Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

Hon. Mariam Madalu Nyoka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027

MHE. MARIAM M. NYOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Kwanza, ninaipongeza Serikali ya Awamu ya Sita ikiongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na ninaipongeza Wizara kwa hotuba yao nzuri ya bajeti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitachangia kwenye zao la mahindi Mkoani Ruvuma. Mkoa wa Ruvuma tunapata mbolea za ruzuku na pia tunapata mbegu. Hata hivyo, ninaiomba Serikali kupitia Wizara yake iandae utaratibu kwa wataalam wetu kupita mashambani ili wapate takwimu sahihi za wakulima ili mahitaji ya wakulima yaendane na mahitaji yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna changamoto kwenye zao letu hili. Serikali inanunua mahindi kupitia Wakala wake wa NFRA, lakini hawanunui mahindi yote kulingana na uwezo au labda sijui utaratibu wao ambao wamejiwekea. Mahindi yale yakibaki yananunuliwa na walanguzi, hivyo kusababisha walanguzi wale kupanga bei ambayo iko chini kwa mkulima na ambayo haimnufaishi mkulima wetu. Ninaiomba Serikali, kutokana na NFRA kuwa na uwezo usiokidhi kununua mazao yote, basi kuwe na soko huria ili mkulima aweze kuuza mazao yake popote pale ili awaze kupata manufaa kwenye mazao yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto nyingine ni Serikali kuchelewesha malipo ya mazao kwa wakulima wetu. Ninaiomba Serikali iwalipe wakulima kwa wakati kwani kuchelewesha kuwalipa wakulima hawa kunasababisha kushindwa kulima kwa wakati na kukosa pembejeo. Hali ambayo inasababisha msimu mwingine wa mazao kuchelewa kulima kwa ajili ya ukosefu wa fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaiomba Wizara kupitia wataalam wake, ni vyema wakazalisha mbegu za kutosha ndani ya nchi. Tena ziwe mbegu zenye ubora na zipatikane kwa bei nafuu. Kutegemea nje inakuwa siyo sawa, hata hivyo, tunaona madhara ambayo tunayapata hata sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, ninaiomba Wizara iandae utaratibu wa kufanya ukaguzi wa maduka ya pembejeo mara kwa mara ili kuweza kubaini mbegu na viuatilifu visivyo na ubora na vilivyopitwa na wakati wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuunga mkono hoja. Ahsante. (Makofi)