Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Tunduru Kaskazini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
2
Ministries
nil
MHE. ADO S. ADO: Mheshimiwa Spika, awali ya yote niseme kwamba ninafahamu kwamba mjadala wa Wizara ya Ulinzi, siyo mjadala wa kawaida, ninafahamu. Ni mjadala nyeti wenye maslahi mapana kwa Taifa, kwa hiyo nitazungumza kwa ufupi na nitazungumza kwa mipaka inayohitajika. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, la kwanza jambo la kwanza ni juu ya maslahi ya maveterani wa vita ya Kagera. Kama inavyofahamika na nimesoma Hansard za Bunge lililopita katika mwaka wa fedha huu tulionao; Serikali ilitoa ahadi ndani ya Bunge kupitia Waziri aliyepita Dkt. Tax, kwamba kuanzia mwezi Julai maveterani wa vita ya Kagera ambao hawapati posho wataanza kulipwa rasmi posho na Serikali. Hiyo ilikuwa ni ahadi ya Serikali kwa mashujaa wetu...
SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, ninaongeza muda mpaka tumalize kazi yetu. (Makofi)
MHE. ADO S. ADO: Mheshimiwa Spika, hiyo ilikuwa ni ahadi ya Serikali kwa wapiganaji wetu, ahadi ambayo inajenga msingi kwa wapiganaji wa sasa kwamba wakienda mstari wa mbele wakapambana, watapewa tuzo, watatazamwa. (Makofi)
Mimi jimboni kwangu wazee hawa wapo, wengi wao umri wao ni baina ya miaka 70 mpaka 90, vikongwe lakini taarifa nilizonazo wanasema hawajaanza kulipwa.
Mheshimiwa Spika, sasa mimi ninataka Waziri atakapokuja kwenye majumuisho kwa kweli ninasita sana kuzungumza lugha ya kushika shilingi ila aje atoe maelezo kwamba Serikali ahadi ile kwa maveterani wa vita ya Kagera ilikuwa ni siasa ya maneno matupu na tunaweza kufanya siasa kwenye Wizara ya Ulinzi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mimi nina mapendekezo ya ziada, ninapendekeza ukiacha ahadi ile ya posho tufanye kama mtindo ambao baadhi ya nchi zinafanya, tuwe na mfuko maalum wa maveterani wa vita ya Kagera. Mimi ninapendekeza tuwe na mtindo kama wa The Kagera War Veteran Fund na nchi nyingine wanafanya, Marekani wanafanya, Afrika ya Kusini wanafanya, Uingereza wanafanya kwa mtindo tofauti tofauti. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, la pili ninakubaliana na Mheshimiwa Liwaka kwamba ni lazima tufanye sensa sio sensa ya kubaini idadi yao tu, tuangalie na hali yao, wanaendeleaje wazee wetu hawa waliopigana katika vita ya Kagera.
Mheshimiwa Spika, la pili na la mwisho; Jeshi la Wananchi ni jeshi la ukombozi wa Afrika, ni Jeshi la haki. Haikuwa kwa bahati mbaya jeshi hili lilipokelewa Uganda kwa shangwe, haikuwa kwa bahati mbaya jeshi hili lilipokelewa Kariakoo kwa shangwe, haikuwa kwa bahati mbaya Oktoba kwa yale yaliyotokea jeshi hili lilipokelewa kwa shangwe. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninatoa changamoto kwa jeshi, kuna kitu kimoja wakilinde kwa nguvu zote, kitu hiko ndio roho ya thamani yao; jeshi lijitenge na siasa, hicho ndio kitu wakilinde kwa nguvu zote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hivi karibuni vimekuwepo vidole na huwa wanasema kwa sababu jeshi bado ni chombo hata katika zama hizi ambazo tunasema utumishi wa umma umekuwa politicized bado imani ipo...
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)