Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Vijijini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. MASANJA K. KADOGOSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nianze kwa kushukuru kwa fursa hii, vilevile ninamshukuru Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono haya ambayo tunayazungumza kwa sababu mpango maana yake sasa tunawekwa katika namba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashukuru sana vilevile Waheshimiwa Mawaziri, Waziri wa Fedha, Waziri wetu wa Mipango na Uwekezaji Profesa kwa wasilisho zuri sana na la kitaalam lakini kubwa mawazo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Taifa ni vizuri tukajipongeza pamoja na kwamba tunayo safari ya kwenda. Nilikuwa ninasoma kitabu cha Mheshimiwa Benjamini Mkapa Marehemu (My Life My Purpose). Kufikiri kuanza kuwa na dira ya Taifa ilianza mwaka anazungumzia mwaka 1995, ndiyo mawazo yalianza hapo pamoja na kwamba ilichukua muda kidogo kabla hatujawa na mipango ya miaka mitano mitano, lakini tulianzia huko na wakati huo bajeti yetu, siyo bajeti kwa maana ya makusanyo yetu kwa wakati huo tunazungumzia takribani kama bilioni 334na point kadhaa. Huko ndiyo tulikoanzia na mpaka Mheshimiwa Mkapa anatoka alikua kwenye trilioni two point something, lakini sasa hivi tunazungumzia makusanyo kwa taarifa tulizopata hizo tulifikia above 34 trillion.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tulikotoka ni mbali sana. Kwa hiyo, ni vizuri sana kama Taifa tukawa proud kwamba kuna kazi kubwa sana imefanyika na mpaka hapa tulipofika na tunajenga sasa base kuanzia hapa kwenda mbele na ndiyo maana tunakuwa na jeuri ya kusema sasa tunauendea uchumi wa dola trilioni moja ni kwa sababu kuna bases ambazo zimetangulia na watangulizi wetu, wazee wetu wamefanya kazi kubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukianza na Baba wa Taifa kwa maana ya ujenzi wa Taifa moja, hii imetupa base nzuri sana ya kuzungumza haya makubwa tunayoyazungumza, ukija ‘Mzee Ruksa’ amefanya kazi kubwa sana ya kufungua uchumi kwa maana ya kwamba tuwe na uchumi ambao unakaribisha na private sector.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mzee Benjamin Mkapa na pengine jambo moja ambalo ni la muhimu sana, TRA mnayoiona hii wazo lilianzia kwa ‘Mzee Ruksa’ alipounda President Commission na baadaye Mzee Mkapa alipokuja akai-pick up then tukawa na TRA. Wakati wa Mheshimiwa Benjamin Mkapa kuna institutions nyingi sana zilitengenezwa kwa ajili ya ujenzi wa uchumi. Ukizungumzia TANROADS sijui TRA na hizi institutions nyingi ambazo tupo proud sasa hivi kama regulators zimetengenezwa wakati huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile hata BOT Act kwa sababu kwa historia ni kwamba hata ukizungumzia kwa mfano monetary policy ilikuwa part ya department ndani ya Wizara ya Fedha, mambo ya pension lakini then zikatengeneza institution.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninachosema ni nini? Kwamba kama Taifa tumetoka mbali na kuna mambo ambayo yamefanywa ya msingi kuanzia wakati ule, ukianzia kwa Mzee Mkapa kama nilivyosema, kwa Mzee Jakaya Mrisho Kikwete, tumejenga shule za Kata nchi nzima, jambo kubwa sana kwa Taifa. Tumejenga UDOM, tumejenga diplomasia wakati huo ilipanda sana upande wa diplomasia. Tulikuwa na Marais watatu kwa wakati mmoja, Rais wa Marekani ambaye yupo madarakani, Msaidizi wake ambaye alimtangulia na Rais wa China alikuja hapa ku-launch mipango ya Afrika, kwa maana ya Afrika na China.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kusema ni nini hapa? Kuna mambo makubwa ambayo yamefanyika kama Taifa ni lazima tuwe proud na ndiyo maana sasa hivi tunaweza tukazungumzia mambo makubwa. Nimezungumzia Jakaya Mrisho Kikwete, lakini amekuja Magufuli amefanya mambo makubwa sana, tumeanza SGR, tumeanza ujenzi wa Bwawa la Nyerere, tumehamia hapa Dodoma, hivi vitu vyote kama Taifa inatufanya tujiamini tunakokwenda mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kenned alikuwa anazungumzia kuhusu ukomavu wa Taifa, upevu wa Taifa unapima uwezo wa kufikiri, ku-design na kusimamia mipango mikubwa katika Taifa, hilo tumeweza kulifanya na ndiyo maana kama Taifa sasa tunaweza tukasema tunasonga mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa, ukiacha mambo ya kuendeleza SGR alivyoikuta, mambo ya madaraja makubwa tuliyokuwa tunajenga vilevile Bwawa la Mwalimu Nyerere lakini na mambo mengine mapya ambayo ameanzisha, kama vile tunatoka Dodoma tunaenda Mwanza kwenye SGR, tunatoka Dodoma tunaenda Kigoma, tunatoka Dodoma tunaenda Burundi. Haya ni maamuzi makubwa sana kwa kiongozi, yanahitaji uzalendo na yanahitaji uthubutu mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuzungumza hayo, kwa sababu ninataka tuanze kwanza kwa kujipongeza na kujua kwamba kuna kazi kubwa sana imefanyika katika Taifa hili, kuna baadhi ya watu wanaweza wakazungumzia katika akili yao inavyowatuma, lakini Taifa hili tumefanya mambo makubwa sana na tuna uwezo sasa wa kufikiri mambo makubwa ya kufanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nizungumzie mambo matatu ambayo hasa katika mchango huu, kwa maana ya mpango wetu kwa mwaka mmoja, miaka mitano na miaka 25. Vilevile kabla sijaanza hapa tulianza na kuzungumzia hotuba ya Mheshimiwa Rais. Kwa hiyo, nini maana yake? Maana yake ni kwamba tunapoanza kuzungumzia mpango ni muhimu ika-reflect consistency ya kile Rais alichokizungumza. Kwa hiyo, tunategemea kwamba mipango yote izungumze na hotuba ya Rais, kwa hiyo, consistency izungumze kila mmoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna sehemu moja ambayo ninafikiri Profesa inabidi wakaliangalie. Kwa mfano, mpango wa muda mrefu wa miaka 25, tunazungumzia target yaku-archive inter-model, lakini hotuba ya Rais inazungumzia multi-model transport system.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi vitu viwili ni tofauti. Multi-model transport system katika logistics ndiyo system ya hali ya juu ambayo nchi inatakiwa kwenda huko. Kwa maana nyingine ni kwamba lazima kuwe na consistency kwa sababu haya ni makabrasha ambayo yanaishi, inawezekana watekelezaji wa sasa hivi wasiwe watekelezaji baada ya miaka mitano wakaja watu wengine. Kwa hiyo ni lazima tuweke mambo yetu vizuri tuwe na consistency.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninazungumzia ukurasa wa 145-149. huku tunazungumzia inter-model unapo-refer inter-model, what’s the difference between the inter-model na multi-model? Hii inazungumzia kufungamanisha kwa maana kuna modes mbalimbali, unafungamanisha vipi? Maana yake unakuwa na contract moja. Kwa wale wa zamani kidogo hapa na mimi nimeshakuwa muhenga kidogo. Zamani mlikuwa mnatoka kutoka Bukoba mnakuwa na tiketi moja unapanda meli, unakuja kwenye reli unatumia tiketi hiyo hiyo, unashuka pale Itigi, unatumia tiketi hiyo hiyo kwenda huko Kyela kwenye mabasi. Sasa hiyo at least ina-come a little bit closer, but it is not real reflection ya multi-model.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninachosema ni nini? Hizi document lazima zizungumze, try to speak to each other, kuwe na consistency, lakini kuna wakati mwingine kuweka timeline, unasema unataka kufanya transformation ya mindset ambayo ni jambo kubwa sana katika nchi, kama tutaenda katika mambo haya ya kubadilisha mtazamo wetu, ni wakati gani unataka tukamilishe? Unapoweka 2050 wakati ni kitu muhimu tunapoanza utekelezaji then kunakuwa kidogo na mushkeli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninataka kuzungumzia namba zinasema nini? Namba zinazungumza na bahati nzuri katika ripoti ukianzia Profesa amezungumza vizuri sana, kwamba mpango wetu tuta-fund kwa trilioni 477 na 70% ya hiyo comes from private sector na only 30%, now ukirudi mpango ulioisha tulikuwa na trilioni 114, trilioni 40 zilikuwa zinatoka kwenye private sector na the rest zilikuwa zinatoka kwenye public, maana yake kuna shift.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hapa Profesa amezungumza vizuri sana, tunahitaji shift kubwa ya sera, sheria na kanuni ndani ya Serikali, sasa to what extent? Is it 70%, 60%, 50% shift? Sasa hilo ni suala la kuangalia katika utekelezaji. Kwa hiyo, ninafikiri nizungumzie katika hilo na ninampongeza sana Profesa kwa kuliona hilo kwa sababu it takes guts, unajua mtu mwingine unapozungumza private sector, now has to drive, mwingine anaweza akaja na scenario ya kusema, sasa tunataka kuachana na ujamaa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujamaa haina maana ya umaskini! Watu kwa mfano wa China, ninafikiri Rais wa China wakati huo alikuja na slogan ya kusema kama cat eeh? I don’t care, it doesn’t matter kama cat is black or white so long as anaweza kukamata panya! That was a shift katika policy za Kichina.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ni la mwisho, mipango hii inahitaji pesa, sasa ni lazima tuwe innovative. Tunapozungumzia private sector kuwa part ya ku-fund mipango yetu ya miaka mitano 70%, tunazungumza PPP. Maana yake ni nini? Ni lazima kuwe kuna total change ya the way tunavyoangalia funding organisation kwa mfano Wizara ya Fedha, yawezekana structure uliyonayo inatakiwa ibadilike. May be the biggest department now tunapozungumzia Wizara ya Fedha inaweza ikawa ni bajeti lakini kwa ujio huu yawezekana tukawa na total change ya namna ambayo tunavyo-organize katika funding.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la ku-fund pengine kwa kutumia future asset, tuseme labda madini. Tunafanyaje kuona kwamba haya madini tuna-leverage…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Mheshimiwa muda wako umeisha.
MHE. MASANJA K. KADOGOSA: Okay, Mheshimiwa Mwenyekiti ninakushukuru sana. (Makofi)