Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Musoma Vijijini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. PROF. SOSPETER M. MUHONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuanza mchango huu. Waheshimiwa Wabunge yote tuliongea kwenye mambo ya mipango sasa hii Wizara ndiyo Wizara husika kweli kweli. Mataifa yote duniani mambo ya uchumi na ustawi wa kila Taifa, unategemea nishati. Kwa kuwa mambo yake ni mazito na ni mazuri, leo mchango wangu utakuwa kuhusu uzalishaji wa umeme; mambo ya usafirishaji, usambazaji na mambo ya gesi asilia hayo tutatafuta siku nyingine kwa sababu muda hautoshi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niwaeleze vilevile ndugu zangu historia ya TANESCO ambayo ndiyo inatoa umeme na kusambaza. Enzi za ukoloni ilikuwepo DARESCO ilikuwa inatoa umeme kwa ajili ya Dar es Salaam, halafu ilikuwepo TANESCO Tanganyika ya mwaka 1961, lakini ilikuwa inahudumia wale viongozi wetu wa Kikoloni. TANESCO mpya imeanzishwa mwaka 1964 na inafanya vizuri. Ina mizigo mizito lakini inafanya vizuri na vizuri zaidi ni REA. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kusema kweli REA lazima tuipongeze sasa. Tunaipongeza Serikali yetu na bajeti inavyozidi kuendelea. Tulikuwa kwenye mabilioni tukaja kwenye shilingi trilioni moja leo hii naona wamefika shilingi trilioni 2.6. Hongera kwa Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuongeza bajeti ya hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kujadili uzalishaji wa umeme ninaweza tu nikawaeleza tutazalisha kutoka hapa, hapa, hapa, hapa itakuwa haina maana, ni lazima niende na mifano iliyofanikiwa na iliyokuwa inafanana na sisi. Wabunge wasisahau kwamba mapinduzi ya kiuchumi ya viwanda, first industrial revolution ya mwaka 1760 mpaka 1860, hiyo miaka 100 ya kwanza. Mapinduzi haya makubwa yalitegemea nishati na teknolojia kubwa ilitegemea makaa ya mawe kuchemsha maji ili kupata engine zinazotumia mvuke (steam engine). Kwa hiyo, unaona hapa first industrial revolution bado ilikuwa ni nishati. Second industrial revolution 1870 mpaka mwaka 1960 ndiyo tumeanza mass production. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kilicholeta mafanikio hayo nayo ni ugunduzi wa umeme (nishati). Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge nimechukua nchi ambayo tulikuwa tunafanana nayo imefanikiwa na ndivyo nitakavyotoa vyanzo vyao vya uzalishaji wa umeme na kupendekeza vyanzo vya uzalishaji wa umeme wa Tanzania. Kwanza Mheshimiwa Waziri amefanya vizuri nimemsikia anataja vyanzo, yuko sahihi kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaongezea hapo, nimetoa mifano ya nchi mbili ambazo kila mara na tunazifuatilia duniani. Wanasayansi wanazifuatilia kweli kweli India na China, lakini kwa ajili ya muda leo hebu niende na moja, nikienda na mbili muda hautatosha, halafu kama nilivyowaeleza inabidi wapige makofi taratibu huku wanachukua na takwimu. Kwa hiyo mapinduzi makubwa ya China yalifanywa baada ya Mao kufariki, aliyekuja yule Ding mwaka 1978 ndiyo mapinduzi makubwa kweli kweli ya uchumi wa China. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kabla ya mwaka 1978 Uchumi wa China ukuaji wake ulikuwa kama uchumi wa Tanzania wa asilimia sita (growth). Ilikuwa asilimia sita inakwenda, inashuka, inakwenda, inashuka kama wa Tanzania ulivyo sasa hivi. Hiyo China ilikuwa kabla ya 1978, baada ya 1978 uchumi wao ukakua kwa kasi kubwa sana kwa zaidi ya 10%, wakati mwingine ulifika 15%, ndiyo maana mlisikia ninapendekeza kwamba Dira yetu ya Maendeleo kufanikiwa lazima uchumi ukue kwa zaidi ya 10% kufikia hiyo trilioni moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mwaka 1978 GDP per capita ya China ilikuwa dola 156, lakini umeme waliokuwa wanatumia mtu mmoja mmoja, consumption of electricity per person per annum ilikuwa kilowatt 255, karibu tunalingana hapo. Hata hivyo, miaka 48 toka 78 mpaka leo GDP yao imeenda zaidi ya dola 14,000 na matumizi ya umeme ya mtu mmoja mmoja yameenda zaidi ya kilowatt yaani unit zaidi ya 7,000, tunafanana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Tanzania kabla sijapendekeza vyanzo hali yetu ilivyo tulikuwa na ile Vision 2025 tulisema kufika mwaka jana tulivyokuwa tumejipangia GDP per capita iwe dola 3,000 na capacity yetu ya kuzalisha umeme nchi nzima iwe zaidi ya megawatt 10,000. Hivyo tulijipangia hivo kufikia mwaka jana. Tulikuwa tunatoka megawatt 1,500 mpaka megawatt 10,000. Sasa kilichopo mbele yetu 2,050, tunasema tunataka kupata GDP per capita dola 7,000.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuja bado sijafikia hata mapendekezo yale, twende polepole. Sasa hapo wanakula muda wangu wapunguze na kweli yeye ndiye amesema, safi kabisa Mheshimiwa Musukuma. Sasa GDP 7,000 ndiko tunakokwenda, trilioni moja na umeme wetu sasa hivi ni megawatt takriban 4,400 na matumizi ya umeme ya mtu mmoja mmoja ni unit 243. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyowaeleza China walikuwa kama sisi wamefanikiwa na sisi nao tunaweza kufanikiwa, hiyo ni point ya muhimu kwamba kufanikiwa tunaweza. Sasa kutokana na hiyo, ninatoa mapendekezo ya vyanzo vya uzalishaji wa umeme. Tunahitaji umeme mwingi, tunahitaji umeme wa bei nafuu, tunahitaji umeme unaotabirika kwamba upo. Tutakavyokaribia 2,050 tutaingia kwenye uchumi wa kutumia data center, hatuna data center hata moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, data center moja inatumia karibu megawatt 100, hatuna hata moja. Kwa hiyo, ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge umeme haujatosha, tumejitahidi lakini haujatosha. Kwa hiyo, ninaongelea umeme wa kuelekea 2,050 vyanzo: kikundi cha kwanza ni none fossil yaani jadidifu green economy, ninapendekeza tuwekeze sana kwenye umeme jua (solar).
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa China 20% ya umeme wao sasa hivi ni wa solar wana asilimia, ndiyo maana sisi tutatumia asilimia tusilinganishe na wingi sisi ni wadogo lakini shares percentage inabaki pale pale. Umeme wao sasa hivi China wa jua ni 26% wanazalisha gigawatt 1,232 kwa hiyo muwe mnazidisha na 1,000 kupata megawatt, nibaki kwenye gigawatt huku. Tanzania kwa solar nimemsikia vizuri Mheshimiwa Waziri, ninashukuru ule wa Shinyanga umeanza kazi tulikuwa na megawatt 15 tumeongeza megawatt 50. Kwa hiyo, tuzidi kuzalisha umeme kutoka kwenye jua kwa sababu jua likiwaka sana unapata watts 1,000 kwa kila square meter moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, cha pili umeme wa upepo. China sasa hivi nchi nzima umeme wao uwezo wake ni 13% wana gigawatt 498 zidisha mara 1,000 upate megawatt. Tanzania upepo hatujapata lakini spidi ya upepo inayoweza kuzalisha umeme inatakiwa iwe meta 11 kwa sekunde kama ile ya pale Same na ile ya kule Makambako. Kwa hiyo twende kwenye upepo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, cha tatu hydro (maji) hii tunayo tayari. Kwa sasa hivi China 13% ya umeme wao ni hydro, wana gigawatt 498. Sisi ndio chanzo kikubwa cha umeme wetu kwa zaidi ya 68% tuna gigawatt 2.7 yaani megawatt 2,800 hivi, tuongeze kwenye maji. Ukitaka kujua kwamba kweli maji yanazalisha umeme mwingi duniani ulikuwa unatoka Three Gorges kwa wale ambao wameenda China. Huo mtambo mmoja ulikuwa unazalisha gigawatt 22, yaani megawatt 2,500; linganisha na bwawa la kwetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi wanajenga jipya kabisa kule Tibet, litazalisha gigawatt 60 yaani wanazalisha wanajenga mitambo ya kuzalisha megawatt 60,000 kutoka kwenye bwawa moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, chanzo kingine cha nne, ninakaribia kumaliza nilipewa muda …
MWENYEKITI: Nimekuongezea dakika tatu.
MHE. PROF. SOSPETER M. MUHONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, dakika tatu, haya ninamalizia. Chanzo cha nne ni nuclear, kwa sasa hivi China wanazalisha gigawatt 125 kwa nuclear ambayo ni 1.5% ya umeme wao, sisi hatujaanza na ndiyo tunaanza pale Mkuju, tuna uranium nyingi katika maeneo mengi nchini likiwemo lile la kule Namtumbo ambapo tuna kama tani 60,000. Kwa hiyo, twende kwenye nuclear.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namba tano biomass; kwa China ni asilimia 1.3 ya umeme wao wote unatoka biomass ambayo ni gigawatt 50 yaani megawatt 50,000, sisi ya kwetu tuna megawatt 20.5 karibu ni 0.52. Kwa hiyo, tuongeze kwenye bio energies.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namba sita ni geothermal na Tanzania tumeanzisha kampuni ya geothermal, lakini China asilimia 1.2 ya umeme wao unatoka kwenye geothermal ambayo ni gigawatt 46 na umeme wa dunia ya sasa unaitwa ni ule battery storages, wanatunza umeme kwenye battery halafu baadaye wanautumia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, chanzo cha pili, kikubwa sasa ndiyo fossil fuels, namba nane ni natural gas. Sisi Tanzania tunazalisha zaidi ya 28% ya umeme wetu ni natural gas ambayo karibu ni 1.1 gigawatt zaidi ya megawatt 1,000. China ni 2.8% of the total installed capacity, inatoka kwenye natural gas ambayo ni gigawatt 150.
Mheshimiwa Mwenyekiti, chanzo cha tisa ni makaa ya mawe (coal); China ni zaidi ya gigawatt 1,100 ambayo ni 31% ya umeme wa China wote. Sisi tulikuwa na megawatt 10 kule Mbeya umeenda unapotea, lakini reserve yetu ya makaa ya mawe ni zaidi ya tani bilioni tano ya makaa ya mawe tuliyonayo Tanzania, lakini hatuna hata megawatt. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni petroleum ambayo China wanaachana nayo, sisi tuna megawatt 103 ambayo ni karibu 2.6% ya umeme wetu wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hivi ndivyo vyanzo 10 ambavyo tunapaswa kuongeza kuzalisha umeme tupate umeme mwingi wa bei nafuu na unaotabirika. Bei ya sasa ya senti tisa za Marekani kwa unit tukiwa na umeme mwingi na tukitaka kufanya mageuzi ya viwanda lazima tushushe umeme wetu uje kwenye bei ya senti sita mpaka saba za Marekani mengine tutaongea siku nyingine. Ahsanteni sana. (Makofi)