Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Dr. Selemani Said Jafo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kisarawe

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza awali ya yote naomba kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, Mola ambaye ametuwezesha siku hii tunakuja kujadili bajeti ya Wizara ya Ulinzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa kazi kubwa anayoifanya, lakini kubwa hasa katika suala zima la kusimamia masuala ya amani, ulinzi na usalama katika nchi yetu. Mheshimiwa Rais, amejipambanua katika utawala wake unaona ameweka nguvu kubwa sana kuhakikisha Wizara hii inaendelea kufanya vizuri katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumpongeza sana Waziri, Mheshimiwa Dkt. Rhimo kwa kazi kubwa ambayo ameanza kuifanya ndani ya muda mfupi, lakini ameonyesha leadership nzuri, yenye hekima kubwa sana katika Wizara hili, lakini sambamba na hilo Katibu Mkuu, Dkt. Faraji Mnyepe ambaye nasema huyu ni encyclopedia ya Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni muda mrefu sana Katibu Mkuu huyu ameendelea kufanya kazi kubwa sana tumpongeza sana, Dkt. Mnyepe unaisimamia vizuri katika upande wa utendaji wa Wizara hii.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimpongeze sana Mkuu wetu wa Majeshi Jenerali Jacob John Mkunda kwa kazi kubwa unayoifanya katika suala zima kusimamia Jeshi letu, tunaimani kubwa, tuna heshima kubwa kama nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania inapozungumza, East Africa, Afrika, SADC tunaheshimika sana kwa sababu Jeshi letu liko imara na limekuwa saidizi kwa kiwango kikubwa sana katika suala zima kusimamia amani na migogoro Barani Afrika na maeneo mbalimbali, hakika Mkuu wa Majeshi hongera sana, sana, sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumpongeze Mnadhimu Mkuu wa Jeshi letu ambaye kwa kweli hekima yake naye ni kubwa Ndugu Salum Haji Othman, sisi Wajumbe wa Kamati tunamfahamu kwa hekima yake, weledi wake unaona kweli huyu ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi letu, hakika hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niwapongeze sana Mameja Jenerali wote, tukianza na ndugu yangu Rajabu Mabele wa JKT, hakika umefanya kazi kubwa. Leo hii tunaona JKT inavyofanya kazi kubwa katika Taifa letu hili na taasisi yetu ya SUMA-JKT ambayo hii tuna kila sababu sisi kama Wabunge tuwapongeze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Wakuu wote wa Kamandi mbalimbali na Vikosi na Wanajeshi wote katika Taifa letu.

Ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge, mimi ni Mjumbe wa Kamati, naomba niwaambie, katika Wizara hizi tuna kitu kinaitwa untold stories, lakini tukija kusema ni kwamba naomba tuwaaminishe Waheshimiwa Wabunge katika sehemu tunafanya kazi kubwa Wizara hii inafanya kazi kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kwa kazi kubwa ni suala zima tu la itifaki wa kawaida, lakini hapa alivyomaliza Mwenyekiti wetu wa Kamati tunasema ahsante basi Waziri njoo tumalize kumaliza hoja hii. Kwa sababu hii ni Wizara ya aina yake na kazi kubwa sana imeendelea kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa zaidi niiombe Wizara ya Fedha na hasa tunapopitisha bajeti niombe sana, hii Wizara tunasema ile first charge, tuhakikishe kwamba tunaiwezesha amani yetu, utulivu wetu na nchi yetu na heshima yetu ni suala zima la usalama. Nchi yoyote inapokosa kuwa na chombo chenye kusimamia usalama wa nchi, hakika nchi hiyo inaondoa heshima yake kama Taifa hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo sisi tushukuru sana Wizara hii na Jeshi letu, limeendelea kuwa imara kusimamia kwamba suala zima la amani na utulivu nchi yetu inaendelea kuwa vizuri. Kwa hiyo, niiombe Wizara ya Fedha tunapopitisha bajeti hapa na hususan bajeti ya maendeleo, tunaomba sana bajeti hii iende vizuri zaidi kama ilivyopangwa kusaidia vyombo hivi, chombo hiki kifanye kazi vizuri kazi yake ni kubwa sana. Kama nilivyosema kazi yake ni kubwa sana, naomba tuishie hapo kwanza kusema kazi yake ni kubwa sana, niiombe Wizara ya Fedha ihakikishe isaidie sana upelekaji wa fedha katika Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika upande mwingine niombe sana katika uwezeshaji wa fedha kuangalia katika mfano Jeshi letu, Mwenyekiti wa Kamati amezungumza hapa, kuna maeneo mengine yametwaliwa, kuna wakati mwingine kuna maneno mengi sana ya wananchi na migogoro mingi sana, tuliheshimishe Jeshi letu, tuiheshimishe Wizara, twende tukalipe fidia kuondoa ile hali kidogo wakati mwingine wananchi wanalitazama Jeshi katika sura siyo nzuri zaidi, niombe jambo hilo tulifanye vizuri na hasa Wizara ya Fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ikiwezekana twendeni tukaanzie pale Kisarawe tuna 2.5 billion pale kwa wale wananchi ambao wametoa eneo lao kwa Kikosi cha Jeshi Kisarawe twendeni tukatoe zile fedha, huu ndiyo utaratibu mzuri hivi tutakuwa tumeenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, otherwise mimi nishukuru sana na niwaombe Waheshimiwa Wabunge wenzangu tuunge mkono hoja hii kwa 100% basi kazi yetu iendelee na kazi na utu tunasonga mbele. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja ahsante sana. (Makofi)