Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kasulu Vijijini
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. EDIBILY K. KINYOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kuniona ili niweze kutoa mchango wangu kwenye Wizara ya Kilimo. Kwanza ninawapongeza Wizara, nimeona mikakati waliyonayo kwenye kilimo, mikakati hiyo kama wakiitekeleza inaweza ikatutoa hatua moja na hatimaye ku-boost uchumi wetu, kwa maana ya GDP.
Mheshimiwa Naibu Spika, uchumi wetu kwa 60% umeajiri watu kwenye sekta ya kilimo. Sekta hii ya kilimo inachangia zaidi ya 23.3%, kwa mujibu wa World Bank, kwenye pato la Taifa letu na pia, zaidi ya 20% kwenye export, kwenye mauzo ya nje. Maana yake ni kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninayo machache ya kuchangia. Ukiangalia uchumi wetu kwa asilimia 42.9 umejengwa na shughuli za msingi (Primary activities), kwa asilimia 19.7 shughuli za upili (Secondary activities) na tertiary activities kwa asilimia 37. Hii inaashiria nini? Ni kwamba, kilimo ndiyo chenye mchango mkubwa kwenye uchumi wetu. Sasa hii nayo ina athari zake, maana kikitokea chochote kwenye kilimo, uchumi wetu una hatari ya kwenda kuanguka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, miaka ya 1970 uchumi wetu ulianguka kutokana na ukame uliojitokeza kwenye Taifa letu. Kama tunataka kukipeleka kilimo chetu mbali, kujenga uchumi wetu na kuhakikisha kwamba, tunafikia Dira yetu ya 2050 ya kuhakikisha tunafikia pato la shilingi 1,000,000,000,000 lakini pia, dola 7,000 kwa capital income, ninashauri tuwekeze kwenye viwanda vya kuongeza thamani mazao yetu ya kilimo. Tutoke kwenye stage ya uchumi wetu kuchangiwa na shughuli za msingi, kuuza mazao ghafi, tuuze mazao ambayo yameongezwa thamani; maana yake ni tujenge viwanda. Viwanda hivi vitatusaidia masoko na vitatuongezea ajira. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa takwimu 2002, kwa mujibu wa Wizara ya Viwanda, kulikuwa na viwanda zaidi ya 50 vilivyoanzishwa, lakini vilivyoweza ku-survive ni viwanda 23 tu. Tuna viwanda vingi ambavyo vilikufa, viwanda vya textile, viwanda vingi vya kutengeneza nguo. Kwa mujibu wa bodi pia, 80% kwenye zao la pamba wanauza nje, maana yake sisi tunazalisha kitu ambacho hatukitumii, ninaishauri Wizara tuwekeze kwenye viwanda ili viende vika-boost mazao yetu tunayolima, wananchi wetu wanaolima tuweze kuhakikisha soko lipo la uhakika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimeona pia kwenye zao la muhogo, Mheshimiwa Waziri anisaidie kiwanda cha kuchakata zao la muhogo pale Kasulu Vijijini, tuna shida ya kiwanda.
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa ahsante sana.
MHE. EDIBILY K. KINYOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na ninaomba kuunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri. (Makofi)