya kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepitia mpango umezungumzia 70% ni kuwekeza kwenye sekta binafsi, hapa pia unagusa kwenye economic zone. Nilikuwa ninapitia taarifa mbalimbali za kwenye Wizara ya Viwanda, leo hii maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji ni hekta 59,000 kwa ajili ya economic zone, hiyo ni pamoja na kwenye Wizara, taasisi, hii pia ni pamoja na Halmashauri na pamoja na TIC.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye TIC peke yake, kwenye special economic zone hekta zilizotengwa 17,000 lakini imetumika asilimia moja tu, hekta 1,600. Ukiangalia hayo maeneo yaliyotumika, ukienda kule Kwala, Bagamoyo, Nala, Benjamini Mkapa, impact yake ya kiuchumi ni kubwa. Sasa tumelipa watu maeneo makubwa, lakini bado hatujaamua kwenda kuwekeza kwenye viwanda, hii yote inaenda sambamba na ujenzi wa vyuo kila Wilaya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Sasa tunajenga vyuo kila Wilaya, tuna eneo kubwa la uwekezaji bado hatujalitumia, wananchi wamepisha maeneo, tunazungumzia kukuza uchumi wa Taifa letu, lakini haya maeneo lazima tukayawekeze, hizi ni hekari nyingi sana na nchi hii haijawa na uchache wa kuwa-convince wawekezaji waje wawekeze kwenye nchi yetu. Kinachohitajika wawekezaji wa ndani pamoja na nje ya nchi ni kuhakikishiwa mazingira mazuri ya uwekezaji. Wanahitaji kuona sheria zetu, bylaws zetu kwenye halmashauri ni rafiki, vilevile Mheshimiwa Waziri tunahitaji kubadili mentality ya watu, siyo kila mwekezaji mwizi, tuone wawekezaji wanaokuja nchini ni chachu ya kuchangia mabadiliko ya uchumi wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tubadilishe vilevile hali ya watendaji wetu kwenye maeneo yetu na huu mpango huu asilimia kubwa unakwenda kutekelezwa na TAMISEMI, mindset za Wakurugenzi wetu zipoje? Kazi yake pale ni kukimbizana na ujenzi na ukarabati wa madarasa na vyoo au Mkurugenzi ndiyo CEO wa kusimamia mabadiliko ya kiuchumi kwenye eneo husika?
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya yote yanapaswa kwenda sambamba katika kuhakikisha mpango huu unatekelezwa kikamilifu na Waziri amesema hatujawahi kuwa na tatizo la maarifa na kupanga mipango mbalimbali. Sasa Serikali ya Awamu ya Sita inataka kutekeleza kwa vitendo. Twendeni tukaongee na Watendaji kwenye maeneo mbalimbali waone hii dhamira ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ili maendeleo chanya na huu mpango uweze kutekelezeka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Saashisha alizungumzia jambo moja la kujenga miradi mbalimbali, tunajenga miundombinu mbalimbali, tunajenga madarasa, tunajenga shule, hivi hata siku moja tumeshawahi kufikiria kuwa na fungu maalum kwa ajili ya ukarabati? Hivi tunavyozungumza ni Bunge hili tulianzisha Mfuko wa Maji leo unafanya kazi kubwa sana, ni Bunge hili hili tulianzisha Mfuko wa Barabara, leo unafanya kazi kubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu fikiria ziwe shule maalum za wasichana zinazojengwa kwa zaidi ya bilioni nne kama hakuna pesa kwa ajili ya maintenance ndani ya miaka kumi zitakuwa kwenye hali gani? Mimi Jimboni kwangu nimefanya utafiti, kwenye shule za primary na shule za sekondari ambazo zimechakaa zinahitaji bilioni 1.6, imagine nchi nzima kwenye miundombinu tunayojenga nchi nzima, kwenye shule zetu tunazojenga nchi nzima, kwenye hospitali tunazozijenga zinagharimu kiasi gani? Tunajenga sana. Sasa kama Taifa ni jukumu letu kutenga pesa kwa ajili ya kulinda miundombinu yetu, kwa ajili ya kulinda shule zetu, kwa ajili ya kulinda hospitali zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ninashukuru sana. (Makofi)